Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Tatizo wazazi wa kibongo ni miungu watu na wanaamini wako sahihi kila jambo.

Miaka 28 ilibidi uwe unamwelekeza mwanao ona sasa ndo kwanza unapangiwa maisha.

Wewe olewa
Kuna watu huko juu wamesema wana haki ya kuwa miungu watu juu yetu...na mimi umri nilionao ni mtoto tena foolish age
wakati wao wazazi kwa umri wangu walikua washazaa mizao kadhaa.
ila sasa sisi bado tunapangiwa maisha wanavyotaka katika umri huu ilihali kama ni mengi nmeyaona japo hayafikii yake ila atleast hata aniskilize
 
Mazaako ana vituko asee[emoji16][emoji16][emoji16][emoji38][emoji38]
 
Pole sana Miss ushauri wangu Wewe simamia kile unachokiamini na hakuna kitu kinachodumu kama hakina changamoto. Hizo ni changamoto tu na hawa Mama zetu wa kiswahili wana shida sana. Yameshanikuta mengi sana na Mama mzazi tena ni magumu mno, nikaamua kukaa Kimya tu na kuendelea na mambo yangu. Mbona yeye mwenyewe alijigundua kanikosea sana na akaniomba sana msamaha. Na mimi huwa sihifadhi chuki moyoni maana chuki ni uchafu wa roho. Endelea na mshikaji wako kama kawaida na kama una nafasi kila Jumatatu na jumatano uwe inasikilizwa radio TBC taifa kuanzia saa 5 usiku utafaidika na mengi sana.
asante ngoja niweke alarm.
Ntajitahidi kuchanganua mema na mabaya ila najua kwenye maisha hakuna kitu permanent hata ikiwaje maachano yapo kikubwa ni kuachilia na kupunguza madhara ila popote yapo ni kuomba Mungu aepushe na abariki juhudi kumuachia yeye aamue yaliyofaa na yasiofaa
 
Mazaako ana vituko asee[emoji16][emoji16][emoji16][emoji38][emoji38]
wamesema nimsikilize mana ni mkubwa nisiolewe na mvuta bangi mana mpaka nachoka mimi
manake yangu mi naona yanaenda tu na amani ya moyo napata ila watu sasa [emoji119]
 
princess ariana Mimi naamini huyo mshikaji anakupenda kuliko wewe unavyompenda kwa sababu anakusikiliza na ameacha kutumia mambo yetu baada ya kumwambia. Na ulevi wa pombe au madawa ya kulevya wakati mwingine huwa yanatokana na upweke. Pendaneni bhana huyo Mother wako atakuja kuelewa tu. Upendo ndio kila kitu. Yeye anakulazimisha upate Bwana mwenye hela Yeye anadhani hela ndio chanzo cha furaha? 😂
 
tatizo mna complicate mambo wapi nmesema naolewa???
nani kakwambia nna nyege??
kwahiyo ushauri wako katika yote nilioongea umeona useme hivyo
Kuna wengine humu ni wapuuzi tu na huwa wanatumia uhuru wao wa kutoa maoni vibaya. Maisha ni yako na Nyege ni zako achana na watoto ambao bado wanakula chakula cha Wazazi wao
 
Wazazi wengi hasa wamama ndo zao hizo
Namshukuru Mungu mama angu alinishauri tu wangoni na wamakonde nisijaribu
Ila wengine hakaaa kikubwa tupendane hata kama ni muislamu wala nisiogope
 
Hilo limewai nitokeaa mam alisema Kam nitamuoa huyo mwanamke nitatute sehemu nikaishi na Kweli alikuwa sahih demu yule alikuwa viazi haswa
 
Punguza kumwambia kila kitu maza,, hapo kwenye hadhi anajiona kazaa beyonce sio[emoji23][emoji23]ila wazazi wengine wanazingua
Ukikutana na mazaangu sasa si ungechoka[emoji16][emoji16][emoji848]

Yaan nisingejipindua kukataa maushauri yake ningedoda[emoji38]

Kila mwanaume hamtaki sasa sijui alikuwa anamtaka Bill Gates [emoji848]
 
princess ariana Mimi naamini huyo mshikaji anakupenda kuliko wewe unavyompenda kwa sababu anakusikiliza na ameacha kutumia mambo yetu baada ya kumwambia. Na ulevi wa pombe au madawa ya kulevya wakati mwingine huwa yanatokana na upweke. Pendaneni bhana huyo Mother wako atakuja kuelewa tu. Upendo ndio kila kitu. Yeye anakulazimisha upate Bwana mwenye hela Yeye anadhani hela ndio chanzo cha furaha? [emoji23]
kwake yeye mwenye hela hata akinichoma na gunia mbili ni sawa, hata nikiwa sina amani mana ana hadhi na yeye ataonekana kuwa ana mkwe wa maana.
Ila mkaka wa watu kama kunipenda nanaipenda nagarama nmemtia mpaka namuonea huruma maana sio rahisi mwanaume apangue mipango yake asikilize yako, ilibidi akapaue nyumba yake ila ndo nikaingikia mfumo, na amehama mbali na biashara yake ili tu mama asinione nikimtembelea kanunua kila kitu kipya mana siunajua maisha ya pekeake baadhi ya vitu hakua navyo mambo ya masufuria na mwiko.. na kazi alikua anafanya 18 hours mana home anasema alikua hataki kurudi mapema anaona upweke, pombe kapumzika yani ananitahidi na upendo anao pia ila ndo hivyo hatakiwi anaambiwa anajitutumua anipate
 
Back
Top Bottom