Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

How many in-laws (brothers and sisters) do you have and what type of relationship do you have with them? Unawatembelea au unawakaribisha vizuri? Your hubby ni mtoto wa ngapi kwenye familia yao?
 
Nadhani shida ni meno tu

1615889130959.png
 
Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
DU POLE SANA, WATANZANIA WENGI KWA SASA WANA CHAGAPHOBIA, USILAZIMISHE UNAWEZA UKAPOTEZA MAISHA YAKO KAMA NDUGU HASA BABA NA MAMA MKWE HAWAKUTAKI. KAMA NI WIFE MATERIAL UTAOLEWA TU.
 
Miss Chuga mdogo angu;
1. Ni wanaume wachache sana ambao wanaweza wakaamua kwenda kinyume na wazazi wao, especially mama zao. Wanawake tukipenda huwa tunaforce kivyovyote huko nyumbani hadi mchumba atakubaliwa, wakibisha sana tunabeba mimba au tunahamia kwa mwanaume bila ndoa, maisha yanasonga. Ila hawa wenzetu, atakaloliamua mama mkwe mara nyingi ndiyo linakuwa final say. Usijiaminishe sana kwamba mchumba wako ana msimamo sana na hautobadilika. Nina rafiki angu Mmachame yalimkuta kama yako, mwisho wa siku mchumba akamwambia mimi siwezi kuendelea na mipango ya ndoa bila wazazi wangu. Ila Mungu sio wakwe, alikuja akaolewa zake na mtu mwingine na yupo anadunda na ndoa yake. (Hopefully wa kwako atapambana hadi mwisho)

2. Kamwe usije ukaungana na mtoto wa mama mkwe kwenda kinyume na mama mkwe; huo utakuwa ni ugomvi wa maisha, na ikiwezekana ugomvi utaendelea hadi kwa watoto wako (ya Hamissa na Mama Diamond). Yes kuna muda wazazi wanazingua, but still tunahitaji baraka zao, hata kama watazitoa kinafki na kuja kujumuika nanyi kwenye sherehe yenu. Usikubali kufunga ndoa na huyo mchumba wako kama wazazi wake hawajaridhia. Yeye anachotakiwa kufanya ni kuwalainisha na kuwaelewesha huko nyumbani kwao hadi waje wakubali. Usishindane na mama mkwe; kesho watapatana na kijana wake ila wewe ndiyo utabaki kuwa adui yake.

Naweza kukuelewa unajisikiaje, aibu unayoiwazia, kuchekwa na kuchambwa na wananzengo, bado muda wako na upendo ulioinvest kwenye hayo mahusiano, labda unaona na umri umeshaenda aisee inaumiza sana. Lakini pamoja na yote hayo, ikitokea imeshindikana kufunga hiyo ndoa; lia mshukuru Mungu kwa yote. Na usije ukakaa unajilaumu sijui ukaharibu maisha yako kisa umeachwa; hujafanya kosa lolote la kukufanya uachike: wewe kuzaliwa mchaga sio kosa wala sio dhambi na huwezi kubadili kabila lako ili kuwaridhisha wakwe. Kuvunjika kwa uchumba sio mwisho wa maisha

Imagine ukiforce hiyo ndoa, utaishi maisha ya aina gani na wakwe zako? Usije ukajidanganya kwamba labda mtaishi mbali na wakwe zako so ni sawa tu; mdogo angu hao ndugu mtawahitaji tu, na watoto wako watawahitaji hao ndugu wa baba zao pia.

Na usijidanganye kubeba mimba, kwa sababu unaweza kubaki single mom, ndoa isifungwe na hata huyo mtoto wako wasiwe na habari naye. Acha mambo yaende naturally, muache mchumba wako apambane hadi kieleweke. Ikishindikana basi mama, wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kuvunja uchumba, na wakati mwingine ni bora kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa. Familia nyingine unaenda kujipa mateso tu.

Muombe Mungu, mapenzi yake yatimizwe kwenye huo uchumba wenu. Litakalotokea lolote, kubaliana nalo then mshukuru Mungu. Yeye anakuwazia mema siku zote, na anaijua kesho yako.

Na nyie wanaume muulizage mapema kwa mama zenu, wawaambie hawataki muoe kabila gani: sio unakaa na mtoto wa mtu miaka 5 afu ndiyo mama mkwe anakuja "sitaki mchaga sijui mnani". Afu alivyokosa huruma eti aliruhusu kabisa utolewe mahari. Mungu amsamehe, hiyo mbegu isije ikamea kwa mabinti zake.

Ukiona linakuchanganya sana, washirikishe ndugu zako. Usije ukadondoka kwa presha bure. Mungu na akutetee
 
Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
Kwanza jiamini na hakuna jambo geni hapa duniani hata akikuacha utapata mwingine, na hakuna aibu yeyote usiishi kwa kuangalia watu watasemaje
Katika jamii kuna taarifa nyingi kuhusu makabila, kama wanawake wa kichanga wanatuhumiwa kuwa ni wezi,mume akiwa na pesa wanaua, hawapendi wamama au Baba wa Mume, na wako loyal kwa jamii Zao, zarau nk. ukiangalia hizi Tabia ziko kwenye makabila mengine pia hivyo kwa mtu muelewa sio tatizo kwani inategemea sana mtu mwenyewe.
Muulize ujue hasa kwa nini anakataa usiolewe ili kama ni hizo taaria zilizoko kwenye jamii aleweshwe, ajue tuko kwenye dunia ya kisasa na hizo ni stori za zamani.
Kuwa Loyal kwa Jamaa yako, kuwa Rafiki wake na tulizo, kuwa, kuwa mshauri na msaidie kwenye kufanya maazu acha panic. Mtavuka salama
 
Hapa kuna walakini, walakin huo huenda uko upande wako, suala bado analishughulikia tayari ushaanza na kusema kakupotezea muda, bora ungeambiwa mapema, kivipi? msikilize mmeo kile anachokisema mpaka hapo alipofikia ana nia ya dhati ya kukuoa, acha kelele.
 
Kimeumana.

Ndoa ni ya kwenu wengine wote including mama mkwe ni wapewa taarifa tu. Wazazi, ndugu na jamaa wanaweza kuwashauri ila sio kuwaamulia. Kila kitu kina mipaka including wazazi, in this case mama mkwe kavuka mipaka yake. Kama jamaa ana msimamo, mnapendana na mmetoka mbali sema screw it proceed with the plan.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Unaonekana uko vizuri kichwani hivyo wewe msikilize anasemaje lakini pia kumfahamisha unamvyompenda na kutaka awe mume wako. Pia mfahamishe hilo la aibu kwa familia yako pindi akiamua hataki tena kukuoa.
Kama bado yuko serious na harusi basi ni lazima nyote wawili muamue muda muafaka wa kufunga pingu za maisha. July au August haitakuwa mbaya. Usisahau kutuletea mrejesho ya yanayojiri kati yenu.

Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
 
Hivi ni kweli wanawake wa kichaga wanatabia za kutazama pesa tu kuliko upendo kwa wenza wao, nakumbuka ninipataga demu mchaga veta sasa marafiki wa chuo wakawa wananiambia nimeangukia, mtoto wa watu nilimuacha kimnya kimnya alihangaika kunitafuta harafu alikuwa na msimamo wa upendo kwangh mpaka leo hii namjutia ,kisa marafiki walonipa mastory ya kijinga kuhusu wachaga[emoji86][emoji86][emoji86][emoji86][emoji86][emoji86][emoji86]
Hawana shida yoyote dada zangu wale..

Tatizo lao ni moja tu, sio wanyonge huwezi kumuonea nae anakua na sauti aka kibass,wanajiamini ukimzungua kesho unamkuta kwao[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
Kumekucha

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
"Kama hu-date na mchaga nyota yako ya mafanikio ni hafifu" Twilumba, 2002
 
Back
Top Bottom