Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Na ndokinachoniumiza hizi vurugu angefanya kabla ya mahari Mimi ningejikataa zangu ila swala la kunilipia mahari ni Kama wamenitia nuksi hata tukiachana kupata mtu nahisi itakuwa shida coz naskia kulipiwa mahari na kuvalishwa Pete ni Kama Agano
Kibiblia hakuna katazo la kuvunja uchumba, sio agano. Agano niko kwenye Unyumba kama mlifanya
 
miss chuga balaa uje uzingue huko mbele,yani makaburi yatafukuliwa na kila mtu,show atasimamia huyo mama mkwe.

Kama utakubali kuolewa na huyo jamaa utahitaji kuwa makini sana sababu hata kama migogoro ikitokea haiwezi kupelekwa kwa wazazi wa mume tena.
 
Dogo langu lilikomaa na kuoa mchaga, tukalikatalia mhehe na mchaga wapi na wapi.?
Akasema Kweli wachaga ni changamoto ila kwa aliyemuoa yeye yupo safi.
Tukaibariki ndoa yao.!
Kila movie lazima ianze na trela, sahiz yupo steji ya trela ila kashaa choka.
Mchaga akiigiza kupenda utasema nipo na Malaika, ila ngojea mzae muwa na vimali kidogo wengi akili zao huwa zinajichaji.
Sio wachaga tu hata wapare..

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
kwa nini mkuu,kama hutojali unaweza kutushikrikisha sababu ya kwa nini hutoweza kufanya hivyo?
mkuu wachagga sisi bhna yaani unavowaona tu hawajui mapenzi yaani ukiwa na mchagga faragha utachukia sana, achana na hizo za faragha lakini hoja yangu ya msingi sisi wachagga tunapendwa na wazazi wetu kama ilivo sawa na jamii za kihindi unavoziona, kwa sisi kuna ile wazazi na ndugu wanachukulia maanani swala la mtoto wao hasa anapopiga hatua (usipopiga hatua kwenye jamii zetu unadharaulika sana, hata salamu hupewi wala wazazi hawatakujali) pia wachagga wakijua una oa wanataka mtu wa maana.
Kuhusu wadada wakichaga wanadharau, hawajui kupenda huwezi kuta mwanamke wa kichagga anakupigia magoti eti salam, au anakusikiliza kwa heshima, ukizuba zuba unaeza hata kupigwa na kudhulumiwa mali. sasa dada zangu jirekebisheni.
 
Mimi sina tatizo lolote na kinachotuchanganya mtoto wake wa kwanza kaoa mtu wa kabila lake tena majirani Ila bado mama mkwe na mawifi wanamfanyia vituko huyo dada sasa nahisi itakuwa ni tabia zao tu kuchukia wakwe na mawifi bila sababu Ila kwangu watakuwa wamechukulia kabila langu tu Kama kivuli Cha kuficha chuki zao

aiseee pole sana
 
mkuu wachagga sisi bhna yaani unavowaona tu hawajui mapenzi yaani ukiwa na mchagga faragha utachukia sana, achana na hizo za faragha lakini hoja yangu ya msingi sisi wachagga tunapendwa na wazazi wetu kama ilivo sawa na jamii za kihindi unavoziona, kwa sisi kuna ile wazazi na ndugu wanachukulia maanani swala la mtoto wao hasa anapopiga hatua (usipopiga hatua kwenye jamii zetu unadharaulika sana, hata salamu hupewi wala wazazi hawatakujali) pia wachagga wakijua una oa wanataka mtu wa maana.
Kuhusu wadada wakichaga wanadharau, hawajui kupenda huwezi kuta mwanamke wa kichagga anakupigia magoti eti salam, au anakusikiliza kwa heshima, ukizuba zuba unaeza hata kupigwa na kudhulumiwa mali. sasa dada zangu jirekebisheni.
ah okay kumbe ndo ilivyo asante kwa kushiriki hili na sisi

na nadhani haya maneno yako yataeleweka zidi kwa sababu yametoka kwa mtu kutoka huko pia
 
Kuna mambo huwa hayalazishwi. Mama na mtoto wana bound ya milele. Mchumba akitenda kinyume na matakwa ya mama ndoa yenu itakua na changamoto nyingi za upumuaji.

Ni afadhali mpate aibu ya kutolewa mahari na kutoolewa kuliko kuishi kwenye ndoa isiyo na amani. Ingekua uko kwenye ligue na mwanamke mwingine ningekishauri usife moyo lakini ligue na mzaa chema ni ngumu sana.
Amani,very important thing in marriage,hata kama mtakuwa na mali na magari mnaweza msione thamani yake kama ndoa yenu haitakuwa na amani...
 
Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
Ukisikia mtihani wa maisha ndio huu sasa
 
hilo haliwezi kutokea kama wewe utamproove wrong mama mkwe wako na huyo mume wako,

lakini ukimfanya mumeo aione ndoa chungu au kufanya mambo yoyote ambayo sio,utamfanya mumeo ajutie kutomtii mama yake sikuzote za maisha yake na utampa mama mkwe nguvu ambayo haijawahi tokea,lakini ukiwaproove walikosea kumzuia kijana wao kukoa,mumeo atatembea kifua mbele na kamwe hatojutia uamuzi wake wa kwenda kinyume na mama yake na mama utamtia aibu ambayo haina mfano wake,na wewe unaweza kuwa chanzo cha kurudisha upatano kati yake na mama yake na hilo litakuwa chachu ya mapenzi yenu sikuzote.
This is best and wisdom comment.!

Inapaswa bint ajitahid japo kubadir asili ni ngumu ajitahid kwa Kweli kufuata ushaur wako mzuri.
 
Siwezi zingua tuna mwaka wa 7 sahivi toka tuanze mahusiani hajawahi kuona kasoro yoyote kwangu ndomana anaumia
miss chuga balaa uje uzingue huko mbele,yani makaburi yatafukuliwa na kila mtu,show atasimamia huyo mama mkwe.

Kama utakubali kuolewa na huyo jamaa utahitaji kuwa makini sana sababu hata kama migogoro ikitokea haiwezi kupelekwa kwa wazazi wa mume tena.
 
Siwezi zingua tuna mwaka wa 7 sahivi toka tuanze mahusiani hajawahi kuona kasoro yoyote kwangu ndomana anaumia
Mmh, huna kasoro kabisa.!
Honger sana bila Shaka wazaz wake pia wanakufahamu vzr zaidi ya miaka 2 au uchumba wenu ulkua wa siri sana.

Kwa miaka zaid ya 6 atakua amekupotezea muda sana na hivyo huna kasoro inatakiwa wazaz wenyw wakukubalie bila tatizo.
 
Hivi ni kweli wanawake wa kichaga wanatabia za kutazama pesa tu kuliko upendo kwa wenza wao, nakumbuka ninipataga demu mchaga veta sasa marafiki wa chuo wakawa wananiambia nimeangukia, mtoto wa watu nilimuacha kimnya kimnya alihangaika kunitafuta harafu alikuwa na msimamo wa upendo kwangh mpaka leo hii namjutia ,kisa marafiki walonipa mastory ya kijinga kuhusu wachaga🙉🙉🙉🙉🙉🙉🙉
Tuliambiwa wamachame wanauwaga waume zao mara baada ya watoto wao kuwa wakubwa.kimsingi inadaiwa ni study imefanyika.inamaanisha Miongoni mwa wajane kundi kubwa ni la wachaga.labda ifanywe study upya itakayo prove wrong hii story."Wachaga husababisha vifo vya waume zao pindi watoto wao wanapokuwa wakubwa".

Personally niliaminishwa hivyo miaka hiyo na ikapelekea nikawaepuke wanawake wa kichaga na wanyiramba ktk harakati zangu za kutafu mke.
 
Kinachoshangaza watu hao ndugu zake hawanijui hata huko mtwara sijawahi kwenda ndomana mtoto wao aliwambia mtu hata hamumjui mnaanza kumchukia na mkikaa nae si itakuwa shughuli, yani nyie acheni tu imefika hatua mama mtu ikipita hata masaa 5 hajapigiwa simu na mwanae utaskia toka uwe na huyo mwanamke umebadilika kitu kidogo ambacho Mimi sihusiki utaskia toka uwe na huyo mwanamke umebadilika me wakati mwingine huwa nacheka tu maana vingine vinachekesha

Back
Top Bottom