Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Jamani Africa tunakwama wapi? Umeona binti umempenda umeulizia bei gani (mahari) umelipa ili uachane nao kiroho safi! Kumbe ndo unaenda kubeba ukoo na utitiri wa ndugu kisa unaishi nyumba kubwa either umepanga au umejenga. Ungekuwa na chumba kimoja au chumba na sebure wangekuja? Africa! Tunakwama wapi?
Chumba na sebule wanakuja mkuu utajua wewe watalalaje
 
Je huyo mke wako hana wadogo zake wa kiume au wakike wanaojitegemea? Hahaha daah jamaa yangu wewe una roho mbaya aisee
Mimi sioni kama ana roho mbaya, mama anaishi Kwa mtoto wa kiume na hilo wengi hawalijui, mtoto wa kike muolewaji tu anakwenda kusalimia na kurudi labda kama kuna sababu maalum ya kukaa pale, huyu kijana kwenda kukaa Kwa dada aliyeolewa nyio mnaona sawa? Labda kuwe na sababu ambayo itamfanya muoaji katoa wazo la huyo shemeji aje kukaa hapo, yupo sahihi
 
Dunia inaenda kasi mnooo... kuna watu ni wachoyo sana
 
Haahhaha hahahaha ..hold my beer please
mr.London, Kwa mama mkwe wa hivyo hamtamaliza hata miaka miwili mbele lazima wewe na mkeo muachane!
Tofauti na hapo wakupige limbwata uwe bwege then familia nzima wahamie hapo halafu wakubandike na kajina ka utani "kijeba" ni full kukusema kutwa nzima ukiwa job na kukuigiza unavyotembea na kuongea[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Pole sana vumilia tu bila ivyo utaonekana mchoyo na una roho mbaya
 
Hahaah
Hii haijalishi ni ndugu wa nani wanazungumziwa hapa, tatizo ni USWAHILI. Unaongea kwa uchungu kwa kuwa hata sasa unaishi kwa shemeji yako eeh? Toka hapo mama nenda kwako, utaharibu ndoa ya dadaako. Tujifunze pia kuzaa kwa mpango
 
Hahaahaha
Ukiwa unadate na binti wa kukuletea utitiri wa ndugu utamjua tu mwanzoni. Unamtoa out au mko kwenye maongezi yenu mara simu inalia anaongea anaanza kukutambulisha na kukupa simu sijui msalimie anti/uncle/mama/Dada/kaka/ mdogo wangu, n.k. ukioona hivyo ni dalili tosha huyo manzi chaka!
 
Dawa ni kupiga show ya ukweli, mpaka mkeo awe anatukana ukoo mzima kwa sauti akiwa hajitambui ndo watahama.
 
No retreat no surrender, Wanakuja tu dar familia ngapi zinaishi chumba na sebule na ndugu karibia watu8 humohumo na maisha yanaenda?!

Tuache utani wangekua ndugu wake yeye mwanaume angelalamika?!
Mkuu kuna familia na familia Sisi kwetu utatimuliwa tu hakuna kukaa Kwa Kaka wala Kwa dada, hivyo vikao na simu kutoka Kwa ndugu, utaondoka bila kuaga, mwenye kukuuliza utaondoka lini huko, mwingine atakwambia kabisa ondoka mwache mwenzio aishi Maisha yake usimpe karaha, mkuu humalizi mwezi utaondoka tu tena bila kinyongo
 
Sisi tusio na mihemko ya kuoa Tuna wachora tu

Yaani haiwezekani kisa papuchi ni muweke Mtu ndani kisha nianze kumuhudumia kila kitu nikikosa kutimiza majukumu yangu nianze kupatwa na stress almanusura kupata nusu uchizi ...Huo ujinga,siwezi kuu'apply katika maisha yangu(mtani samehe)

Kuoa ni kujipa majukumu yasiyo na ulazima na ni kujitakia Kufa mapema (lol)
 
Namshukuru Mungu nilioa wa mwisho, wengine wote wameoa na kuolewa afu wote mkoa mmoja na wilaya 1. Familia yangu nayo wilaya 1.
Hakuna anayekuja kulala au kuishi kwangu au kwa mwenzake
 
Ngoja sasa mzee baba nikufundishe ghubu la kibaharia. Ukirudi tu job, mrushie mamkwe kashkamoo ka juu kwa juu, mkung'ute wife bonge la busu halafu mburuzie chumbani...fanya ule mchezo wetu kwa muda mrefu kiasi ukimuachia anaona haya kutazamana na huyo kaka yake usoni.

Siku ukishinda home fanya mchana kutwa. Baada ya wiki 3 njoo utupe mrejesho.
 
Shida za kuoa Kilimanjaro halafu wewe uaishi pale moshi mjini,nauli mtu haizidi hata 5000

Mtu anaoa Dar halafu anaenda kuishi mbezi beach oooh hooo kila sku ndugu hawakauki tena

watakuja kila week end kukusalimieni tu,Dawa ya Ndoa Unaoa Dar unaenda ishi Kigoma huko

Unaoa Bukoba unaleta kambi Dar,yani mtu akifikiria kuja kwanza lazima apige simu kutoa taarifa

sio mambo ya kuoa Sakina halfu unaenda kuishi ngaramtoni huo ndo uzwazwa maji...
Hahahahaaa my foot
 
Kweli mifano ni mingi

Haujaona tu unakuta mtu ana appartment kapanga ila ndo hvyo ndugu na watu baki kama wote na sababu wanafahamiana na mwanaume
Iliwahi kumtokea bro wangu. Wamekaa mara bi mkubwa huyo na watu kama watatu hivi. Ukiangalia nyumba vyumba vitatu. Jamaa ana mke na watoto 3, na mfanya kazi na wadogo za mke we 2.

Siku natinga pale nikakutana na bonge la timu. Nikamuuliza jamaa kulikoni. Akaniambi mambo ya bi mkubwa. Nikamuuliza mnaishi je humu ndani. Akaniambia kuna wengine kawalipia guest na haijulikani wanaondoka lini. Pesa nilikuwa sio ishu; ishu ilikuwa ni Uhuru.

Nilichokifanya nilimkalisha bi mkubwa chemba nikamuuliza hawa ni akina nani mbona siwafahamu? Majibu aliyonipa hata undugu hatuna; nikampa makavu laivu. Nikamwambia awambie wajiandae warudi kijijini.

Walivyoondoka jamaa alinishukuru sana maana yeye alishindwa kusema.
 
Mkuu huna mashamba, tafuta mashamba wakifika tu hata kama mvua hamna unawapeleka kulima mchincha wa kumwagilia yani kazi kazi hakuna maisha ya kukaa unatizama seaaon uone kama watakuwa wanakuja
 
Back
Top Bottom