Mama mkwe ana mwezi hana dalili ya kuondoka, chumba kimoja, nimemmisi mume wangu

Mama mkwe ana mwezi hana dalili ya kuondoka, chumba kimoja, nimemmisi mume wangu

Kweli makabila tunatofautiana mila
Kwetu mzazi wako hathubutu kulalia kitanda ambacho mwanae analala na mumewe au mkewe

Mama mkwe kakosa ustaarabu
Mume nae hajitambui

Ila kwa vile huuo ni mzazi wavumilie tu

Mpaka siku hamu zitakapowakaba wakatafuta pa kupunguza fasta fasta

Kama wana ndugu wengine mjini basi wamwambie azungukie wengine kuwasalimia abgalau watapata wasaa wa faragha
 
Duh! huyo mama nahisi amekuja na mkakati wa kuvunja ndoa ya mwanae..........

hebu chunguzeni kwa makini mpate ajenda nyingine iliyomleta town.
 
Unafikiri kila mtu ana ufahamu na utashi wa kusoma mazingira?
a.rahabu Kuanzia huyo mwanaume na mama yake wamekosa huo utashi. Mwanaume ndio alipaswa kuliona hilo mapema hata kabla hajaja na awe amepanga ramani nzima.

We unafikiri na huyo Mume huko aliko hawajamchoka? Ukweli nae wamemchoka. Mume anapaswa atumie hekima kidogo tu. Aende akanunue vizawadi vya pasaka haswa vyakula (Mafuta, mchele etc) na hela kidogo ampelekee mama yake amwambie akale na familia kusheherekea pasaka nyumbani. mchezo umeisha. Ila kwa wabongo tulivyowanafiki, mdada akijidai kwenda kumwambia Mumewe ajue imekula kwake maana inaonekana na mumewe hajitambui vizuri kupembua mchele na mpunga.

Kwa tamaduni za kikwetu nyumbani Mkwe au hata mama ajue una kachumba kamoja, Hata Umhonge na hela Juu hatakaa afikie kwako kamwe.

umenena mkuu
tatizo ni hawa kina mama wa kidigitali hawawazi mbali
 
Last edited by a moderator:
Yani kwa kweli umaskin nao ni kikwazo cha kua na maisha kama hayo!sidhan kama mama mkwe angekua anajiweza angefanya hzo mambo!
 
Karibu Chem.

Unadhani kama mama amekuwa wa kidigitali... huyo mume ndo tusemeje sasa? he is really something dude!!!

Hahahaaa!! Si muda mrefu tutaona post hapa waliomuhifadhi huyo mume wakilalamika. heading huenda ikawa
''Wana MMU, Hivi mtu akiomba usingizi kwa siku tatu akakaa zaidi ya mwezi na hana dalili za kuondoka unafanyaje? Naomba mawazo wadau''
umenena mkuu
tatizo ni hawa kina mama wa kidigitali hawawazi mbali
 
Karibu Chem.

Unadhani kama mama amekuwa wa kidigitali... huyo mume ndo tusemeje sasa? he is really something dude!!!

Hahahaaa!! Si muda mrefu tutaona post hapa waliomuhifadhi huyo mume wakilalamika. heading huenda ikawa
''Wana MMU, Hivi mtu akiomba usingizi kwa siku tatu akakaa zaidi ya mwezi na hana dalili za kuondoka unafanyaje? Naomba mawazo wadau''

hahahahaha umeona eeeeh sana atawakaribishia michepuko na hali ya hewa hii mmhhhh
 
Hahahaaaa. yaani hali ya hewa we acha tu. Inanitamanisha sana nikaoteshe matikiti/mihogo mahali.
hahahahaha umeona eeeeh sana atawakaribishia michepuko na hali ya hewa hii mmhhhh
 
Yaani mama analala kwenye kitanda chá mtoto wake wa kiume na mkamwana wake?
Hii kali Aisee
 
Duh hizo ndo changamoto za ndoa..avumilie tu kaja kwa mwanae kula bata loh si mnajua wamama wakwe wengine?! ! Lakinii......inamana huyo mdogo wako na mumewe hawawezi kutoka hata siku moja kwenda mahali pa faragha wakamalize shida zao huko then wakarudi maisha yakaendelea?? Aaah jamani mbona simple hivyo embu mwambie afanye hivyo kwanza ....
Dah munkari ukisikia mtumwa ktk nchi yako ndo ivi.Asa watapeleka mechi ugenini adi lini kwa vile tumeshavaa Uafrika inamlazimu jamaa atafute tunyumba twenye angalau tuvyumba tuwili.Ila jamani inaumaje unanyang`anywa uhuru bila chuki.akh karibu nisaau Munkari vp kwako ipo chansi waje wapige cha voda fasta?
 
Vumilia tu, walishasema kwenye ndoa kuna kupanda milima na kushuka, hiyo ndo milima yenyewe sio kila siku unashuka tu, as long as mmeo nae hajiongezi.
 
Kitu cha self containal!! Mjini pazuri bwana asikwambie "ntu"
 
kuwa mpolee. ameshafanya kosa lakulala kwenye kitanda cha mwnae anapo fanyia tendo la ndoa. akae tu mpaka iyoo pasaka iishe. mtapata baraka.
 
Back
Top Bottom