Mama mkwe anamhimiza mke wangu anichune; naomba ushauri

Naumia sana mkuu hasa ukizingatia sina namna ya kurejesha ghrama zangu
Shimo lenyewe wanatushangaa kwanini hata tunalipia hela za mahali,hawa wadudu sio poa kabisa,kama una uwezo acha
kila kitu,Kumbuka wanaweza kukuua wakifanikiwa mission Yao
Kuna jamaa kafukuzwa kwake Dsm na jumba lake.la gholofa kalikimbia na amekuwa confused hata biashara zote akifanya.mke anaziaharibu ili Mwamba ateseka,hawa watu ni hatari sana nina kesi nyingi za wanaume waliobugi kama mimi wanawake akikuwahi,done deal.
Lakini kama Kuna haja stay away from that toxic familia
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Achana na huyo Mke uishi na Mama Mkwe.
 
Majuto ni mjukuu. Najuta kumjua huyu mwanamke.
Bado hujachelewa,mpige chini anza upya,huko mbeleni hakuna dalili nzuri,

Utaishi na huyo mkeo kwa maisha ya wasiwasi tu,

Life is too short,usiishi kwa kujitesa,piga chini kabla hujamzalisha ili watoto wasije kuteseka na single mother,sioni future ya ndoa hapo.
 
Your case is very complicated.

1st of all jaribu kujua msimamo wa mke wako, je yupo upande wa wako au wa Mama ake?? Umesema alimjibu mama ake "sawa mama nimekuelewa" ila hilo ni jibu tata, hata mm wazazi wangu wakinambia kitu ambacho sikubaliani nacho na sitaki nigombane nao ntajibu hivohivo kama huyo mkeo na sitofanya chochote, so tafuta kujua msimamo wa mkeo ukoje, hapo sasa inabidi utumie tricks za kiume kama kujifanya umefulia, kama utafikiria njia zingine sawa apply them.

Ukishajua msimamo wa mkeo na upendo wake kwako umelalia wapi, bac unaweza sasa uka proceed kufanya maamuzi mengine magumu.

Hii ni kama midlife crisis, kukosea kuoa kunaweza kufanya maisha ya mwanaume yakawa miserable hadi anakufa, Good Luck broo.
 
Badilika anza kuwa huna hela usimshirikishe mambo yako. Badilika ghafla. Usimwambie kitu.

Hapo umekutana na kausha damu.
Sali sana mzee hao ni vigagula visokoropwinyo vibaka kabsa....

Ila haya mambo ya mapenzi unaweza kurudi home ukamwaga siri wana JF ndio tumekushauri. Akatuloga na sisi.😄... penzi la limbwata noma sana....

Kabla sijasahau. Mtie mimba dabo dabo amsahau mama yake awe busy.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Sasa tatizo la mkeo au Mama mkwe? Unaanza kumhukumu juu ya watoto, hata hamjazaa? Anakuibia kivipi na duka ni lenu?
 
Kweli kabisa mkuu. Kwa hayo mambo makuu niliyomtendea mke wangu na familia yake sikutarajia kama mama mkwe angenifanyia umafia kama huu.
Kata misaada kiujanja na akikisha una Mfilisi mtaji ulio mfungulia na chuguza Bank ana Akiba ya kiasi gani.
 
Kadri siku zinavyoenda ndo identify ya mwanaume inavyopotea, umeshajua nini kinaendelea siyo kwa kusimuliwa bali kwa kuona kwa kukusaidia fanya mambo mawili kati ya haya, mwite mwambie kila kitu option hii kama bado unampenda na bado unataka kuendelea na ndoa japo kuna asilimia nyingi huko mbele itakuja kukukost option ya pili inahitaji moyo wa chuma vunja ndoa achana nae kwa amani itakusumbua mwanzoni lakini hiyo ndiyo dawa ya kudumu the option is up to u bro
Mkuu hiyo option ya pili wanaiweza Wazungu kwa %100
 
Kadri siku zinavyoenda ndo identify ya mwanaume inavyopotea, umeshajua nini kinaendelea siyo kwa kusimuliwa bali kwa kuona kwa kukusaidia fanya mambo mawili kati ya haya, mwite mwambie kila kitu option hii kama bado unampenda na bado unataka kuendelea na ndoa japo kuna asilimia nyingi huko mbele itakuja kukukost option ya pili inahitaji moyo wa chuma vunja ndoa achana nae kwa amani itakusumbua mwanzoni lakini hiyo ndiyo dawa ya kudumu the option is up to u bro
Ijapokuwa bado nampenda na ananipa mambo ya nguvu kitandani, sasa uvumilivu wangu umefika. Ndugu zangu wengi nilioongea nao pia walinipa hii option namba 2 lakini nahitaji kwanza kukusanya ujasiri kabla ya kutekeleza hilo mkuu.
 
Back
Top Bottom