Mama kabandika picha sebuleni ambazo yumo ex, mke kazing'oa. Hapa kosa la nani?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
JE, HUU NI UUNGWANA?

Mama wa rafiki alikuja na picha ya frem ili aiweke sebuleni, kwenye picha yupo yeye, rafiki yake mwengine na ex wake.

mke wake alipofika nyumbani aliitoa hio picha, mama akaanza kulalamika kagharamika na kutumia muda mwingi kuchagua picha.

mama akaanza kumwambia kachagua picha pekee aliyoipenda ambayo mtoto wake yupo na rafiki yake aliemzoea tangu wakiwa wadogo, wife alipoanza kulalamika kuhusu huyo ex, mama akamwambia ex ni sehemu ya maisha yaliyopita ya mtoto wake na hawezi kuifuta historia ya mtu kwahio ampuuze huyo ex.

Binafsi nimempongeza mke wake kwa kuwa na akili maana njlitegemea nae ataweka picha ya ex wake.
 
Nyumba ya Nani? Ya Mama Mkwe? Au Mama Mkwe ndio kaenda Kwa Watoto wake huko ndio akabandika hizo picha kwenye nyumba ya mwanamke mwenzie (mkamwana)?
 
Acha umbea.

Hujaombwa ushauri. Kiherehere kimekusababisha uje uanzishe uzi kwa ajili ya maisha ya watu.
 
Kosa ni Kukosa Busara.....

(Kwa yoyote yule ambaye hajui feelings na tabia za Mwenzake) - Kabla haujafanya kitu una-weigh matokeo; Huo ndio Ukubwa...
 
He jamani mbona mkali hivyo?
Mkuu,

Mwanaume unapaswa kuwa na guts. Kasikia umbea, angebaki nao. Kuna sehemu popote kaombwa ushauri? Likamshinda na yeye kuamua kuja jukwaani kuomba ushauri?

Unajua nini? Pengine ile familia ikawa humu, comments za wanazengwe zinaweza kutibua na kulianzisha upya baada ya kuzipitia. Jambo ambalo huenda limeshamalizika.
 
Mi huwa nasema kila siku, wanaume wa siku hizi ni wambea sana,ndio maana zile shingo za zamani zina kinundu hazionekani kabisaaaa....yaani ukimpa mwanaume Siri amini usiamini umeimwaga
 
Mi huwa nasema kila siku, wanaume wa siku hizi ni wambea sana,ndio maana zile shingo za zamani zina kinundu hazionekani kabisaaaa....yaani ukimpa mwanaume Siri amini usiamini umeimwaga
Eti shingo za zamani zenye kinundu..... hahahaaa! ngoja nianze kuangalia wanaúme wenzangu,nione kama kweli HAWAPO.... daaah! JF ina mambo sana.
 
Hii inamhusu mwenyewe hapa kazunguka tu.
Jiongeze mkuu mbona ni code rahisi sana kuifungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…