Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Kijana , umri miaka 30 , alifiwa na mke wake ambaye walikuwa na mtoto mmoja tu wa kike umri wa miaka 2.
Mwana-uume huyo alikuwa akiishi nyumba moja na mama mkwe wake pamoja wamashemeji zake kwakuwa walikuwa hawana pa kukaa na nyumba ilikuwa na hati jina ni la huyo mwanaume.
Mke alifariki baada ya ajali , mama mkwe akasubiri mume ameenda kazini akaiba vitu vyote vya nyumbani pamoja na kuiba mtoto, mume akaamua kwenda Mahakamani hapa Mbeya kudai mali ambaopo mama mkwe alikana kuiba na kudai yeye ndio alikuwa anamlea mkwe wake na pili akasema mtoto ni mdogo kwahiyo abaki na huyo mtoto na mahakama ya watoto ikasema kweli mtoto ni wa kike na mdogo hivyo abaki na bibi yake.
Mume ameoa mke mwengine mpya, sasa anataka mtoto wake aliyeachwa na marehemu na mtoto amefika miaka 7 ila bibi hataki kumuachia mtoto.
Lakini pia, bibi na naye ameingia mahakamani pale Mahakama Jumuishi Kituo cha Temeke anataka mirathi, kwamba na yeye ni mrithi wa marehemu na ameweka zuio kwenye kesi iliyokuwa imefunguliwa .
SWALI:-
1. Hivi huyu mume na mke wangekuwa wanakaa mbali, say AFRIKA KUSINI, huyu bibi angeweza kupora mali, angeweza kudai naye ni mrithi? angeweza kufanya vioja vyote hivi?
2. Je, huyu baba tumshauri nini kwenye ndoa yake mpya kuhusu kukaa na wakwe?
3. Tumshauri nini kuhusu mapenzi?
4. Tumshauri nini kuhusu mirathi na haki zake?
5. huyu mwanaume sasa ameoa mke mwengine, je akae muda gani kwenda kumchukua mtoto wake aishi na mama mpya?