Mama Janeth Magufuli nikikuangalia naona upendo, nikikusikiliza nasikia upendo; Mungu akubariki sana!

Mama Janeth Magufuli nikikuangalia naona upendo, nikikusikiliza nasikia upendo; Mungu akubariki sana!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Kupitia TBC jana, katika kipindi kinachozungumzia yaliyojiri wiki hiyo, nimekuona ukiwa katika ibada/misa ya kumuombea marehemu mume wako ambaye pia alikuwa raisi wa JMT. Ulipokaribishwa mbele kwa ajili ya kutoa neno, kinywa chako kilinena vema kabisa.

Katika mengi uliyoongea, kamwe hukusahau kutoa shukrani kwa Mh Raisi, mama Samia kwa kuwa pamoja nawe katika kipindi chote tangu alipofariki mumeo. Ukaweka wazi pia kuhusu uamuzi wa Raisi kumtuma binti yake kuungana na familia yako na ukamalizia kwa kuwaomba/kuwasihi kumuombea Mh Raisi ili aendelee vema katika kuisimamia na kuiendeleza kazi aliyoachiwa na marehemu mumeo ya kuihudumia Tanzania. Uungwana ulioje!

Uungwana ulioje, nilipatwa na furaha na matumaini sana:
1. Maneno yamejaa humu kuwa TBC na vyombo vingine havitaki kabisa kumzungumzia jpm, mi nimekuona kupitia TBC.
2. Threads zimejaa humu kuwa mama Samia amekupotezea wewe na familia yako, ushuhuda wako umewaumbua vibaya sana. Walivyo na roho ngumu wanaramani hata usingekaribishwa kule mbele kutoa neno.
3. Maneno yako ni ishara kuwa moyo wako umejaa imani, upendo na subra; kinyume kabisa mitazamo ya kishari ambayo maadui wa mama Samia wanataka kukuvesha.

Umewaumbua wanafiki,
Umewachinjilia mbali wafitini!

Ubarikiwe sana mama Janeth Magufuli, Ameen!
 
Yule Mjumbe Wa Halmashauri kuu Zenji Somebody .... Suluhu Hassan nilifikiri Huenda ni Mdogo wa Raisi aama Vinginevyo,Kumbe Mwanae, Naomba Kujuzwa Raisi anatumia Majina yake na wazazi wake ama Ya Mumewe??

Sipo Interested sana Na siasa kwahyo Sielewi.
Mi linapokuja suala la siasa ndo afadhali wewe upo mbali, unawajua hadi wajumbe? Tena wa zenji?!!!! Mi ndo hata kufahamu siwafahamu.

Labda kidogo, tuache kufadhaika na aibu tuliyoipata, turudi kwenye mada!
 
Huyu Mama aliteseka sana wakati Magufuli yuko hai, muache sasa afurahie maisha yake. Tabasamu na afya aliyo nayo inaonekana anaishi kwenye uhuru. Magufuli alitesa sana Watanzania including familia yake. Mungu aliamua, jina lake lihimidiwe
 
Huwo ndio Ukristo wa kweli. Wapo wanao muonea wivu wapo wanao tamana hata na yeye angeondoka. Ila Mungu anampenda umaarufu wa mume umeamia kwake.
 
Yule Mjumbe Wa Halmashauri kuu Zenji Somebody .... Suluhu Hassan nilifikiri Huenda ni Mdogo wa Raisi aama Vinginevyo,Kumbe Mwanae, Naomba Kujuzwa Raisi anatumia Majina yake na wazazi wake ama Ya Mumewe??

Sipo Interested sana Na siasa kwahyo Sielewi.
Waislamu kila mtu anatumia jina lake yaani hawatumii majina ya mume kama wakristo yaani ww jina lako litakuwa hivyo hvyo kama ulivyopewa na wazazi wako labda ki protocols kama sijui sheria zao ila kwenye uislam ni kawaida.
 
Kwa Mantiki Hiyo, yule ni mdogo wake na si mwanae kama Mjumbe mmoja alivyosema hapo juu.
 
Waislamu kila mtu anatumia jina lake yaani hawatumii majina ya mume kama wakristo yaani ww jina lako litakuwa hivyo hvyo kama ulivyopewa na wazazi wako labda ki protocols kama sijui sheria zao ila kwenye uislam ni kawaida.
Kwahiyo Binti kutumia jina la Babu yake atakuwa ni mtoto haramu sio?
 
Kwahiyo Binti kutumia jina la Babu yake atakuwa ni mtoto haramu sio?
Inawezekana ikawa ni mdogo wake japokuwa sijashuhudia tukio live ila kwa mantiki hyo atakuwa mdogo wake.
 
Back
Top Bottom