"Life starts at 40"
Kila nafsi ina namna inavyoingia kwenye mwili ili maisha yaanze na hapo ndipo huwa mtu kamili.
Binadamu wote hapa ulimwenguni wamegawiwa vipawa na karama mbali mbali.
Hii inakuwa rahisi kutokana na mfumo na kanuni za uumbaji zilizopo ambazo kila mtu anatakiwa azijue ili achague uwanja utakaomfiti yeye.
Mfano kuna mtu yeye ili awe na mafanikio mazuri na maisha yasiyokuwa na misukosuko ni anaanzisha ufugaji wa wanyama na wale wanyama wanamuinua kiuchumi na anakuwa na passion na hiyo mifugo kiasi cha kufika hata kugombana na mkewe.
Wewe utaona mafanikio kupitia yeye lakini ukijaribu kufanya wewe unakuta hufikii mafanikio kama ya yule.
Sasa wewe unajikuta ni konda Daslam kumbe kipawa chako ni Mkulima wa mpunga hivyo ulitakiwa uwe pale Kyela.
Life starts at 40..
Siku ya 40 baada ya mimba kutungwa ndio Nafsi hutoka kwenye sayari nyingine kutokana na tarehe na mwezi husika.
Nafsi ile huingia moja kwa moja kwenye tumbo la mama mjaa mzito na kujikita ndani ya mwili wa mtoto ndio maana wanawake hawezi kubeba mimba leo kisha kesho au baada ya siku mbili mtoto akacheza tumboni,, never
So nafsi ile ikiingia ndiyo hufuata masuala nyeti ambayo wanajimu huyaita nyota
Hii ndio huamua uwe na nani maishani mwako kama rafiki, msaidizi kazini kwako ama mke wako.
Hujawahi kukutana na mtu halafu mkabond katika mazingira ya ajabu ajabu tu?
Au ukakutana na mwanamke kisha usitumie nguvu kubwa katika kumtongoza na ukijiangalia wewe sio kwamba ni una mvuto kihivyo wala kipato kwamba labda umejibrand sana.
Unakuta anakuambia tu kuwa alivyosikia sauti yako au kukuona amesisimka sana.
Haya yote ni masuala yatokanayo na chanzo cha "Life starts at 40". Hii pia inaunganisha ile hali ya usiku ambayo wengi tunaita ndoto lakini si kweli kuwa ni ndoto..
Isiwe ndefu sana ikakera maana
Atoto wangu hapendi ndefu sana ananiambiaga inamkera hasikii utamu wake.