Mama mkwe anamhimiza mke wangu anichune; naomba ushauri

Mama mkwe anamhimiza mke wangu anichune; naomba ushauri

Naingia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Pole sana, deal nae perpendicular ila mwanamke mwenye tamaa yq mali hata kwa waganga atakuendea

Kama mama mzazi ndio mwenye akili hizo, basi hapo huna mke
 
Your case is very complicated.

1st of all jaribu kujua msimamo wa mke wako, je yupo upande wa wako au wa Mama ake?? Umesema alimjibu mama ake "sawa mama nimekuelewa" ila hilo ni jibu tata, hata mm wazazi wangu wakinambia kitu ambacho sikubaliani nacho na sitaki nigombane nao ntajibu hivohivo kama huyo mkeo na sitofanya chochote, so tafuta kujua msimamo wa mkeo ukoje, hapo sasa inabidi utumie tricks za kiume kama kujifanya umefulia, kama utafikiria njia zingine sawa apply them.

Ukishajua msimamo wa mkeo na upendo wake kwako umelalia wapi, bac unaweza sasa uka proceed kufanya maamuzi mengine magumu.

Hii ni kama midlife crisis, kukosea kuoa kunaweza kufanya maisha ya mwanaume yakawa miserable hadi anakufa, Good Luck broo.


"kukosea kuoa kunaweza kufanya maisha ya mwanaume yakawa miserable hadi anakufa, Good Luck broo"📌
 
Wakuu mnazidi kututisha kama mambo yenyewe ndio hayo, sasa yale maviapo makanisani na misikitini ya nini, ivi MUNGU huwa anaweka baraka kweli kwa ndoa za kitapeli?, bora nisije oa kbsaa maan nitaenda jela.
 
Me Kila siku huwa nasema Hapa

MKE ana thamani kubwa Sanaaaaaaa... Wala thamani yake haiwezi kulinganishwa na vyote vitamanikwavyo juu ya hi ardhi

Kama thamani ya MKE ni kubwa Sana basi hata kumpata huyo mke kuna gharama kubwa Sana na Sio ya fedha wala mali

Na ukiwaambia vijana haya maneno wanakujia juu Sana na Wakati huo wanaapetite ya kuoa na kuingia katika NDOA

Kuna tofauti kati ya MKE na MWANAMKE

Kama hi simulizi ni ya Kweli basi huyu Mkuu ameoa MWANAMKE na Sio MKE na ni HATARI Sana kwa future ya MWANAUME kuoa MWANAMKE

Tazama yaliyomkuta kamwe MWANAMKE hawezi kua na huruma na wewe, atakuigizia upendo fake na target yake ipo kwenye Pesa na mali zako

Wanaume walifanikiwa kuoa WANAWAKE wamekufa mapema Sana



Nakazia Tena kwa vijana wenzangu wa kiume

KOSEA VITU VYOTE ILA USIKOSEE KUOA.... TAFUTA MKE UOE USIKUBALI KUOA MWANAMKE ATAKUMALIZA 📌

NOTE : ILI UPATE MKE LAZIMA NA WEWE UWE MME
 
😂😂😂😂😂😂

TAFUTA MKE kijana uoe, usioe MWANAMKE
huyo unampta wapi mkuu? hao walioend age ni used wakutupwa, hivi vibint vya 2000 bado vinataka kula bata wee, havijui maisha, sometimes nikifikiriaga sana nasema potelea mbali bora nije nizalishe nilee wanangu tu.
 
Mkuu simple sana, fanya uchunguzi anapendelea nini, mtume binti yake ampelekee kama mara 3 hivi safar ya nne peleka mwenyewe. Kisha siku nyingine mwambie kuna kitu mkwe nataka kukutana nawe nikuelezeee unishauri, akija muitie sehem lounge kali sana, mpe anavyopenda kula na kunywa, ksiha muombe radhi umeitwa dharula, kwa vile anapenda hela muachie laki mezani. Mwamvie utamuita tena, wakat unafanya hayo unamsoma respond yake, pia unamvuta aanze kukuwaza.

Ukimaliza hii hatua nirejee hapa nikupe point ya kumalizia vua chupi hiyo maza ujenge heshima.
Ikibidi naweza kumpelekea ili kulipiza fedha zangu ambazo nimetumia kumjengea choo na jiko la kisasa lakini naanzia wapi mkuu?
 
Jambo ni moja kuwa kila mnachofanya sio kwa ajili yenu tu bali na kwa watoto wenu, hivyo hamna budi kuhakikisha mnajenga misingi bora kwa ajili ya siku zijazo.

Asipoelewa hapo huko mbele sikio la kulia litakuwa kwako wakati la kushoto lipo kwa mama na ndoa itakuwa kwenye vikwazo.
 
huyo unampta wapi mkuu? hao walioend age ni used wakutupwa, hivi vibint vya 2000 bado vinataka kula bata wee, havijui maisha, sometimes nikifikiriaga sana nasema potelea mbali bora nije nizalishe nilee wanangu tu.

Mithali 19:14

"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana"

Inategemea mahusiano YAKO na MUNGU wako, kama ni mazuri atakuongoza kupata MKE 😁
 
Mkuu simple sana, fanya uchunguzi anapendelea nini, mtume binti yake ampelekee kama mara 3 hivi safar ya nne peleka mwenyewe. Kisha siku nyingine mwambie kuna kitu mkwe nataka kukutana nawe nikuelezeee unishauri, akija muitie sehem lounge kali sana, mpe anavyopenda kula na kunywa, ksiha muombe radhi umeitwa dharula, kwa vile anapenda hela muachie laki mezani. Mwamvie utamuita tena, wakat unafanya hayo unamsoma respond yake, pia unamvuta aanze kukuwaza.

Ukimaliza hii hatua nirejee hapa nikupe point ya kumalizia vua chupi hiyo maza ujenge heshima.
Huyu mother kweli anaudhi sana aisee! Dawa yake inaweza kuwa hiyo mkuu. Ngoja nitafute ujasiri kwanza.
 
Tulishasema tukatae ndoa jamani.
Me sina cha kuchangia sababu ni scenario sijawahi experience na sitarajii, Mungu anisaidie. Mke wangu alinikuta tayari nina baby mama ambao situation za kuwaoa zilikuwa almost ni impossible but ever since niko naye, hayo ya michepuko nimewaachia wenzangu. Mimi ni wa mke wangu tu.
😂😂😂😂😂😂😂😂 Jamii forum ina bipolars
 
Back
Top Bottom