Mama mkwe kamtorosha Mke wangu, nifanye nini niko njia panda

Kuna muda inabidi ujikaze mtoto wa kiume uendelee kupambania kombe, sasa ukiendelea kulalamika na kuleta uzi humu naanza kupata mashaka na wewe. Mwanaume sio wa kulalamika lalamika. Tafuta suluhisho kama ni kupiga chini au kausha hadi waje wenyewe kuomba hela ya matumizi.
 
Ama kwa hakika mkuu nimejifunza mengi sana sitakaa nirudie tena kwasababu mke na mama yake ni kama mtu wanafanana matendo
 
Ndio nafanya maamuzi mkuu lakini kupata mawazo ya watu tofauti tofauti pia ni vizuri kwasababu mimi sio wakwanza kukumbwa na tatizo kama hili
 
Ndio nafanya maamuzi mkuu lakini kupata mawazo ya watu tofauti tofauti pia ni vizuri kwasababu mimi sio wakwanza kukumbwa na tatizo kama hili
Ilishanikuta hii ila ilikuwa tofauti kidogo kwa hiyo kutokana na hilo nashauri usifuate mkumbo wao. Endelea na maisha kama hakuna kilichotokea maana watakuja wao wenyewe tu. Nature ya mwanamke imekaa kukomoa ili muwe sawa kwa hiyo usifuate mkumbo wao kabisa.
 
Nashukuru sana na kinacho endelea itakua ni ivyo ivyo kukomoa ila ngoja nipotee mazima na mimi mpaka atakaporudi yeye mwenyewe
 
Sitaki kuwa mshauri wa mapenzi maana hata mimi ninamaumivu yangu , ila bro kwakifupi wanakufanyia hivyo kwasababu huna pesa
Mkuu pengine unaweza kua sawa ila siwezi jua.
 
Pole bro maumivu ya kuonyeshwa dharau kama hizo ni makubwa sana chamsingi Acha kulazimisha mapenzi pambana na maendeleo yako binafsi kwanza
Hakika icho ndio naenda kufanya kwa sasa.
 
Case kama hii inafanana na jamaa mmoja ila mke na mume walikuwa miji tofauti...bana eeh kumbe jamaa mtoto sio wake...siku anarudi mke amekimbia kwa mama mkwe ...na mama mkwe kamficha...jamaa anasema anachotaka DNA wakamwambia mtoto sio wake..
Hapo mtihani sana.
 
Achana nao endelea na mambo yako.

Muda ni mwamuzi mzuri zaidi.

Mnaumiza vidole vyenu Bure
Mnamshauri
PUNGUANI WAHED
 
Waue
 
Fika police dawati la jinsia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…