Mama Mkwe wangu ananivunjia heshima

Mama Mkwe wangu ananivunjia heshima

mtafute mhaya jirani akutafsirie hii....OBWIGUSI BWEMANA NYOKOZALA OMWETA MAE!
Alaf lifanyie kazi!
 
Aisee! Wewe jamaa bhana utakuwa umelogwa wewe siyo bure..
1. Mama mkwe anatakiwa aje kwako mara moja kwa mwaka.

2. Mama mkwe unatakiwa uwasiliane kwenye simu mara moja tu tena pale kunapo tokea tatizo kubwa linalo hitaji mkusanyiko wa watu weng na baada ya hapa unasepa..

Wewe jamaa unaendekeza ujinga sana
Mm wake zangu mpaka wananipigia wao,maana siwezi kuwapigia simu mara kwa mara yote kuepuka haya
 
Tatizo la kuokoteza wanawake hovyo
Zamani wazazi wetu ndio walikuwa wanaridhia au kutuma watu kuwajua wakwe
Siku hizi mnabeba mpaka watoto wa wazinzi
Sasa wewe endelea tu hapo wife anaficha yake au nae anafanya kama mama
Like mother like daughter
Hapo hakuna kitu
Ukikaa vibaya anakupa
 
"Akina mama wa Kidamba yaani Wandamba wa Malinyi Morogoro hii ni asili yenu au huyu mama mkwe wangu ana lake jambo.

Iko hivi nimeoa kwa ndoa sasa mwaka wa pili ndani mke wangu tunaheshimiana sana changamoto ni mama mkwe akija nyumbani kusalimia hakuna kazi atafanya ikitokea Binti yake anaumwa basi nitafanya Mimi kazi za ndani mama anaangalia tu lakini pia sisi tukitoka nyumbani kwetu nilishatoa maelekezo Kwa mke wangu haijalishi nyumbani amebaki nani lazima chumba tunacholala na mke wangu kifungwe na funguo tuwe nazo sisi wenyewe

lakini ajabu siku moja mama mkwe alihoji kwa Nini mnafunga chumba chenu wakati Mimi nipo? Hatukumjibu Siku za hivi karibuni nilienda Malinyi kwani shughuli zangu za kilimo ni huko tulishajenga kibanda cha kufikia lakini kwa vile sisi tunaishi mkoa mwingine pale tulimwacha mama mkwe akae.

Akiwa anafahamu kabisa kwamba nipo safarini naenda Malinyi huyu mama katika chumba chetu alileta mwanaume maana yeye hajaolewa nilifika usiku kwa changamoto za usafiri pale nakuta anajivinjari nililazimika kulala Lodge asubuhi mapema niliamkia pale nyumbani nikabadili nguo nivae za kwendea shamba bado nikamkuta hawara yake yupo.

Kwa tamaduni za kwetu sikuingia ndani alitumwa mtoto akaniletea nguo nikabadilishia bafuni nikaenda shamba.Hilo likapita wakati naandaa shamba yeye alisema kijana wake ambae ni shemeji yangu ana ng'ombe hivyo nisitafute ng'ombe wa kulimia kwingine basi nikalipa pesa kabisa kuwahi nafasi ili msimu ukianza waanze kunilimia Mimi

lakini tarehe za kulima zilipofika wakagoma kulima shamba langu nikamuuliza shemeji kwa nini wakati nilishalipa pesa mapema nikajibiwa mama mkwe amezuia kulimiwa Mimi hadi wamalize mashamba yao.

Naunganisha dot naona kama huyu mama mkwe heshima ninayompa hailingani na anayonilipa nasisitiza binti yake hana tabia hizi naomba kujua nifanye nini au huyu mama kusudio lake nini kwenye ndoa yetu na zaidi ni mbinafsi hata tumpe msaada kiasi gani haonyeshi kurizika ni lawama tu amefikia hatua ya kusema mwanaume anaemuoa Binti yake ikiwa hatoelewana na yeye mama mkwe basi hatodumu na Binti yake.

Mimi nilikuwa nikisikia huyu mama ana uhitaji wowote nitapambana kumtimizia lakini kwa hizi tabia na matendo na kauli zake nafika hatua natamani kuamua niishi kwa kutoelewana nae ili niweke mipaka ya kutozoeana kwa Afya ya ndoa yangu. Naomba maoni na ushauri wa wadau tafadhali"
mkwe mkwee....anataka dyudyu
 
Ipo siku watakufukuza hapo kwako. Na kabla hujafukuzwa mkeo atagongwa na mchepuko wake hapohapo kwako. Wewe huheshimiwi na familia nzima ya ukweni kwako akiwemo mkeo. NIMEKEREKA SANA. Watu tuna masikitiko ya mlinzi wa maiti kutaka kuua mtu ili asimdhuru maiti halafu wewe unakuja na huu ushuzi!! 😡😡😡
 
Back
Top Bottom