Mama mkwe anamhimiza mke wangu anichune; naomba ushauri

Cku za mwanzo za ndoa akili za wanawake wengi bado zinakaa kinyumbani zaidi,Unatakiwa kumtoa nyumbani kifkra kumweka kwako.Usifadhaike we mpime mkeo kama anakupenda,an zidisha upendo,tafuta jinsi ya kumweka mbali na mamaake (anaonekana alikuwa mchunaji ujana wake),kama ana ratiba ya kwenda kwa mama ake kila wkend tafuta jinsi ya kuipiga chini kwa kumtengenezea ratiba zingine
Mzalishe watoto (muhim sana hili).
 
Kadri siku zinavyoenda ndo identify ya mwanaume inavyopotea, umeshajua nini kinaendelea siyo kwa kusimuliwa bali kwa kuona kwa kukusaidia fanya mambo mawili kati ya haya, mwite mwambie kila kitu option hii kama bado unampenda na bado unataka kuendelea na ndoa japo kuna asilimia nyingi huko mbele itakuja kukukost option ya pili inahitaji moyo wa chuma vunja ndoa achana nae kwa amani itakusumbua mwanzoni lakini hiyo ndiyo dawa ya kudumu the option is up to u bro
 
Cku za mwanzo za ndoa akili za wanawake wengi bado zinakaa kinyumbani zaidi,Unatakiwa kumtoa nyumbani kifkra kumweka kwako.Usifadhaike we mpime mkeo kama anakupenda,an zidisha upendo,tafuta jinsi ya kumweka mbali na mamaake (anaonekana alikuwa mchunaji ujana wake),kama ana ratiba ya kwenda kwa mama ake kila wkend tafuta jinsi ya kuipiga chini kwa kumtengenezea ratiba zingine
Mzalishe watoto (muhim sana hili).
Hakuna kitu kama hicho huwezi badili akili na fkra za mtu mzima sana atabadili mbinu tuu lakini lengo lipo pale pale na pengine anaweza tengenezewa mbinu za kumtoa uhai kabsa ili mke arithi mali
 
Naungia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Wamama wa mjini ni shida sana. Wanawafanya wanao kama kitega uchumi. Na ukute mipango yote anayokuambia mkeo ya kimaisha anakuwa ameelekezwa na mama ake. Pole sana mwamba
 
Cc Natafuta Ajira
FB_IMG_1713899152545.jpg

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Uliyoandika yote hayo nimeona ni ya kawaida sana, ila kipengele ulichosema kuwa mama yako haujamfanyia jambo la maana kwa mfano huo!! nimejikuta naumia sana.

Pole sana brother, napenda kukushauri lakini tueleze kwanza msimamo/majibu ya mkeo yalikuwaje kwa mama yake?
Asante sana mkuu. Alikubali masharti ya mama yake
 
Naungia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Mkuu sijasoma uzi wote, ila mama mkwe anae ingiilia anga zako mpelekee moto
 
Wamama wa mjini ni shida sana. Wanawafanya wanao kama kitega uchumi. Na ukute mipango yote anayokuambia mkeo ya kimaisha anakuwa ameelekezwa na mama ake. Pole sana mwamba
Asante mkuu. Yaani hawa wakwe wa mjini wanatia hasira sana
 
Back
Top Bottom