Mama hamtaki Mpenzi wangu

Ungekuwa ni dada yangu unaolewa na mtu mwenye sifa kama hizo hapo juu ningesikitika. Umetaja sifa za mtu ambaye huwa namkwepa kuwa rafiki yangu wa kutafuta mishe mtaani na jioni kila mmoja kwake, sasa wewe unaenda kumfanya mumeo wa kuishi nae nyumba moja.
 
Mkuu, tunaingia kwenye mahusiano na watu ambao ni sisi ndio tunawaelewa na kuwafahamu undani wao. Kisha ndio tunawashirikisha wengine, mfano wazazi na familia.

Wewe ndio unamfahamu huyo jamaa Kwa undani sana. Ni mlevi, mvuta bangi ila still umemkubali, may b kuna vitu ambavyo umeviona kwake.

Ni ngumu kuolewa nae kama mama yako hataki, lakini pia ni ngumu kuachana nae kama moyo wako ndio umemchagua.

Nakushauri usipingane na Mama yako, lakini pia usikubaliane nae. Kwasasa hairisha ilo zoezi la utambulisho au urasimishaji hayo mahusiano yenu. Endeleeni hata kwa Siri, huku ukitafuta namna nzuri ya kuweza kumuaminisha Mama yako kuhusu huyo jamaa. Lakini pia itakupa muda zaidi wa kuendelea kufahamiana nae, maana miezi mitatu uliyojuana nae ni michachr mno, na ni rahisi mtu kuigiza.

With time, mkiwa serious ni rahisi mama kuwaelewa
 
NIMESOMA COMMENT NYINGI ILA UKIONA HIYO MAMA YAKO ALISHALIWA NA HUYO JAMAA..NDO MAANA ANAWEKA VIPINGAMIZI VINGI SANA USIFANIKIWE.
 
Kwa hio hakuna mtu mwingine anaeweza kumshauri mama abadirishe maamuzi yake kwamba kijana yumempa muda wa kumuangalia tumemuona, mjomba (kaka wa mama) mmemshirikisha maana kuna tamaduni mjomba akisema NO ni big NO hata ufanye nini mjomba akikugomea ndio imetoka hio kaka wa mama yako amesemaje km Shangazi yako amesema ndio mjomba anasemaje ili aongee na dada yake hapo waweke Mambo sawa,
 
Dear we km na huyo shemela mnapendana na mmeweka malengo ya dhati juu ya maisha yenu kwa pamoja endelea kuwa nae, achana na mbambamba za mama, kikubwa wee ni mtu mzima na unajua nn unafanyaa.

Mama mpe heshima yake km mzazi, mambo yako binafsi uamuzi uko kwako na ni haki yakoo. Kumbuka kuwa huyo jamaa unampenda wee na sio yeye, na hata kuishi utaishi nae wee sio yeye, na hata ya ndani zaidi utayajua wee sio yeye.

Kuwa huru na moyo wako kufuata hitaji lako lilipo, usiishi kwa kutaka kumridhisha huyo mama yako utapata tabu sanaaa, mambo mengine usikubali yeye atie mkono wake atakuharibia mipango yako.

Pambania furaha yako wee mwenyewee, sio kupambania furahaa ya mama yako, hilo ni yake yeye.

Nakusisitiza, fuata moyo wako, maisha ni vile wee unaamua, maisha yako binafsi ni juu yako ni hakii yakoo, hupaswi kuingiliwa.
 
Sio rahisi kuongea kwa ukali na Bi Mkuwa au Mzee, unahitaji busara mno kuweza kuongea naye vitu ambavyo tayari wana majibu yao
 
Ndo nilitakaa niseme mie amuulize huyo mama ake, yeye kuwa na baba ake alichaguliwa au kwa ridhaa yake, wala hakuna heshima kuvunjwa anapaswa kumuuliza.
Nimemwambia huyu Muhanga kwamba inawezekana hata mama yake anavutiwa na huyo mpenzi wake lakini kama ni single parent family
 
Mama yako yuko sawa.

Yaonesha wewe ndo unalazimisha kuolewa

Maana kama umembadilisha na kumwambia ahame naye akahama, huyo jamaa hajitambui.


Kwanza inakuwaje mwanaume una miaka 38 na huna hata mtoto?
 
Na hivyo vitu sio kivile, pombe ameacha tangu nimwambie mi pia staki hivyo vitu akishindwa kuacha tutakua tu casual amenielewa anayafanyia kazi hayo

ukimuuliza anasema umemtukana
Unazugwa tu.
Ukiolewa tu anaanza

Tabia ni kama ngozi, huibadilishi kamwe
 
Usithubutu kumuamini. Watu wasanii kwenye kutaka kufanikisha mambo yao. Usimlie yamini mlevi anayesema anafanyia kazi ulevi wake kwa ajili yako.
Pombe, Bangi, Sigara haziachwi kwa kuambiwa.
Watu wana Kansa ila wanaendeleza kutumia tu.

Hapo anazugwa atamkumbuka Mama yake
 
Lazimisha uolewe mkuu. Mwanakulitaka mwana kulipata,mtoto akililia wembe mpe

Yaani umembadilisha mazingira na kila kitu inaonekana jamaa ni mario
 
Hapo bangi itoe sasa maana bangi kete 1 ni shilingi 300 unalewa tosha…Mtut atashindwa kuhudumia familia kisa kafirisiwa na miatatu?
 
Sio rahisi kuongea kwa ukali na Bi Mkuwa au Mzee, unahitaji busara mno kuweza kuongea naye vitu ambavyo tayari wana majibu yao
Yaan sio mie, bora nichukiwe ila kukubali unafiki hiyo hulka sina kwa kweli. Ukweli nitawaambia haijalishi watanionaje au watanifikiriaje sijali kikubwa mie unafiki nimeukataaa.

Tena kwa jambo langu binafsi ndo kabisaa nitawafurahishaa mbna. khaaaah
 
mwambie maisha yanataka "humble beginnings". Pengine atakuelewa
Yani ni mwamba miaka yote mama alikua anasema anatuweka kikao na mabinti wengine kuwa tunachagua sana mabwana, tunataka matajiri
tukipata wanaume wenye mapenzi ya kweli tuolewe haijalishi wana hali gani ila ukipata mwenye upendo unajenga maisha, nikamwambia nina mpenzi nmeanza nae kulala chini ila he took me for granted pia naogopaga kukuletea wakwe mana sina bahati sana na wanaume wazuri wazuri na hata mimi hawanivutiagi ila kwa historia yako unayosemaga unawapa kura za ndio vijana watanashati ila hawaoi tukawa tunaongeaga kawaida sometimes
sasa imetokea mtu aliokua anamsema ndio kanasa kwenye ndoano hamtaki kasahau yote
sasa
 
Mtumiaji wa pombe
Bangi
Sigara
Ugolo

Hawaachi kamwe
 
Mdogo wangu huyo Mama inawezekana ana mzimia mchumba wa mwanae. Hata kama ni mlevi au mvuta bangi sasa ndio mapenzi yamechukua nafasi awaache waendelee. Huyo Maza ni nongwa tu inamsumbua
 
Kama mama anataka mme msomi mwenye hela na hadhi angemwandaa alafu akuozeshe .miaka 28 unasubiki msomi na mwenye hale itafika hatua utasema yoyote ilimradi mradi awe anapumua
 
Mdogo wangu huyo Mama inawezekana ana mzimia mchumba wa mwanae. Hata kama ni mlevi au mvuta bangi sasa ndio mapenzi yamechukua nafasi awaache waendelee. Huyo Maza ni nongwa tu inamsumbua
hata kama.... najaribu kusema tu uraibu wa pombe na bangi sio kitu cha kufumbia macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…