Mama mkwe apora Mali za marehemu, mgane alia kwa uchungu mahakamani!

hizo blah blah umeandika hapo juu, hazina mantiki kwa upande wangu.

what i know and have observed kuanzia nikiwa mdogo ni kwamba mwanaume aliyeoa kwa kufata taratibu zote zinazotakiwa na jamii kwa ujumla, ikitokea mwanamke wake akapoteza maisha, next of kin upande wa mali na mtoto/watoto anapaswa kuwa mume wake.

kuniambia kwamba mama mkwe anamngangania mtoto wa jamaa nadhani kuna jambo tunafichwa na halipo sawa. Mimi pia nina watoto na hata leo hii mzazi mwenzangu akitangulia mbele ya haki, Mwanangu hakuna sehemu anaenda. Wakwe zangu infact, Hawawezi hata jaribu kuleta hayo mawazo karibu yangu.
 
Inagawanywa wazazi, mtoto, baba
Tungepata mwanasheria hapa ingekua rahisi kuelewana.

Kumbuka huyo bibi mzaa mama anataka urithi kwa manufaa ya mjukuu wake.
Wewe na huyo bibi akili yenu ni moja na ina ujinga ndani yake. Wewe ni mkwe unatakaje urithi wa mwanangu wakati mimi niko hai?

Huyo bibi hana hata hiyo mandate ya kupora mtoto angali ni mkubwa, na sheria haiko upande wake.

Huyo jamaa ni mzembe kiasi cha kutosha.
 
Upo sahihi kwa upande wako, lakini usahihi wako unauzungumzia wewe hapo MR DELETED. na sio huyo mwingine, experience za maisha yako ni tofauti kabisa na za huyo mwingine. Baba yako, mama yako na uliokua nao Huyu anaeomba ushauri hajalelewa na hao, Huenda mmetofautiana kabila, dini na elimu vyote mmetofautiana.

Mwisho kabisa, zingatia wewe mwenyewe umesema "KWA UPANDE WANGU" Hivyo ishi hapohapo, Lakini tukirudi kwa upande wa huyu jamaa sisi hatuna shauri la maana zaidi ya porojo sababu "Hatujasikia upande wa pili"
 
kwani kwenye ndoa mpya pia anakaa na wakwe?
 
Hiyo nyumba kajenga nani? Tuanzie hapo, mama mkwe ameanzaje kudai urithi kwenye mali ambazo hakutafuta yeye na kuna mtoto yupo? Kuna jambo nyuma ya pazia haliko sawa
 
Hiyo nyumba kajenga nani? Tuanzie hapo, mama mkwe ameanzaje kudai urithi kwenye mali ambazo hakutafuta yeye na kuna mtoto yupo? Kuna jambo nyuma ya pazia haliko sawa
Nyumba imejengwa na Kijana , hati ya ARdhi tena ya mfumo inasoma jina la kijana peke yake.
 
kwani kwenye ndoa mpya pia anakaa na wakwe?
Mama mkwe alikuja kama kuwapikia si unajua ndoa changa ni kukaa chumbani na kanga moja? Mama mkwe kakaa akawa mwenyeji na akawa anawapikia na kuwatengea chakula chumbani ili shughuli iwe moja tu...!
 
Hiko kibibi ujana wake kiliutumia vp had kudai mirathi hivo, nuksi kweli.. jamaa akaze tu Haki Iko upande wake na hivi kaka kaoa tena hakuna excuse kwamba mtoto atalelewa vp.
 
Hakuna neno mgane kwenye kiswahili,mwanaume akifiwa ni mjane na mwanamke akifiwa ni mjane
 
Kweli mkuu hapo umeongea point kubwa huyo Baba anatakiwa akaanze maisha mapya kama ameoa mke mpya anatakiwa wakaanze maisha mapya sehemu yingine na watafute mali upya, hizo maliza walizotafuta na Marehem mkewe anatakiwa azimiliki huyo Mtoto wake kama Mama mkwe ataendelea kuisha na huyo mtoto ni vizuri zaidi, Baba mtoto anatakiwa awe anakwenda kumtembelea mtoto wake na kumpa huduma.
 
Upo sahihi!
 
Hakuna neno mgane kwenye kiswahili,mwanaume akifiwa ni mjane na mwanamke akifiwa ni mjane
Kiswahili kinakuwa kijana wangu, na wewe ukue.
Zamani tuliita "vipofu" sikuhizi watoto hawajui hilo neno wanajua "watu wasio weza kuona"

Zeruzeru --""walemavu wa ngozi"
 
Kiswahili kinakuwa kijana wangu, na wewe ukue.
Zamani tuliita "vipofu" sikuhizi watoto hawajui hilo neno wanajua "watu wasio weza kuona"

Zeruzeru --""walemavu wa ngozi"
Sasa kati ya wewe na mimi nani mkubwa? Mimi ni 64 yrs,kuhusu kujua kwa lugha ni pale ambapo hatuna neno fulani ndipo tunapochukua au kukopa kutoka lugha nyingine.Neno mgane halipo kwenye lugha yoyote ya kibantu,sasa utasemaje ati kiswahili kimekua kwa kuchukua neno toka lugha yoyote ile.Na nchi yetu ni mpaka pale bakita ikithibitisha neno fulani ndipo linakuwa rasmi
 
WEw are almost age mate , the rest jifunza kujifunza kwa wengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…