Mama Mabula kaa chonjo hapo Ardhi, kuna genge la wafanyakazi wezi na waporaji viwanja!

Mama Mabula kaa chonjo hapo Ardhi, kuna genge la wafanyakazi wezi na waporaji viwanja!

Nafikiri hii wizara, ina ka laana flani hivi.
Ina tia kichefu chefu sana.Mama aikalie kooni haswa.
Ni zaidi ya laana
Miaka ya Mzee Mwinyi nasikia washamtapeli kiwanja chake wakijua kabisa ni cha Mh.Rais
Alifukuza hadi Waziri wa Ardhi

Sijui wanajikuta akina nani
Tumuogope Mungu jmn
 
Nataka kumtahadharisha mama yangu Mpendwa Mama Dk Angelina Mabula.
Amekaa hapo Wizara ya Ardhi kwa muda mrefu sasa lakini hajui kuwa kuna kakundi au genge la wezi na waporaji wa viwanja.

Suala linaanzia hapo kwa Msajili wa Hati.
Mafaili ya viwanja yanapotezwa na kuna nyakati mafaili yanakuwa hayana nyaraka kabisa zilizotayarishwa ili kupatiwa Hati.
Wahusika wanajulikana lakini inaelekea kuna kamtandao ambako kameshindikana kuvunjwa maana kuna wakubwa wanfaidika.

Mchezo umehamia kwa sasa sehemu ambazo demand ya viwanja imekuwa kubwa, yaani Tegeta, Bagamoyo, Kibaha.
Mchezo unakuwa hivi;
-Faili hupotezwa
-hata likipatikana linakuwa halina nyaraka zozote ndani yake
-anapatikana mteja anauziwa haraka haraka kwa pesa ya juu sana na anapatiwa Hati fasta fasta
-mmiliki wa awali akiendelea kulalamika , anaambiwa asiwe na wasiwasi atapatiwa kiwanja kingine

Mchezo huu unafanyika bila haya wala soni, na bado mawaziri wetu wapo.

Hapo kwa Msajili wa Hati kuna matatizo makubwa sna.
Mlipofurahia Lukuvi kuondolewa eti kisa tu ni Pro-Magufuli,na akapelekwa Riziwani Kikwete,akaanza na Nyumba ya Nakonda Oysterbay!

Sasa hiyo wizara imo mikononi mwa GSM....

Mama anaupiga Mwingi kazi iemdelee!
 
Back
Top Bottom