Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imeisha hiyo.Kama mtu huwezi kuheshimu mipaka yako. Nani atakuheshimu?
Tatizo lipo kwa Mtoa mada na sio huyo Mama mkwe.
Vile unavyojiweka ndivyo Watu wanavyokuchukulia
Kwanza katudanganya, huyu jamaa anaishi ukweni.Aisee we ni bonge la kiazi.
Mm wake zangu mpaka wananipigia wao,maana siwezi kuwapigia simu mara kwa mara yote kuepuka hayaAisee! Wewe jamaa bhana utakuwa umelogwa wewe siyo bure..
1. Mama mkwe anatakiwa aje kwako mara moja kwa mwaka.
2. Mama mkwe unatakiwa uwasiliane kwenye simu mara moja tu tena pale kunapo tokea tatizo kubwa linalo hitaji mkusanyiko wa watu weng na baada ya hapa unasepa..
Wewe jamaa unaendekeza ujinga sana
Hakuna dawa nyingine zaidi ya Kumpelekea Moto!
Inaonekana jamaa alipata jiko akiwa mdogo sana yaani anaendeshwa hovyo sana au Itakuwa amewekwa kwenye chupa😂😁Aisee
mkwe mkwee....anataka dyudyu"Akina mama wa Kidamba yaani Wandamba wa Malinyi Morogoro hii ni asili yenu au huyu mama mkwe wangu ana lake jambo.
Iko hivi nimeoa kwa ndoa sasa mwaka wa pili ndani mke wangu tunaheshimiana sana changamoto ni mama mkwe akija nyumbani kusalimia hakuna kazi atafanya ikitokea Binti yake anaumwa basi nitafanya Mimi kazi za ndani mama anaangalia tu lakini pia sisi tukitoka nyumbani kwetu nilishatoa maelekezo Kwa mke wangu haijalishi nyumbani amebaki nani lazima chumba tunacholala na mke wangu kifungwe na funguo tuwe nazo sisi wenyewe
lakini ajabu siku moja mama mkwe alihoji kwa Nini mnafunga chumba chenu wakati Mimi nipo? Hatukumjibu Siku za hivi karibuni nilienda Malinyi kwani shughuli zangu za kilimo ni huko tulishajenga kibanda cha kufikia lakini kwa vile sisi tunaishi mkoa mwingine pale tulimwacha mama mkwe akae.
Akiwa anafahamu kabisa kwamba nipo safarini naenda Malinyi huyu mama katika chumba chetu alileta mwanaume maana yeye hajaolewa nilifika usiku kwa changamoto za usafiri pale nakuta anajivinjari nililazimika kulala Lodge asubuhi mapema niliamkia pale nyumbani nikabadili nguo nivae za kwendea shamba bado nikamkuta hawara yake yupo.
Kwa tamaduni za kwetu sikuingia ndani alitumwa mtoto akaniletea nguo nikabadilishia bafuni nikaenda shamba.Hilo likapita wakati naandaa shamba yeye alisema kijana wake ambae ni shemeji yangu ana ng'ombe hivyo nisitafute ng'ombe wa kulimia kwingine basi nikalipa pesa kabisa kuwahi nafasi ili msimu ukianza waanze kunilimia Mimi
lakini tarehe za kulima zilipofika wakagoma kulima shamba langu nikamuuliza shemeji kwa nini wakati nilishalipa pesa mapema nikajibiwa mama mkwe amezuia kulimiwa Mimi hadi wamalize mashamba yao.
Naunganisha dot naona kama huyu mama mkwe heshima ninayompa hailingani na anayonilipa nasisitiza binti yake hana tabia hizi naomba kujua nifanye nini au huyu mama kusudio lake nini kwenye ndoa yetu na zaidi ni mbinafsi hata tumpe msaada kiasi gani haonyeshi kurizika ni lawama tu amefikia hatua ya kusema mwanaume anaemuoa Binti yake ikiwa hatoelewana na yeye mama mkwe basi hatodumu na Binti yake.
Mimi nilikuwa nikisikia huyu mama ana uhitaji wowote nitapambana kumtimizia lakini kwa hizi tabia na matendo na kauli zake nafika hatua natamani kuamua niishi kwa kutoelewana nae ili niweke mipaka ya kutozoeana kwa Afya ya ndoa yangu. Naomba maoni na ushauri wa wadau tafadhali"
Jamaa mama mkwe kamuweka kwenye chupa 😂 inafaa mwamba aondoke maeneo hayoCharles kilian uje umpe ushauri huyu mtu
🙏🏽Na Mwenye sikio asikieJamaa mama mkwe kamuweka kwenye chupa 😂 inafaa mwamba aondoke maeneo hayo