2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 3,130
- 4,735
Bas usiwe na shakaSiwezi zingua tuna mwaka wa 7 sahivi toka tuanze mahusiani hajawahi kuona kasoro yoyote kwangu ndomana anaumia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bas usiwe na shakaSiwezi zingua tuna mwaka wa 7 sahivi toka tuanze mahusiani hajawahi kuona kasoro yoyote kwangu ndomana anaumia
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Namuunga mkono mama mkwe.
Habari zenu wapendwa?
Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.
Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10
Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa
Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.
Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,
Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.
Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
How many in-laws (brothers and sisters) do you have and what type of relationship do you have with them? Unawatembelea au unawakaribisha vizuri? Your hubby ni mtoto wa ngapi kwenye familia yao?
DU POLE SANA, WATANZANIA WENGI KWA SASA WANA CHAGAPHOBIA, USILAZIMISHE UNAWEZA UKAPOTEZA MAISHA YAKO KAMA NDUGU HASA BABA NA MAMA MKWE HAWAKUTAKI. KAMA NI WIFE MATERIAL UTAOLEWA TU.
Yuko sahihi..wachaga hamchelewi kuleta mgogoro wa mirathi mkishawaondoa waume zenuHabari zenu wapendwa?
Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.
Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10
Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa
Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.
Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,
Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.
Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
Miss Chuga mdogo angu;
1. Ni wanaume wachache sana ambao wanaweza wakaamua kwenda kinyume na wazazi wao, especially mama zao. Wanawake tukipenda huwa tunaforce kivyovyote huko nyumbani hadi mchumba atakubaliwa, wakibisha sana tunabeba mimba au tunahamia kwa mwanaume bila ndoa, maisha yanasonga. Ila hawa wenzetu, atakaloliamua mama mkwe mara nyingi ndiyo linakuwa final say. Usijiaminishe sana kwamba mchumba wako ana msimamo sana na hautobadilika. Nina rafiki angu Mmachame yalimkuta kama yako, mwisho wa siku mchumba akamwambia mimi siwezi kuendelea na mipango ya ndoa bila wazazi wangu. Ila Mungu sio wakwe, alikuja akaolewa zake na mtu mwingine na yupo anadunda na ndoa yake. (Hopefully wa kwako atapambana hadi mwisho)
2. Kamwe usije ukaungana na mtoto wa mama mkwe kwenda kinyume na mama mkwe; huo utakuwa ni ugomvi wa maisha, na ikiwezekana ugomvi utaendelea hadi kwa watoto wako (ya Hamissa na Mama Diamond). Yes kuna muda wazazi wanazingua, but still tunahitaji baraka zao, hata kama watazitoa kinafki na kuja kujumuika nanyi kwenye sherehe yenu. Usikubali kufunga ndoa na huyo mchumba wako kama wazazi wake hawajaridhia. Yeye anachotakiwa kufanya ni kuwalainisha na kuwaelewesha huko nyumbani kwao hadi waje wakubali. Usishindane na mama mkwe; kesho watapatana na kijana wake ila wewe ndiyo utabaki kuwa adui yake.
Naweza kukuelewa unajisikiaje, aibu unayoiwazia, kuchekwa na kuchambwa na wananzengo, bado muda wako na upendo ulioinvest kwenye hayo mahusiano, labda unaona na umri umeshaenda aisee inaumiza sana. Lakini pamoja na yote hayo, ikitokea imeshindikana kufunga hiyo ndoa; lia mshukuru Mungu kwa yote. Na usije ukakaa unajilaumu sijui ukaharibu maisha yako kisa umeachwa; hujafanya kosa lolote la kukufanya uachike: wewe kuzaliwa mchaga sio kosa wala sio dhambi na huwezi kubadili kabila lako ili kuwaridhisha wakwe. Kuvunjika kwa uchumba sio mwisho wa maisha
Imagine ukiforce hiyo ndoa, utaishi maisha ya aina gani na wakwe zako? Usije ukajidanganya kwamba labda mtaishi mbali na wakwe zako so ni sawa tu; mdogo angu hao ndugu mtawahitaji tu, na watoto wako watawahitaji hao ndugu wa baba zao pia.
Na usijidanganye kubeba mimba, kwa sababu unaweza kubaki single mom, ndoa isifungwe na hata huyo mtoto wako wasiwe na habari naye. Acha mambo yaende naturally, muache mchumba wako apambane hadi kieleweke. Ikishindikana basi mama, wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kuvunja uchumba, na wakati mwingine ni bora kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa. Familia nyingine unaenda kujipa mateso tu.
Muombe Mungu, mapenzi yake yatimizwe kwenye huo uchumba wenu. Litakalotokea lolote, kubaliana nalo then mshukuru Mungu. Yeye anakuwazia mema siku zote, na anaijua kesho yako.
Na nyie wanaume muulizage mapema kwa mama zenu, wawaambie hawataki muoe kabila gani: sio unakaa na mtoto wa mtu miaka 5 afu ndiyo mama mkwe anakuja "sitaki mchaga sijui mnani". Afu alivyokosa huruma eti aliruhusu kabisa utolewe mahari. Mungu amsamehe, hiyo mbegu isije ikamea kwa mabinti zake.
Ukiona linakuchanganya sana, washirikishe ndugu zako. Usije ukadondoka kwa presha bure. Mungu na akutetee
Unaonekana uko vizuri kichwani hivyo wewe msikilize anasemaje lakini pia kumfahamisha unamvyompenda na kutaka awe mume wako. Pia mfahamishe hilo la aibu kwa familia yako pindi akiamua hataki tena kukuoa.
Kama bado yuko serious na harusi basi ni lazima nyote wawili muamue muda muafaka wa kufunga pingu za maisha. July au August haitakuwa mbaya. Usisahau kutuletea mrejesho ya yanayojiri kati yenu.
Bottom line wanasema nini kuonyesha kuwa hawakupendi? Mchoyo, mwizi, muongo etc. Siyo rahisi kumchukia mtu bila sababu. Kwani hubby ameelezwa nini kiasi chakutoa line?
Binti, kikubwa uwe umempenda kweli na ujitoe kuolewa na huyo mmakuwa wako. Mimi nke yangu ni Chagga kama wewe, wazazi wakati naoa hasa mama alikataa akisema ukioa mchagga utaenda kujenga kwao na bla bla. Nikamwambia wangu hayuko hivyo. Nikaoa mchagga wangu na sasa tuna mtoto ni zaidi ya umri wako. Kingine, kwa sasa yeye ndiye kipenzi cha mama ingawa wadogo zangu wameoa kabila letu ila hawamjali kama nke wangu anavyomjali. Kuna siku nilimuuliza kama anakumbuka alivyokuwa anasema, akasema ni maneno ya watu.Habari zenu wapendwa?
Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.
Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10
Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa
Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.
Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,
Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.
Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
Ukoo huo utakiwi, unawaza kupeleka na mtoto asietakiwa, kumpa shida tu mtoto. Muhimu ujione una thamani kwanza kabla yake, kisha maisha yatasongaHabari zenu wapendwa?

Ntaleta mrejesho usijali
Hiyo ni kweli kwa uchagani hata kwenye vitabu vitakatifu Vina depend wazazi hawataweza tena kupokea mahari mara mbili. Ila nahisi kuna Mila itatakiwa kufanyika!Na ndokinachoniumiza hizi vurugu angefanya kabla ya mahari Mimi ningejikataa zangu ila swala la kunilipia mahari ni Kama wamenitia nuksi hata tukiachana kupata mtu nahisi itakuwa shida coz naskia kulipiwa mahari na kuvalishwa Pete ni Kama Agano
Una kibarua Inabidi sasa Umtongoze mamakwe Akukubali . achana nae kwani Wanaume wameisha? Mchagga gani unaolewa mbali hivyo?Kinachoshangaza watu hao ndugu zake hawanijui hata huko mtwara sijawahi kwenda ndomana mtoto wao aliwambia mtu hata hamumjui mnaanza kumchukia na mkikaa nae si itakuwa shughuli, yani nyie acheni tu imefika hatua mama mtu ikipita hata masaa 5 hajapigiwa simu na mwanae utaskia toka uwe na huyo mwanamke umebadilika kitu kidogo ambacho Mimi sihusiki utaskia toka uwe na huyo mwanamke umebadilika me wakati mwingine huwa nacheka tu maana vingine vinachekesha
Mama mkwe tayari amevuka mipaka ameonyesha sura yake halisi licha ya kijana kumvisha Binti pete hataki kujua Aibu ya binti kwa wazazi wake. Mamamkwe ni mtu mwenye Elimu ni Mwalimu. Ni mtu mwelewa ameona amwaribie binti tu sababu zikiwa ni Kabila.Kimeumana.
Ndoa ni ya kwenu wengine wote including mama mkwe ni wapewa taarifa tu. Wazazi, ndugu na jamaa wanaweza kuwashauri ila sio kuwaamulia. Kila kitu kina mipaka including wazazi, in this case mama mkwe kavuka mipaka yake. Kama jamaa ana msimamo, mnapendana na mmetoka mbali sema screw it proceed with the plan.
Unaakili sanaKuna mambo huwa hayalazishwi. Mama na mtoto wana bound ya milele. Mchumba akitenda kinyume na matakwa ya mama ndoa yenu itakua na changamoto nyingi za upumuaji.
Ni afadhali mpate aibu ya kutolewa mahari na kutoolewa kuliko kuishi kwenye ndoa isiyo na amani. Ingekua uko kwenye ligue na mwanamke mwingine ningekishauri usife moyo lakini ligue na mzaa chema ni ngumu sana.
Hiyo ni kweli kwa uchagani hata kwenye vitabu vitakatifu Vina depend wazazi hawataweza tena kupokea mahari mara mbili. Ila nahisi kuna Mila itatakiwa kufanyika!
Kama wazazi wa kijana wameshaanza kuleta Mushkeli na umewashawishi imeshindikana.
Ingia kwenye Maombi umuombe Mungu akuonyeshe kama huyo mume ni wako kweli ama la au ongea Na Baba yako kuna namna flani kule moshi wanafanyaga mila yao huwa wanapanda majani flani ndani ya suku flani yakichipua Basi ni barka kwako
Yasipochipua huyo si wa kwako.
Huyo kijana akikuoa Bila baraka za wazazi wake amini nakuambia hiyo ndoa Itakuwa ngumu sana since day hivi unaendaje kwenye Harusi bila Mama mkwe au Baba mkwe?
Wazazi na ndg watakuona Umemwekea Mtoto wao kitu wewe si MCHAGGA bana!!!
USILAZIMISHE!!