Mama mkwe anapokua mwiba kwenye ndoa

Mama mkwe anapokua mwiba kwenye ndoa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Rafiki yangu alikwenda kusaidia nyumbani kwa mtoto wake wa kiume. Hawakuwa na msichana wa kazi hivyo mtoto wake ambae ndiye mume alimuomba aende mjini kwa muda.

Ameishi miezi mitatu, mama mke wa mwanae ameamua kuhamia hotelini na kumwambia mume wake, hataridi nyumbani mpaka mama yake awe ameondoka.

Mama wengine wanaona mke amekuja kuwa princess kwenye nyumba ya mwanae. Hawajui kuwa mke pia anasaidia majukumu ya nyumbani ili mradi maisha yaende.
 
Mume alimwomba mama mkwe aje mjini ambako ndo naishi mimi na mume wangu,na sababu za kumtaka mama mkwe aje ni ukosefu wa binti wa kaz home.

Mama mkwe kakaa miez mitatu mimi nishachoka nimeamua nifanye mgomo wa kwenda kuishi hotelini nikimtaka mume wangu amwondoe mama yake ndipo nani nitarudi kunyumba
 
Ila haya mama yanaangukia sana upande wa mama mkwe na mke.

Si upande wa pili wa baba mkwe.
 
Shida hapo kila mtu anajihesabia haki kwa kijana....

Mama (huyu ni mwanangu na hapa ni kwake nina haki zote juu yake)
Dada ( huyu ni kaka angu na hapa ni kwake nina haki zote kwake)
Mke (huyu ni mme wangu na hapa ni kwangu/kwetu nina haki zote)

Ukijumlisha na akili zetu wanawake zilivyo, tabu tupu.
 
Sawa teacher!
 
Halafu ndugu wa mume wanaona kama vile mke ni wa kupita tu na anaweza kuachwa any time (hata kama tayari ana watoto). Hii hasa ni kwa jamii zinazoruhusu talaka.
 
Mke, ma mkwe na wifi hawa viumbe wakiketi pamoja hugombea utawala na hiki ndo chanzo cha mitifuano yao, ni wakwe/mawifi wachache sana wanaoweza ishi na wake zetu kwa amani.
Labda uoe kwenye familia ambayo ni rafiki wa mama, at least wanaweza kupatana kidogo.
 
Hivi siku hizi unann???

Sio kwamba unatumia Misamiati migumu hapanaa

Ila kiswahili chako ,sentensi hazieleweki .

Unaandika unakimbia?? Kama yule jamaa wa Irudiwee
Hahahaaa mkuu wala sio siku hizi tu dadaangu Sky ndo muandiko wake hivi hivi tangu na yangu

Na kuna mwingine wa kuitwa Pdidy dah hawa huwa natulia nasoma mara 3 ndo naelewa😂😁
 
Back
Top Bottom