yah uko sawa, ivi nikuulize kitu, MUNGU huwa hawai wala hachelewi, vipi akiamua kuniletea baada ya miaka 20, hapa kati kati naishije, kitu kingne MUNGU akiamua kukupa labd binti aliyekuwaga malaya , ila yeye akisema huyo anakufaa na atamdadilisha yeye mwenyewe, hii kitu inakaaje?, mana kuna sehem moja katika bible kun mtu alipew mke ,ila yule mke mazingira aliyokuwapo ni kma danguro ivi,
MKUU HAPO INAKUAJE?.
Mkuu kwanza niseme kitu Hapa B'se tunaweza kua tunawalaumu Sana awa viumbe kumbe na sisi waoaji tunamatatizo au ndo chanzo cha matatizo yote, MWANAUME ndie muoaji Kwaiyo akioa
MWANAMKE mpumbavu tatizo ni yeye na Sio MWANAMKE kwasababu MWANAUME ndie aliemfuata kwa Roho na mwili wake na kwa Akili zake akaona huyu Mwanamke ni SAHIHI kua MKE na mama wa watoto Wangu
"UKWELI NI KWAMBA KUMPA MWANAMKE SAHIHI (MKE) KUNAANZIA NA WEWE KUA SAHIHI"
Kuna msemo mmoja wa waswahili husema ndege wafananao Ndio huruka pamoja, UKWELI Huwezi kupata MWANAMKE SAHIHI (MKE) kama wewe MWANAUME sio MTU SAHIHI (MME), Ebu anza kua MME before hujaingia katika NDOA nakuhakikishia utapa MKE 😁
Mithali 19:14
"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana"
"mtu hupewa na Bwana" 👉 hapa sio kwamba utashushiwa kimiujiza Hapana ila MUNGU atakutumia wewe mwenyewe kukupa MKE mwenye busara
Sasa tujiulize swali👇
utamjuaje MWANAMKE mwenye busara kama wewe mwenyewe huna busara?
ndipo tunaludi kwenye point yetu ya kwanza kupata MTU SAHIHI kunaanza na wewe kua SAHIHI (i.e utapewa wa kufanana na wewe kama ni mpumbavu utapewa mpumbavu mwenzako
mkashindane na kuhangaika na kuvumiliana katika NDOA, kama ni mwelevu utapewa mwelevu mwenzio
mkaishi katika NDOA hakuna miujiza Wala shotcut katika hili wakuu na kuna watu wanasema NDOA za sikuizi ni kama betting Sio Kweli ila uhalisia ni Kwamba TUNAPEWA WANAWAKE TUNAOFANANA NAO TABIA)
Wisdom is the accumulation of knowledge/enlightenment while wise is the application of wisdom Kwaiyo kamwe huwezi kua na BUSARA kama huna HEKIMA Kwasababu BUSARA ni matokeo ya Hekima
Kwa lugha NYEPESI BUSARA ni kutenda kwa HEKIMA kwa maana ya Kwamba ukiwaza kwa HEKIMA, Matokeo yake utatenda kwa hekima Kwaiyo hivi ni vitu viwili muhimu sana na vinategemeana hasa HEKIMA Ndio muhimu
Ayubu 28:28
"Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu."
👉kumcha Bwana ndiyo hekima 👉na Ndio usahihi tunao zungumzia Hapa ina maana kua na smart minds ........ukishakua na HEKIMA aise kamwe huwezi kuoa MWANAMKE mpumbavu never LAZIMA hadi unafikia siku ya tukio la kuunganishwa kati ya wewe na mke wako utakua umehakikisha MKE wako ni mwenye HEKIMA hivyo anayo BUSARA Sasa hi Sio KAZI NYEPESI na Sio swala la siku, week, mwezi, au Mwaka it gonna take More than one years B'se HEKIMA ina ambukizwa Mkuu kwa kufundishwa na kiukweli ni wajibu wa MWANAUME kabda , na baada ya kuoa kumfundisha MKE wake Maarifa ili awe na HEKIMA siku zote
Kwaiyo Kuhusu swala la kuletewa MKE baada ya miaka 20 halina Uhalisia wowote ila ni wewe mwenyewe ukikaa mkao wa kua MME na WAKATI wa kuoa umefika utaletewa Mwanamke wako uanze KUMBADILISHA kua MKE na kuna gharama kubwa Sana hapa B'se it need a lot of time For this phenomena
to change a women into prudent wife
Na kuna viashiria utawekewa NDANI Yako juu ya MWANAMKE utakae kua una muandaa kua MKE mwenye BUSARA na utafahamu Hakika huyu ndiye wa ubavu Wangu 😁
hupewa na BWANA Sio kwamba utashushiwa kama mvua hapana ni tukio ambalo litachukua muda KIDOGO Hadi kukamilika na tunajua hi miili YETU ni nyumba (hekalu) la MUNGU ina maana MUNGU lazima aweke makazi NDANI ya mwili wako then atakua anakuongoza katika Mambo yote hata hili la kumuandaa mke mwenye busara Kwaiyo this phenomena honestly inategemea sana mahusiano binafsi kati ya MWANAUME na MUNGU wake
Kuna kitu nimalizie hapa utawezaje kujua kwamba This girl NDIE MKE Wangu ambae MUNGU amenikilimia haijalishi ni alikua kahaba au Lah kwa mara ya kwanza utakapo kutana nae ni KWAMBA 👉 atakua msikivu kwa kila kitu SAHIHI unachomwambia/kumfundisha na atakua yupo tayari kubadilika in Short atakua na ITII sio kwako na sio kwasababu ya KAZI, au pesa au mali zako Sasa hapo ni kua makini B'se wanawake wengi waigiza upendo means atakutii kwasababu ya vitu, pesa au Mali zako na ukishindwa kutofautisha hapa kiukweli utaingia choo cha kike na utajuta
MWANAMKE usimtangulizie vitu au pesa au Mali kamwe hatokua MWEMA Kwako , mwanamke mtangulizie maarifaa na HEKIMA na atakukumbuka na kukushukuru milele
Sasa kama MWANAUME upo kwaajili ya ngono hapo lazima utamtangulizia mwanamke vitu ili kumshawishi na kumlaghai akupe tunda na hu msingi sio mzuri kwa NDOA B'se MTU anaweza kula tunda before NDOA akalielewa then akaweka NDANI aise kwa hu Msingi Lazima utapigwa na kitu kizito Kama jamaa YETU hapo juu
NDOA ni swala seriously Sana na sensitive ila kwa Sasa linachukuliwa simple Sana Ndio maana madhara yamekua makubwa sana kila Siku tunasikia wana ndoa wanatoana uhai na rate ya talaka ipo juu sana ni kwasababu watu tumeacha misingi ya NDOA na kujitwalia wake bila utaratibu
Mithali 2
17 Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake.
18 Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.
rafiki wa ujana 👉 mke au mme wako
agano la Mungu wake 👉 NDOA (i.e vile viapo mlivyo nena kwa vinywa vyenu katika madhabahu ya MUNGU)
Sasa kumuacha mke au mume wako na kuvunja NDOA ya MUNGU ( kulisahau AGANO la wake) ni hatari sana kwakweli kama tunavyo ona kwenye verse ya chini yake 👇
Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.
KOSEA VITU VYOTE LAKINI USIKOSEE KUOA AU KUOLEWA 📌