Mama mkanye mwanao, hakuna cha bure mafanikio hayaji kama mvua

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuna kipindi nilikwenda nje ya Afrika na kuishi huko kama miaka 4 hivi na kidogo. Mwnyeji wetu alichukua muda wake kutueleza mambo ya msingi sana ya kuzingatia katika taasisi ile, mji ule na nchi ile na kukutembeza kwenye maeneo machache sana Muhimu ambayo tunaweza kujipatia mahitaji na huduma muhimu. Kuna mitaa mingine alituasa tusiende kabisa na kama ikibidi kwenda huko basi muwe zaidi ya mmoja na mrudi mapema.

Kati ya maneno muhimu ambayo nilibaki nayo kichwani hadi leo ni haya hapa:

1. Huku kwetu sio lazima wala sheria, lakini kutoa tip (asante ya malipo) kwa mhudumu aliyekuhudumia au taxi driver aliyekuhudumia ni jambo lisilokwepeka kama unataka kueleweka vizuri siku nyingine kama utarudi kupata huduma mahali pale tena. Akatuambia kiwango cha chini (minimum) cha kutoa asante (tip) kwa mhudumu aliyekuhudumia vinywaji, chakula au teksi.

2. Ni mtego huo: Huku kwetu sisi hakuna kitu cha bure; na hakuna urahisi wowote wa kupewa na kupata chochote iwe muda, huduma, vitu wala fedha. Hivyo basi, kama utakutana na kitu cha bure, huduma ya bure, fedha za bure au dili zuri (tamu) sana kwako kirahisi shituka hapohapo bila kusita na ufikirie mara mbilimbili kuhusu hilo dili, madhumuni ya kupewa wewe hilo dili (huduma, wema, fedha, muda, vitu) na sio mtu mwingine. Jiulize anataka nini kwako, anataka umfanyie nini, na nini itakuwa hatima yako, familia na taifa lako kama utakubali hilo dili.

Mzazi mkanye mwanao kuhusu madili yanayofanana na fursa kumbe sio fursa bali mtego wa kumwangamiza yeye mwenyewe, familia au jamii nzima. Ukiona mwanao amepata mafanikio makubwa ghafla kuliko kitu anachokifanya shituka haraka sana, mara nyingi ni mtego huo. Haiwekani mwanao anauza karanga kama wengine lakini akaja na Prado; shituka. Shituka kama mzazi, kama familia, kama jamii na kama taifa lazima kuna kitu hakiko sawa kwa kijana wenu.

Mfano, inafahamika kuwa mtoto wako ni mwandishi wa kawaida, au msanii au mwanamichezo au mfanyabiashara wa viatu vya mitumba wa kawaida tu, lakini kila mara amesafiri kwenda Marekani, Ulaya, Asia na kwingineko na kurudi na mafedha kedekede kutoka huko, ni mtego huo, maana kule hakuna cha bure walisema wenyewe kwa kinywa chao, yeye kapata wapi kwa sababu zipi?

Mzazi kuwa macho na mwanao.
 
Huwezi kuzuia watu na maisha yao mambo ya ovyo yapo tu duniaji toka enzi na enzi na tutayaacha na wengine wataokuja hivyohivyo.
Wewe ishi vizuri inatosha.
 
Sawa, lakini usishangae kusikia mwanao katekwa, kauawa, kalawitiwa, kapigwa au kachomewa nyumba. Lazima mzaji na jamii mjiulize kafanya nini hadi atendewe hivi.

Kama hukushangaa mwanao kuwa na fedha nyingi bila maelezo usishangae pia kama yakimkuta
 
Back
Top Bottom