Wana sisi wazima huku najua hakuna fujo sana, na kuna watu makini wa kunisaidia.
Wapenzi,
Nina mdogo wangu ana kama miaka 26, kaolewa na mtu wa Dodoma. Naishi nae karibu kama nyumba 5 kutoka kwangu amepanga chumba kimoja self container.
Sasa kama mwezi mkwewe alikuja kumsalimu.
Na alisema anakaa siku 3. Jamani, hadi leo mume wake analala kwa marafiki zake. Juzi nasikia anaongea na ndugu zake kuwa atarudi hadi pasaka iishe jamani mwezi na siku kadhaa na analala kitandani bila aibu.
Anaogopa kumwambia mumewe atahisi anamchukia mama yake na hivyo anataka jumamosi kuondoka kwenda kwao Morogoro ila mkwe haoneshi hata dalili ya kuondoka; kasema kama haukai sana utanikuta.
Hebu mshaurini mdogo wangu jamani.