Mama mkwe anamhimiza mke wangu anichune; naomba ushauri

Ntakupigia video call nkuone.....
Piga ile no yangu inaishia na 78 ndio ipo hewani nipo hapa najifunza kuendesha gari namba E kabisa
1726229112033.jpg
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Ksms hukuchunwa wewe wapo watakaochunwa.

Uamuzi ni wako, uchunwe wewe au wengine.
 
Ni kweli lakini sio kwa direction hizo za Mama mkwe. Mtu hata hajazaa jamaa kawarekebishia mazingira, mke kamfungulia biashara.
Na anaendelea kutoa ushirikiano bado anasisitizwa amchune....labda kama sijaelewa kilichoandikwa.

Jamaa kama ni mimi, wala simwambii kuhusu hizo texts. Ila nitapunguza kumshirikisha katika miradi na issue za fedha.

Nitaweka budget aifate, na pesa nyingine itoke katika biashara niliyompakusaidia kwao, labda kuwe na jambo la msingi sana au dharura.

Sitaenda tena kusalimia ukweni kwa miaka 10 hadi 15, akifa sijui nani nani wa karibu ataenda mwenyewe. Nitaenda akifa baba mkwe au mama mkwe.
Nitaimarisha peripherals zangu za imani na ulinzi ikiwa ni pamoja na kuweka kamera maeneo maalumu. NA HII NI KWA SABABU YA HISIA ZA UPENDO NA USTAARABU.

Vinginevyo kwa mudi ya siku husika, ningeenda hard on them direct.... namchana mke wangu hapo hapo live, nampigia mama yake namweleza kuwa hajengi anataka kubomoa, akijibu pumba kesho tu mchakato wa talaka unaanza na nnakuja na demu la kununua lina makalio makubwa nalala nalo ndani na mwanae yupo GODDAMIT 😆
Wanaume sio wa kuwaamini aisee, pongezi kwa huyo mwanamke amefanya kazi nzuri 👏 👏
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Hawana akili na adabu
 
Back
Top Bottom