Uchaguzi 2020 Mama Maria Nyerere: Nimelazimishwa kuja kuongea, niliwaambia nimekuja kuongeza wingi wa watu, Mkutano wa CCM Musoma

Uchaguzi 2020 Mama Maria Nyerere: Nimelazimishwa kuja kuongea, niliwaambia nimekuja kuongeza wingi wa watu, Mkutano wa CCM Musoma

"Mimi kwa bahati nzuri pamoja na Wanamara wenzangu sisi ni kundi lile tulilokuja tuongeze idadi ya watu, vichwa viongozeke kwahiyo sikuja kuzungumza chochote wao walinilazimisha kwamba nizungumze nikasema sina lakuzungumza"- Mama Maria Nyerere

Baada ya ujumbe huu mgumu unaonyesha namna watu wanavyolazimishwa kufanya wasichopenda kufanya, naamini viongozi wamekereka kwa sababu polepole katamka maneno haya:

Mama tunajua una majukumu mengi, endapo ukijisikia kuondoka ondoka upo huru Mwenyekiti amekupa baraka zote.

Huyu mama nadhani ni mara ya kwanza anasimamishwa Kwenye jukwaa la kampeni. Tusiwafanyie hivi watu Hawa waliotumika kwa heshima, waacheni wabaki na heshima yao.
Mama anajua maendeleo ya vitu yaliyopo kule Chato kwa Mheshimiwa na kulinganisha na yale ya pale kwao Butiama kwa Muasisi wa Taifa hili. Pengine litazinduliwa eneo jipya la hifadhi ili wale tausi wapate kuwekwa kama kivutio kipya cha utalii kule Butiama mfano wa Burigi.
 
Mbona makongoro kawachana sana chadema. Au amjamsikia? Na mama akasema yeye ana mengi makongoro amemaliza kila kitu. CHADEMA acheni Kumchonganisha mama wa watu na serikali. Pambaneni na hali zenu maana mna hali mbaya sana. Sema yule makongoro itakua anatumia kijiti.
 
Mbona makongoro kawachana sana chadema. Au amjamsikia? Na mama akasema yeye ana mengi makongoro amemaliza kila kitu. CHADEMA acheni kumchanganisha mama wa watu na serikali. Pambaneni na hali zenu maana mna hali mbaya sana. Sema yule makongoro itakua anatumia kijiti.
Sawa..... Lkn si ameshaongeza idadi km mlivotaka ww kinachokuuma nini sasa.....
 
Amesema amekuja kuongeza vichwa, maaanake kumbe wanaccm wanalazimishwa kwenda kuongeza vichwa.
kama hivi
IMG-20200905-WA0008.jpg
 
kawachoka kumtumia huku watoto ,wajukuu wake wakiishia kuwa walevi kwa sababu ya stress za kutengwa na serikali ya ccm

Mama kiwanja chake kule Rungwe Mbezi beach "A" kimegeuzwa kuwa uwanja wa fisi; wadangaji na majambazi wanapangishwa vibanda vya mabati!! Aibu sana kwa familia ya Mwalimu!!
 
Sawa..... Lkn si ameshaongeza idadi km mlivotaka ww kinachokuuma nini sasa.....
kinachoniuma ni CHADEMA kukosa mbunge hata mmoja bungeni awamu hii .. Sijui wabunge wa CCM watamzomea nani. Inauma sana.
 
Mama wa watu atakuwa ameambiwa kuwa Kigogo 2014 anamfumua vibaya Mama Samia huko Twitter ivyo akaona asiongee maneno mengi asije kuharibu [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah jananiiih JF idumu milele lol.
 
kinachoniuma ni CHADEMA kukosa mbunge hata mmoja bungeni awamu hii .. Sijui wabunge wa CCM watamzomea nani. Inauma sana.
Ccm ni chama cha kishetani.... Hakuna mtz atakipigia kura safari hiii....
Ndio maana mwenyekiti wako anaweweseka tu
 
CCM pumzi hamna... Huko Musoma leo ,maBus ya Zakaria, malori kibao kuanzia saa 10 za alfajir yalikua nakazi ya kusomba watu kuja kuongeza idadi na vichwa kama alivosema mama Maria.

Kwa ufupi..Mama maria hajapendezwa kuona Mwinyi na watoto wake wakiendelea kula bata... Alafu yeye na wanawe wakiendelea kusomeshwa namba.

Kama kuna familia ilotakiwa kutizamwa kwa jicho kubwa ni ya Familia ya Nyerere.
Yaaan huwa naumia mnooh, kweli watoto wa baba wa taifa wanakuwa hoe hae, huku wengine wakila cake za nchi. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
View attachment 1559508

"Mimi kwa bahati nzuri pamoja na Wanamara wenzangu sisi ni kundi lile tulilokuja tuongeze idadi ya watu, vichwa viongozeke kwahiyo sikuja kuzungumza chochote wao walinilazimisha kwamba nizungumze nikasema sina lakuzungumza"- Mama Maria Nyerere

Baada ya ujumbe huu mgumu unaonyesha namna watu wanavyolazimishwa kufanya wasichopenda kufanya, naamini viongozi wamekereka kwa sababu polepole katamka maneno haya:

Mama tunajua una majukumu mengi, endapo ukijisikia kuondoka ondoka upo huru Mwenyekiti amekupa baraka zote.

Huyu mama nadhani ni mara ya kwanza anasimamishwa Kwenye jukwaa la kampeni. Tusiwafanyie hivi watu Hawa waliotumika kwa heshima, waacheni wabaki na heshima yao.
View attachment 1559499View attachment 1559500View attachment 1559501View attachment 1559502
Utu uzima Dawa
 
Back
Top Bottom