Mama Erick Kabendera ni aina ya wamama adimu sana, wanawake wenye maono makubwa

Mama Erick Kabendera ni aina ya wamama adimu sana, wanawake wenye maono makubwa

Ndio uwafundishe watoto wako wasiuze utu wao kwa malipo.

Maandishi ya uongo anayoandika Kabendera leo, ndio aina ya uongo huo huo uliomletea shida huko nyuma.

Halafu unaitungia uongo nchi kwenye magazeti yanayosomwa na potential investors, mafisadi yatengeneze story.
Kwa nini hawakumpooza na kumfanya awe kama Cyprian Musiba??
 
Ndio uwafundishe watoto wako wasiuze utu wao kwa malipo.

Maandishi ya uongo anayoandika Kabendera leo, ndio aina ya uongo huo huo uliomletea shida huko nyuma.

Halafu unaitungia uongo nchi yenye kwenye magazeti yanayosomwa na potential investors, mafisadi yatengeneze story.
Tuambie uwongo wa kabendera ni upi halafu ww utuandkie ukweli au ukweli ni ule kpnd cha shetan magufuri tuliambiwa wapnzan wanatuchelewesha leo wapo ccm peke yao na hakuna jipya na yale magawio fake ya mashirika nk ndo ukweli unaoutaka au
 
Unakwama sana kuchanganya mambo ya kiroho na kimwili punguza chuki kwa wanaoamin mambo ya rohoni kuptia mtu fulani hao wana changamoto ambazo wanaamin znatatulika kiroho huko kwa mwamposa wewe si kweli kwamba una akili kushnda watu wote wanaoenda pale wengne ni matajiri kwao ww ni kapuku tu wengne ni wasomi wakubwa kwao ww ni kilaza tu
Mbowe alikuwa Kwa Mwamposa juzi 😀
 
Tujadili Mambo ya msingi!
Muda ni mfupi mambo ni mengi!
Tuna uchaguzi wa chadema
Tuna uchaguzi mkuu 2025
Tuna shida ya Barabara mbovu
 
Kwa nini hawakumpooza na kumfanya awe kama Cyprian Musiba??
Kila mtu na kazi yake, kwani unadhani Musiba ni mtu alieamua kuwehuka tu from nowhere.

Wengine tuishi kwa calculated risks na kupima madhara yake (usiige watu) usio wajua wengine wana nguvu nyuma yao, ya kupambana hata na hakina Membe.

Vinginevyo uwezi itungia nchi uongo kwa malipo, tena kupitia reputable news sources huko kwa wazungu, ukabainika uchekewe.

It doesn’t work that way, hata huko kwao.
 
Tujadili Mambo ya msingi!
Muda ni mfupi mambo ni mengi!
Tuna uchaguzi wa chadema
Tuna uchaguzi mkuu 2025
Tuna shida ya Barabara mbovu
Waambie mashabiki wa Yanga na Simba.
 
Erick Kabendera anasema mama yake alikuwa mwalimu wa enzi za ukoloni na ndiye aliyemfundisha yeye na kumpa ujuzi mwingi wa Kingereza, Historia na Uandishi. Anasema nyumbani kwao kulikuwa na maktaba kubwa ambapo walikuwa wanasoma vitabu vingi sana pamoja na mama yake.

Kabendera anasema hata wakati anakamatwa walikuwa wanajadili Historia ya mataifa ya maziwa makuu na mama yake mwenye miaka 80! Alimpomtembelea mahakamani alihuzunika sana jinsi watu walivyokuwa wananyang'anya haki zao na watu wengine wako kimya tu.

Anasema wakati wa vitu kuu ya pili ya dunia mama yake alitaka kwenda kusoma nje ya Kagera lakini kulikuwa na amri ya wakoloni kuwazuia wanawake wasitoke ndani ya Kagera kwasababu walikuwa wanatorokea Nairobi ambapo inadaiwa walikuwa wanaenda kujiuza na kurudi na magonjws, mama yake na mwanamke mwingine waliandamana kwa mkuu wa wilaya kupinga amri iliyowazuia wanawake wa Kagera kusafiri nje ya Kagera na wakaruhusiwa kusafiri.

Hakika Kabendera alipata mama bora, labda ndio maana inaonekana hana viashiria vya Utanzania. Wamama wengine wa kibongo kipaumbele kwa watoto wao ni kwa Mwamposa, Sunday School, mafundisho ya komunio au Madrasa na wa kike kuolewa. Sifa kubwa ya wamama wengi wa kibongo wakielezewa na watoto wao ni wacha mungu na waliowafundisha maadili. Mama yake Kabendera aliamua kumnoa mwanae katika elimu dunia.
Huyu jamaa alinyimwa haki ya kumzika Mama yake.
 
Katika mambo yaliyonifanya nimchukie kabisa Magufuli ni ile video ya Mama Kabendera akilia kumuombea msamaha mwanaye, nililia mno!

Mama Kabendera apumzike kwa amani, kijana hodari aliyemlea vyema anaushangaza ulimwengu hii leo.

Kuna wengi tu ambao wamefungwa na kuacha watu wengi wanaowategemea nyuma yao. Je nao wakitoa klip za kumuomba rais msamaha wa kuwaachia kutoka kolokoloni hali ingekuwaje?

Tatizo mnaangalia upande mmoja tu kwamba Kabendera kafungwa. Lakini hamuangalii upande ule muhimu wa kosa lake la kuiumiza nchi. Alikuwa akiichafua nchi kwa mabeberu kwa vipande vya fedha. Halafu mnaona kaonewa. Jambo alilofanya Kabendera halikubaliki popote duniani.
 
Sio sawa kuwafunga watuhumiwa kabla hata ya kupewa hukumu na mahakama.
 
Tupe muamala wa wazungu kwenda kwa kabendera una ushahidi nadhan
We nawÄ™ ndio unaamka, ushaambiwa Kabendera ni freelance writer (analipwa) per article.

Kama ulikuwepo JF from 2015 kulikuwa na mada luluki kutoka ‘The Economists’ na hao wengine ambao wanamtambua kama contributor wao (The Times na The Guardian.

Alikuwa anaichafua serikali huko kwa kutumia pseudonym mpaka alipotajwa jina lake halisi humu JF muhusika ni Kabendera na member ambae ni active (you should have this details, kabla ya kuchagua upande).

Freelance writer analipwa per article kwa wanaochapisha nakala zake au unadhani alikuwa anaandika bure.
 
"...... hata alipomtembelea mwanae gerezani alihuzunika sana" mwisho wa kunukuu dah! Mama alifariki kwa maumivu makali sana kabendera nae hakuweza kumuaga mamaye
 
Amekuwa mkimbizi sababu nchi aliyokuwepo hawapendi ukweli, mama alimlea mwanae katika ukweli na haki ambalo ni kosa lililompelekea mwanaye kesi na kushikiliwa kinyume cha haki.

Mama Kabendera ni mfano kwetu sisi wanawake, tunapaswa kuwalea watoto wetu kama alivyomlea mwanaye Eric ili kuleta mageuzi ya fikra kwa vizazi vijavyo.

Umenena vyema. Mfundishe mwanao ukweli ili umuweke huru. Lakini usiache pia kumfundisha hekima na pia hasara ya usaliti ili awe salama. Hata vitabu vinatuasa usiwe mtakatifu au mwema kupita kiasi ili uwe salama.
 
Katika mambo yaliyonifanya nimchukie kabisa Magufuli ni ile video ya Mama Kabendera akilia kumuombea msamaha mwanaye, nililia mno!

Mama Kabendera apumzike kwa amani, kijana hodari aliyemlea vyema anaushangaza ulimwengu hii leo.
Magufuli karma itamtesa sana. atakuwa case study wa karne hii
 
Erick Kabendera anasema mama yake alikuwa mwalimu wa enzi za ukoloni na ndiye aliyemfundisha yeye na kumpa ujuzi mwingi wa Kingereza, Historia na Uandishi. Anasema nyumbani kwao kulikuwa na maktaba kubwa ambapo walikuwa wanasoma vitabu vingi sana pamoja na mama yake.

Kabendera anasema hata wakati anakamatwa walikuwa wanajadili Historia ya mataifa ya maziwa makuu na mama yake mwenye miaka 80! Alimpomtembelea mahakamani alihuzunika sana jinsi watu walivyokuwa wananyang'anya haki zao na watu wengine wako kimya tu.

Anasema wakati wa vitu kuu ya pili ya dunia mama yake alitaka kwenda kusoma nje ya Kagera lakini kulikuwa na amri ya wakoloni kuwazuia wanawake wasitoke ndani ya Kagera kwasababu walikuwa wanatorokea Nairobi ambapo inadaiwa walikuwa wanaenda kujiuza na kurudi na magonjws, mama yake na mwanamke mwingine waliandamana kwa mkuu wa wilaya kupinga amri iliyowazuia wanawake wa Kagera kusafiri nje ya Kagera na wakaruhusiwa kusafiri.

Hakika Kabendera alipata mama bora, labda ndio maana inaonekana hana viashiria vya Utanzania. Wamama wengine wa kibongo kipaumbele kwa watoto wao ni kwa Mwamposa, Sunday School, mafundisho ya komunio au Madrasa na wa kike kuolewa. Sifa kubwa ya wamama wengi wa kibongo wakielezewa na watoto wao ni wacha mungu na waliowafundisha maadili. Mama yake Kabendera aliamua kumnoa mwanae katika elimu dunia.
Mama mjinga alizaa toto lijinga lijinga hakulifundisha uzalendo. Ajue historia yake na jina lake limeshajifuta anga za Tanganyika, akatafute urais nchi nyingine.
 
taarifa zilizozagaa zilionesha wewe ndo ulinyetisha neno kaflag kutoka gazeti la uingereza la economy kwenda viungani ikulu..kwamba mwenye jinal kaflag ..ni yeye ...zakweli hizo

Nakumbuka bro Pascal Mayalla alilishukia gazette la The Economist kwa kuandika mambo ya uongo na ya kuichafua serikali. Yeye hakuandika kuhusu Kabendera na wala hakuna aliye dhani ni yeye. Licha ya kuwa mwandiko, lugha, mtiririko wa mawazo nk ilionesha kabisa kwamba mtunzi na muandishi wa makala ile ni mwenyeji wa eneo husika. Kwa hiyo Pascal alifanya kitu ambacho wengi walifikiria. Kupinga makala zile.
 
Back
Top Bottom