Mama Kanumba: Lulu ameenda miaka 2 jela na atatoka, Kanumba hatarudi tena

Mama Kanumba: Lulu ameenda miaka 2 jela na atatoka, Kanumba hatarudi tena

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Siku moja baada ya Elizabeth Michael 'Lulu' kuhukumiwa kifungo cha kutumikia jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia, mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Frora Mutegoa amesema wanaombeza kwa kuishukuru mahakama wamuache kwa kuwa hakuna mwenye uchungu zaidi yake.

Jana baada ya Mahakama Kuu kumtia hatiani mwigizaji huyo na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, Mama Kanumba aliishukuru mahakama akisema imetenda haki jambo ambalo lilizusha gumzo wengi wakisema hakupaswa kufurahia adhabu hiyo.

Akihojiwa na waandishi wa habari nje ya mahakama kuu jijini Dar es salaam jana Jumatatu baada ya hukumu kutolewa alisema anashukuru kwa kuwa haki imetendeka na kwamba atakwenda kumzika rasmi mtoto wake.

Hata hivyo, Mwananchi leo Jumanne amenukuliwa akisema asibezwe kwa kauli hiyo kuwa hakuna anayejua uchungu anaoupata kila siku.

"Mimi sijui kama ninafurahia kama wanavyodai, waulize kwamba, yeye Lulu alipokufa mwanangu Kanumba alifurahia? Mimi ni mkristo, sipendi kuona baya likimfika binadamu mwenzangu, lakini Lulu ameenda miaka miwili jela na atarudi, je mwanangu atarudi lini? nitamwona wapi tena"? Amehoji.
 
Huyu mama amuache kama alivyodai mwenyewe. Jaji amemaliza atumikie 2 tusonge mbele. Na jamii kuna jambo la kujifunza kwa mikasa kama hii.
Lakini Kanumba naye hakuwa na kosa? Maana kifo kila mtu atakufa. Ila kilichosababisha kifo ndio hatutaki kukieleza. Ukristo unatuasa tusamehe maana hatutasamehewa kama hatufanyi hivyo.
 
Chini ya miaka 18 lakini akili na mambo yake ni kama ana zaidi ya miaka 25 hapo inakuwaje?
Sheria inasemaje kuhusu kutembea na msichana wa umri mdogo? Ni jela tu tena alikuwa mwanafunzi jelaaaaaaaa
 
Chini ya miaka 18 lakini akili na mambo yake ni kama ana zaidi ya miaka 25 hapo inakuwaje?

Yani ukitembea na mtoto chini ya miaka kumi nane awe amekubari, awe hakuwa bikra, awe ana msululu wa mabwana amewahi kutoa mimba ukikamatwa wewe huwezi jitetea ni kwamba umembaka.

Kisheria mtoto chini ya miaka 18, hana maamuzi binafsi ni rahisi danganywa na shawishiwa.

Lengo si kumsema marehemu ila ni kukuhabarisha wewe ili usije fanya kosa hilo ukiwa wajipa moyo kwani huyu binti mimi wa kwanza mbona na flani kapita...
 
Kama kanumba asingekufa angefungwa jela miaka 30 au zaidi kwa kutembea na binti wa Chini ya miaka 18
Huyo alishatimiza miaka 18 mwaka mmoja nyuma kabla ya kifo cha marehemu na birthday party alifanya huo udogo cjui unatokea wap
 
Huyo alishatimiza miaka 18 mwaka mmoja nyuma kabla ya kifo cha marehemu na birthday party alifanya huo udogo cjui unatokea wap
Hivi we ni kee dia ee
Ok tuje kwenye mada huyu binti hakuanza naye pale walituhadaa tangu akiwa na miaka 15 hao
ac43586d5d532ab56e46685ae2524c34.jpg

Sasa dia ukisema embe bado changa wenzio wanalila na chumvi
Huyu lazima angeenda jela
 
Huyo alishatimiza miaka 18 mwaka mmoja nyuma kabla ya kifo cha marehemu na birthday party alifanya huo udogo cjui unatokea wap
Bwihi bwihi [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] Eti mtoto anaendesha gari anaenda klabu za usiku.. Ok tuache kama ilivyo
 
Bwihi bwihi [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] Eti mtoto anaendesha gari anaenda klabu za usiku.. Ok tuache kama ilivyo
Hilo halifuti utoto, ukianza fuatilia ni watoto wangapi wanaendesha magari na kwenda club mbona wengi tu...
 
Back
Top Bottom