Mama Feisal jitokeze mbele ya kamera uombe radhi Viongozi na Mashabiki wa Mpira kwa kuzungumza mambo ya uongo

Mama Feisal jitokeze mbele ya kamera uombe radhi Viongozi na Mashabiki wa Mpira kwa kuzungumza mambo ya uongo

Mama ameonekana ana akili ndogo mpaka inahuzunisha. Hivi katika hali ya kawaida kabisa unapataje hela ya kununulia sukari ili ulie na ugali, halafu ukose hela ya kununulia mboga za bei nafuu kabisa kama bamia, nyanya chungu, mchicha, dagaa, nk. ili kulia na huo ugali!!

Mbaya zaidi hakuna mji wenye bei nafuu ya chakula kama Dar!! Yaani kabisa ulipwe milioni 4 kwa mwezi, halafu ushindie ugali na sukari!! Kuna watu hapa duniani hawana hata shukrani.
Mama alisema Feisal anategemewa na ndugu zake, pesa zote zinaishia kwa kulipia gharama za shule na mavazi kwa ndugu zake

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mungu awatie nguvu wapambanaji wenzangu katika kutafuta mkate wa kila siku hakika amani ya bwana iwe nanyi.

Naaam twende kwenye lengo kuu lakuandika huu uzi maridhawa kabisa katika sekta yetu pendwa ya michezo hata huu mpira wa miguu unaojiongezea mashabiki nakukua kila baada ya muda.

Ndiyo, hapa Kati Kati kumetokea mgogoro baina ya yanga na mchezaji wao feisal salum abdallah "feitoto' Kama anavyotambulika katika tasnia hii ya mpira wetu wa miguu.

Kabla ya kuelekea kusikiliza kesi ya feisal pale ofisi za TFF, Mama mzazi wa feisal aliibuka nakuongea habari zisizo na mashiko yoyote akilalamika kuwa tff itende haki kwani mtoto wake kateseka sana yanga imefikia hatua ya kula ugali akilumagia na sukari.

Hicho kilichozungumzwa hapo na mama mzazi wa feisal hakika ni uongo asilimia mia kabisa hakuna kitu Kama hicho nakataa.

Kupitia watu wangu wakaribu Kabisa ndani ya yanga wanaoshinda na wachezaji ndani ya klabu, wamenithibitishia hakuna kitu Kama hicho Bali hizo ni propaganda tu zilizo tengenezwa kwa nia ovu kabisa kwa lengo la kuichafua yanga.

Mama feisal hakika umevunja uhusiano Kati ya timu na wewe na pia kwa mashabiki wote wa yanga na wampira kwa ujumla

Hivyo basi, yakupasa kutuomba radhi mashabiki na viongozi wote wa yanga hakika utasuuza nafsi inawezekana ulichozungumza ni propaganda zilizosukwa na watu chochezi kwa nia ovu kabisa ili kuihujumu yanga.

Ni matumaini Yangu watu wema waliokaribu na mama mzazi watamfikishia hizi habari ili achutame na kukiri alipokosea.
..usiongee maneno,thibitisha Kuwa mama ni mwongo na Kuwa Feisal haali huo ugali kwa sukari kama alivyonukuliwa mama.
 
hiyo millon 4 mnaijua mchanganuo wake ? pili maisha ya vibarua yana siri nyng , mm nakula abt 1.....ila kuna muda nakosa nauli napiga lege Makonde to Morocco , sishangai kbs
acha upimbi iyo milion 112 aliyowawekea Yanga ktk account alitoa wapi ?
 
..usiongee maneno,thibitisha Kuwa mama ni mwongo na Kuwa Feisal haali huo ugali kwa sukari kama alivyonukuliwa mama.
Mama feisal akija akithibitisha hadharani kuwa mwanae alikua anakula ugali kwa sukari basi na mimi nitathibitisha niliyoyaongea.[emoji41]
 
Back
Top Bottom