Mama Lulu atamani mwanaye afe tu

Mama Lulu atamani mwanaye afe tu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Kufuatia kuandamwa na skendo za wanaume na kuchafuliwa kila siku, mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu', Lucresia Karugila ‘Mama Lulu' ametoa kauli nzito yenye kushtua kwamba anatamani mwanaye huyo afe tu ili watu wanyamaze kumsemasema. Imemuuma sana!

Lulu.jpg

Lulu akiwa hoi nyumbani.

YOTE HAYA KISA MITANDAO
Mama Lulu amefunguka hayo siku kadhaa baada ya mitandao ya kijamii kuchafuka kwa habari za binti yake na wanaume hasa wa watu huku mwenyewe (Lulu) akiwa nyumbani kwake Mbezi-Beach jijini Dar akiwa hana hili wala lile.



TUJIUNGE NA MAMA LULU
Akizungumza na gazeti hili, mama Lulu alisema mambo mazito kuwa, hakuna mzazi ambaye hata siku moja anaweza kuvumilia kuona mtoto wake akiandamwa na kashfa ambazo si za kweli.

MANENO KUNTU
"Mimi ndiye nimemzaa Lulu, najua uchungu wa mtoto kama mzazi. "Wanaomsema Lulu vibaya wakumbuke hata mimi nina moyo kama wao, si chuma hivyo hata mimi naumia kama ambavyo mwanamke yeyote mwenye kujua uchungu wa mwana ni nini anaweza kuumia."Ni mzazi gani mwenye moyo wa chuma wa kuona mwanaye anabebeshwa shutuma nzito kama hizo kila kukicha halafu akanyamaza au kufurahia?

"Watu wanamfuatilia na kumsakama sana mwanangu. Hawamwachi apumue," alisema mama Lulu kwa uchungu huku machozi yakimtoka.


ElizabethMichaellulu.jpg
Staa wa sinema za Kibongo,
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu'.


Mzazi huyo aliendelea kusema kuwa, anaamini kwamba mambo mengine yanayotokea katika maisha ya mwanaye ni mipango ya Mwenyezi Mungu hivyo haoni sababu ya Lulu kubebeshwa lawama za ajabu.

Mama huyo alisema kuwa watu hao wanataka mwanaye afe kwa sababu kuna wakati anakosa raha ya dunia hivyo naye anatamani afe tu ili watu wamwache apumzike.


KIPINDI KIGUMU CHA MITIHANI
Mama Lulu aliendelea kueleza kuwa, Lulu kwa sasa yupo kwenye kipindi kigumu cha mitihani (anasoma Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Magogoni-Posta jijini Dar) lakini anawezaje kufanya vizuri huku kuna baadhi ya watu wakimsemea maneno yasiyofaa?!

"Atawezaje kufanya vizuri wakati watu wanamwandama kila kukicha? Huko kote ni kumkatisha tamaa hivyo nimemwambia mwanangu amwachie Mungu na kusali sana," alimalizia mama Lulu.


MamaLulu.jpg
Lucresia Karugila ‘Mama Lulu'.

HUYU HAPA LULU
Baada ya kuzungumza na mama huyo, mwandishi wetu alimtafuta Lulu ili kumsikia na yeye ana mtazamo gani kuhusu shutuma hizo ambapo alisema kila kitu anamuachia Mungu pekee na si mwingine hivyo kwa sasa aachwe asome."Kila kitu changu nimemuachia Mungu maana hakuna mtetezi wangu zaidi yake, ndiyo maana ninasali sana ili Mungu anisaidie," alisema Lulu.

Chanzo: GPL
 

Attachments

  • lulu.png
    lulu.png
    154.1 KB · Views: 4,615
hivi mama lulu anajua kuwa lulu ndio anamuumiza na matendo yake?
 
Katapata buz tena aka? kifo si mchezo
 
Jamani warumi I miss you!Huu umbea nitakuja kuupiga baadae nimefurahi tu kukuona tena.

Karibu dada ake, aya nakusubir tuje kupiga umbea wa haja maana ni shidaa
 
Last edited by a moderator:
Maneno uumba Lulu muda si mrefu atawafata aliowatanguliza.

Anajiropokesha tu, lulu akifa nani atamuweka mjini? Vitumbua vyenyewe kaacha kuuza kwa ajili ya lulu
 
Huyo mama ana frustrations? Huwezi mwombea mwanao kifo au anataka rambirambi apige
 
Lulu nenda/rudi msalabani upate amani ya kweli, dunia imejaa taabu lakini kwa Bwana tunafarijika na kupata amani ya moyo!

watu wanadhani wanaweza kupata amani ya moyo kwa kutumia pesa, mali walizonazo etc.....faraja ya kweli inatoka kwa Mungu inatoka kwa Yesu....alituahidi pale msalabani kwa kupigwa kwake sisi tumepona.....amtumainie Bwana ni kama mlima sayuni atatikisika milele......
 
Huyo mama ana frustrations? Huwezi mwombea mwanao kifo au anataka rambirambi apige

kuna Mtakatifu mmoja anaitwa Mtakatifu Ritha ....kwenye historia yake alishawahi kuomba watoto wake wafe ili wasitende ubaya duniani......
 
watu wanadhani wanaweza kupata amani ya moyo kwa kutumia pesa, mali walizonazo etc.....faraja ya kweli inatoka kwa Mungu inatoka kwa Yesu....alituahidi pale msalabani kwa kupigwa kwake sisi tumepona.....amtumainie Bwana ni kama mlima sayuni atatikisika milele......

Amen.. Tujifunze zaidi kumtafuta Mungu kuliko shetani, lulu uko ulipo usijali tupo pamoja tunakuombea
 
Back
Top Bottom