Mama mkwe apora Mali za marehemu, mgane alia kwa uchungu mahakamani!

Mama mkwe apora Mali za marehemu, mgane alia kwa uchungu mahakamani!

Kijana mmoja , umri miaka 30 , alifiwa na mke wake ambaye walikuwa na mtoto mmoja tu wa kike umri wa miaka 2.

Mwanaume huyo alikuwa akiishi nyumba moja na mama mkwe wake pamoja wamashemeji zake kwakuwa walikuwa hawana pa kukaa.

Mke alifariki baada ya kuugua, mama mkwe akasubiri mume ameenda kazini akaiba vitu vyote vya nyumbani pamoja na kuiba mtoto, mume akaamua kwenda Mahakamani hapa Mbeya kudai mali ambaopo mama mkwe alikana kuiba na kudai yeye ndio alikuwa anamlea mkwe wake na pili akasema mtoto ni mdogo kawhiyo abaki na huyo mtoto na mahakama ya watoto ikasema kweli mktoto ni wa kike na mdogo hivyo abaki na bibi yake.

Mume ameoa, sasa anataka mtoto wake na mtoto amefika miaka 7 ila bibi hataki kumuachia mtoto.
Lakini pia, bibi na naye ameingia mahakamani anataka mirathi, kwamba na yeye ni mrithi wa marehemu.
SWALI:- Hivi huyu mume na mke wangekuwa wanakaa mbali, say AFRIKA KUSINI, huyu bibi angeweza kupora mali, angeweza kudai naye ni mrithi? angeweza kufanya vioja vyote hivi?

Je, huyu baba tumshauri nini kwenye ndoa yake mpya kuhusu kukaa na wakwe?
Tumshauri nini kuhusu mapenzi?
Tumshauri nini kuhusu mirathi na haki zake?​
Alilipa mahari?
 
Mtoto ni wa kike, soma tena uzi wa mtoa mada.

Pia, Tabia ya mtoto inaweza kuharibika kwa namna yoyote ile, kama akifata tabia za mama mkwe kwani mke wake alilelewa na nani?

Mwanaume ana udhaifu ndio maana haya matatizo yametokea, yeye ndio kasababisha kufikia hapa wanamchukulia poa na kumfanya mjinga.

Busara ni kuacha kila kitu kiende na akomae na shughuli zake za kila siku.

Dunia ina kila kitu hii asishikilie upande mmoja.
Yaani amtekeleze mtoto wake?
Huna akili.
 
1. Kalipa mahari.
2. Kafunga ndoa kanisani.
3.Alikuwa anasaidia kusomesha shemeji zake wawili.
Asimame kwenye nafasi yake kama mwanaume, all will be well. Asimtelekeze mtoto wake. Ukweni kuna tabia za hovyo pia, it doesnt help na haina maana kabisa kulelewa mtoto wako ukweni.
 
Huyo mtoto yeye atakuwa hana urithi wowote!?
Hujawahi kusikia wazazi wamekufa mahakama inahamuru mali zigawanye kwa asilimia fulani kwa wazazi wa marehemu na watoto wa marehemu?

Watz hatufanyi mambo kwa kuwashirikisha wanasheria ila kuna miongozo mingi ya kuandikishana mali za wanandoa ikiwemo mnaandika majina yenu kwenye jinsi mmoja akifa umiliki wote 100% unahamia kwa aliyekua hai na kuna jinsi ya kuandika majina yenu mmoja akifa umiliki unagawanywa kwa aliyebaki na warithi wengine wa marehemu.

Wanasheria wa jf watakuja kufafanua vizuri.
 
Hapo amefariki mzazi mmoja.
Ndio bibi ana haki ya kudai urithi sababu mtoto wake ana share.

Bibi upande wa mama naamini kabisa anafanya hayo kwa manufaa ya mjukuu wake kumbuka huyo kijana ataoa na kupata watoto wengine hivyo bibi anachukua urithi wa mjukuu wake mapem tena kijanja.

Angekua bibi wa upande wa baba ningejua tu ni tapeli😎
 
Mama mkwe anachekesha sana kama sio mama ako mzazi ila UMASKINI NI MBAYA SANA
 
Achukulie tu amemzawadia mtoto wake, yeye akapambane upya kwenye utafutaji pamoja na mke mwingine.
 
Aise, wewe utakuwa mchungaji au mwanasheria. Ushauri mzuri sana. Huyu kijana akisoma huku atafarijika sana.
Wanaume wanapitia mateso mengi sana wanapofiwa, msione wanakesha baa tunawaita "walevi" wana mengi yasiyo zungumzika!
Asante sana kupokea ushauri huu
 
Ilikua kazi ndogo sana ningemwomba uchi tu mama mkwe analiwa na anarudisha hati hizo
 
Yaani amtekeleze mtoto wake?
Huna akili.
Sio kumtelekeza, ushawahi kujiuliza mtoto anajengekaje kisaikolojia baada ya mzazi kufa na anaona wakubwa wanagombania mali?

Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake mwanaume pia ana udhaifu mkubwa hasa wa kufanya maamuzi mazito. Mahusiano huamuliwa kwa hisia sasa mahakama inaamua kulingana na sheria za nchi, utakua mpumbavu ukiamini sheria ya nchi ipo kwa ajili ya kukuliwaza.

Nnaposema aache maana yake ni kua ajiimarishe, kiuchumi, kiupambanaji ili asilielie huku mitandaoni, Anatafuta msaada sababu ameshindwa kutatua hili tatizo, na yupo sahihi kutafuta mawazo ya watu wengine wamsaidie ila anatakiwa akubali kuweka hisia pembeni na akubali kukabiliana na uhalisia ili kesho isimame.

Mtoto ni wake, kumuacha kwa bibi yake sio kumtelekeza, ni jukumu lake kuhakikisha mtoto anaendlea vizuri anakula vizuri kuvaa vizuri kusoma shule nzuri. Amejaribu kumhamishia shule nzuri mtoto bibi akakataa? amemuhudumia mtoto huyo bibi akakataa? kuna ambae amesikiliza upande wa bibi? Yeye ni mwanaume na mtoto ni wa kike akimchukua anaenda kukaa nae geto au? mazingira anayoishi mwanaume saivi ni rafiki kwa mtoto na familia? Mwanaume saivi ana mpango wa kuoa au yupo kwenye mahusiano mengine? maana mama kafa mtoto akiwa na miaka 3 saivi ana 7. ni miaka 4 imepita, hana mke mwingine?

Kama shida ni malezi, Huyo mke wake aliefariki alilelewa na nani? alimpenda akiwa na tabia mbovu? kama alikua ana tabia njema nini kitabidlisha mtoto wake na asiwe na tabia njema kama mama yake?

mwanamume anaonekana ni dhaifu, akimchukua mtoto akampeleka kwao huoni tutapata mtu mwingine atakaekuja kulalamika humu mitandaoni baada ya miaka 20?

Mwisho nakurudia wewe pia, Uliwahi kutelekezwa? Umesema kua Ukweni kuna tabia za hovyo maana yake hiyo ni experience ya maisha yako, Ukweni kwako kuna tabia gani za hovyo? kwanini umeoa sehemu ukweni wana tabia za ajabu? una kigezo gani kua hata kwenu kwenye macho ya wengine ni watu wa hovyo?.

Mtoto muacheni akue bila kuangalia watu wazima mnashikana mashati na kugombania mali, mtoto atapoteza stability, na kuanza kupanda chuki zisizo za msingi, chuki za kurithishwa. Baba ajiimarishe na amuhudumie mtoto huko huko alipo ili mtoto amtambue baba na ampende, apende ndugu zake aliowakuta sababu yeye hajachagua, amewakuta tu.

Mwanaume mke kafa miaka 4 iliyopita huyu atuambie ukweli kama haoi tena, kama anaoa pia aseme ukweli, na atuambie mtoto atakulia kwa mama wa kambo au hamna.

Muambie aache hizo mali na apambane upya. Akiacha saivi baada ya miaka 3 mtoto atakua na miaka 10, na yeye atakua amepata mwanga mpya wa maono ya kuiona kesho.

Adhuhuri njema.
 
Inawezekana mali zote zilikuwa za mke aliyefariki na inawezekana pia alipewa na mama yake ndio maana mama kapata ujasiri huo.
Na inawezekana mtoto pia alibambikiwa
 
Back
Top Bottom