Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Usiangalie uchoyo tu.. Wengine tunahitaji uhuru, kama mimi kubanwabanwa nilishashindwa iwe na ndugu zangu au ndugu wa mwenzangu..
Kama kuwasaidia nitawaisaidia huko huko waliko sio lazima waamie kwangu, dada angu alijaribu kuleta upuuzi wa kuhamia kwangu.. Kilichomkuta hakuamini mpaka saizi heshima ipo!!
Dunia inaenda kasi mnooo... kuna watu ni wachoyo sana
 
Kwahiyo if ikitokea bahati mbaya kaka/mdogo wako wa kiume afariki halafu ameacha watoto.... watoto wake hauwezi kuwa chukua na kuishi nao kama wanao ??
 
ulimfanyaje??
 
Kwangu mamamkwe na vijana wake wa kiume wamehamia kabisa kwangu, hawana matatizo yoyote yani mama mkwe ndiye kawa sterling anafanya maamuzi kwangu, mashemeji zangu wako kwangu wanaishi na kusoma, baba mkwe naye huja mara kwa mara.

Hii siyo uongo wala chai, yani wamehama kwao mkaoni wamehamia Dar kwangu.

Sasa hawataki ndugu yangu yeyote kwangu, siyo kukaa hata kupita kusalimia hawataki. Na wanafanya wazi wazi kabisa, sielewi hata nifanyeje?

Sina maelewano na ndugu zangu kwasababu nilitaka kumridhisha mke wangu, kwa kuruhusu familia yake kuhamia kwangu.
 
[emoji3][emoji3][emoji3],lazima watoke nduki
kama unataka m Tanzania hakimbie kwako usiwe unapika chakula na kama unataka nyumba yako wageni wajazane tu kuwe kuna uwakika wakupatakikana vyakula vyakutosha watoto wa mjomba, shangaz, baba mkubwa, wajomba zako watakuwa wanakuja kila shule zikifungwa
 
Watoto/mwanafunzi mi kwangu sio tatizo, tatizo ni mtu mzima tena mwenye uwezo wa kufanya kazi eti ahamie kwangu, hilo halipo aisee!
Kwahiyo if ikitokea bahati mbaya kaka/mdogo wako wa kiume afariki halafu ameacha watoto.... watoto wake hauwezi kuwa chukua na kuishi nao kama wanao ??
 
Tatizo tuna watoto na mke wangu, sasa imekuwa taabu kweli kweli.
Ningeweza ku rewind maisha kwa ninayoysona, nisinge muoa huyu mwanamke niliyenaye yani nashindwa nifanyeje.
 
Nanye Go, Hilo swala lakushindaje?
Ila nashukuru kuoa wa mwisho kwao.
Nashukuru wakwe walikuwa wanafanya mishe zao hadi leo wanafanya mishe zao.
 
Huyo mama angekuwa ni mama yako mzazi na huyo shemejio angekuwa ndugu yako ungesema yote hayo??
 
dawa ni kuwapa ugali na maharage mabovu kila siku lazima watoke nduki
 
jamaa wewe ni mjinga
 
Nimekuelewa sana, nafanyia kazi huu ushauri
Halafu kumbuka pia kuwa hawa watu huwa hawachaguliwi sehemu ya kwenda kuishi, huwa wanachagua wao wenyewe! Kwa hiyo kama amepachagua hapo nyumbani kwako, tafadhali sana usimubugudhi. Lakini pia kwa upande mwingine kuna mbaraka wa pekee sana unaoambatana na uchaguzi huo iwapo alikuwa na options kadhaa, na akaamua kuja kwako na si kwa hao wengine. Kuna mbaraka wa pekee kwenye uchaguzi huo kwenu mliochaguliwa!
 
Mkuu bila huyo mama usinge pata kipozeo tena mjali Sana mama kuliko huyo mkeo.
 
Nanye Go, Hilo swala lakushindaje?
Ila nashukuru kuoa wa mwisho kwao.
Nashukuru wakwe walikuwa wanafanya mishe zao hadi leo wanafanya mishe zao.
Unawafanyaje, kuwafukuza siwezi na kwangu kumekuwa kwao, ndugu zangu kwangu hawatii mguu, wao hivyo ndio wanataka lakini kwangu imekuwa ngumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…