Mama mkwe apora Mali za marehemu, mgane alia kwa uchungu mahakamani!

Alilipa mahari?
 
Yaani amtekeleze mtoto wake?
Huna akili.
 
1. Kalipa mahari.
2. Kafunga ndoa kanisani.
3.Alikuwa anasaidia kusomesha shemeji zake wawili.
Asimame kwenye nafasi yake kama mwanaume, all will be well. Asimtelekeze mtoto wake. Ukweni kuna tabia za hovyo pia, it doesnt help na haina maana kabisa kulelewa mtoto wako ukweni.
 
Huyo mtoto yeye atakuwa hana urithi wowote!?
Hujawahi kusikia wazazi wamekufa mahakama inahamuru mali zigawanye kwa asilimia fulani kwa wazazi wa marehemu na watoto wa marehemu?

Watz hatufanyi mambo kwa kuwashirikisha wanasheria ila kuna miongozo mingi ya kuandikishana mali za wanandoa ikiwemo mnaandika majina yenu kwenye jinsi mmoja akifa umiliki wote 100% unahamia kwa aliyekua hai na kuna jinsi ya kuandika majina yenu mmoja akifa umiliki unagawanywa kwa aliyebaki na warithi wengine wa marehemu.

Wanasheria wa jf watakuja kufafanua vizuri.
 
Hapo amefariki mzazi mmoja.
Ndio bibi ana haki ya kudai urithi sababu mtoto wake ana share.

Bibi upande wa mama naamini kabisa anafanya hayo kwa manufaa ya mjukuu wake kumbuka huyo kijana ataoa na kupata watoto wengine hivyo bibi anachukua urithi wa mjukuu wake mapem tena kijanja.

Angekua bibi wa upande wa baba ningejua tu ni tapeli😎
 
Mama mkwe anachekesha sana kama sio mama ako mzazi ila UMASKINI NI MBAYA SANA
 
Achukulie tu amemzawadia mtoto wake, yeye akapambane upya kwenye utafutaji pamoja na mke mwingine.
 
Aise, wewe utakuwa mchungaji au mwanasheria. Ushauri mzuri sana. Huyu kijana akisoma huku atafarijika sana.
Wanaume wanapitia mateso mengi sana wanapofiwa, msione wanakesha baa tunawaita "walevi" wana mengi yasiyo zungumzika!
Asante sana kupokea ushauri huu
 
Ilikua kazi ndogo sana ningemwomba uchi tu mama mkwe analiwa na anarudisha hati hizo
 
Yaani amtekeleze mtoto wake?
Huna akili.
Sio kumtelekeza, ushawahi kujiuliza mtoto anajengekaje kisaikolojia baada ya mzazi kufa na anaona wakubwa wanagombania mali?

Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake mwanaume pia ana udhaifu mkubwa hasa wa kufanya maamuzi mazito. Mahusiano huamuliwa kwa hisia sasa mahakama inaamua kulingana na sheria za nchi, utakua mpumbavu ukiamini sheria ya nchi ipo kwa ajili ya kukuliwaza.

Nnaposema aache maana yake ni kua ajiimarishe, kiuchumi, kiupambanaji ili asilielie huku mitandaoni, Anatafuta msaada sababu ameshindwa kutatua hili tatizo, na yupo sahihi kutafuta mawazo ya watu wengine wamsaidie ila anatakiwa akubali kuweka hisia pembeni na akubali kukabiliana na uhalisia ili kesho isimame.

Mtoto ni wake, kumuacha kwa bibi yake sio kumtelekeza, ni jukumu lake kuhakikisha mtoto anaendlea vizuri anakula vizuri kuvaa vizuri kusoma shule nzuri. Amejaribu kumhamishia shule nzuri mtoto bibi akakataa? amemuhudumia mtoto huyo bibi akakataa? kuna ambae amesikiliza upande wa bibi? Yeye ni mwanaume na mtoto ni wa kike akimchukua anaenda kukaa nae geto au? mazingira anayoishi mwanaume saivi ni rafiki kwa mtoto na familia? Mwanaume saivi ana mpango wa kuoa au yupo kwenye mahusiano mengine? maana mama kafa mtoto akiwa na miaka 3 saivi ana 7. ni miaka 4 imepita, hana mke mwingine?

Kama shida ni malezi, Huyo mke wake aliefariki alilelewa na nani? alimpenda akiwa na tabia mbovu? kama alikua ana tabia njema nini kitabidlisha mtoto wake na asiwe na tabia njema kama mama yake?

mwanamume anaonekana ni dhaifu, akimchukua mtoto akampeleka kwao huoni tutapata mtu mwingine atakaekuja kulalamika humu mitandaoni baada ya miaka 20?

Mwisho nakurudia wewe pia, Uliwahi kutelekezwa? Umesema kua Ukweni kuna tabia za hovyo maana yake hiyo ni experience ya maisha yako, Ukweni kwako kuna tabia gani za hovyo? kwanini umeoa sehemu ukweni wana tabia za ajabu? una kigezo gani kua hata kwenu kwenye macho ya wengine ni watu wa hovyo?.

Mtoto muacheni akue bila kuangalia watu wazima mnashikana mashati na kugombania mali, mtoto atapoteza stability, na kuanza kupanda chuki zisizo za msingi, chuki za kurithishwa. Baba ajiimarishe na amuhudumie mtoto huko huko alipo ili mtoto amtambue baba na ampende, apende ndugu zake aliowakuta sababu yeye hajachagua, amewakuta tu.

Mwanaume mke kafa miaka 4 iliyopita huyu atuambie ukweli kama haoi tena, kama anaoa pia aseme ukweli, na atuambie mtoto atakulia kwa mama wa kambo au hamna.

Muambie aache hizo mali na apambane upya. Akiacha saivi baada ya miaka 3 mtoto atakua na miaka 10, na yeye atakua amepata mwanga mpya wa maono ya kuiona kesho.

Adhuhuri njema.
 
Inawezekana mali zote zilikuwa za mke aliyefariki na inawezekana pia alipewa na mama yake ndio maana mama kapata ujasiri huo.
Na inawezekana mtoto pia alibambikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…