Mama Mkwe wangu ananivunjia heshima

Mama Mkwe wangu ananivunjia heshima

Wewe ni Mjinga na unaonekana hujakamilika kama Mwanaume kamili yaani Mama Mkwe analeta mwanaume wake kwenye kitanda unacholala na Mkeo unahisi kwa nini kafanya hivi?sababu kubwa jitathmini kama ni mwanaume kamili au lah Asante
Sasa kosa Lake ni lipi mkuu?
 
Shukuru kama binti yake hana tabia kama za mama yake.
Muwekeeni mipaka TU na kumvumilia
 
Ujinga ni kuwekeza ukweni,ndio maana una dharaulika,!,mama na mwanaye wamekutawala akili
 
Mama mkwe si ndugu yako, na ndoa ni ya watu wawili, wewe kama kiongozi umeruhusu mtu wa tatu lazima shida itokee. Rudi kwenye nafasi yako fanya maamuzi.
 
kwetu mwiko kabisa mama mkwe kuja kukaa kwangu na mwanae....kwa mantiki hiyo ntakushauri fukuza kabisa hiyo kitu hapo, fukuzaaa iende kwake na mtoto wake akileta maneno fukuza,
 
Wewe ni Mjinga na unaonekana hujakamilika kama Mwanaume kamili yaani Mama Mkwe analeta mwanaume wake kwenye kitanda unacholala na Mkeo unahisi kwa nini kafanya hivi?sababu kubwa jitathmini kama ni mwanaume kamili au lah Asante
Hapa ilibidi jamaa aunge tera wamgonge huyo maza mtungo na huyo bwana ake. Upumbavu sipendagi
 
Huyo mama ni Mndamba mwenzangu.
Nipe namba yake nimkanye kwa kindamba atanielewa tu.

Nitamwambia kama amekosa heshima basi atulize K yake.
Mm ni Mndamba wa Kipingo na ni mstaafu.
Pole sana kijana kupata mama mkwe msela mavi.
 
"Akina mama wa Kidamba yaani Wandamba wa Malinyi Morogoro hii ni asili yenu au huyu mama mkwe wangu ana lake jambo.

Iko hivi nimeoa kwa ndoa sasa mwaka wa pili ndani mke wangu tunaheshimiana sana changamoto ni mama mkwe akija nyumbani kusalimia hakuna kazi atafanya ikitokea Binti yake anaumwa basi nitafanya Mimi kazi za ndani mama anaangalia tu lakini pia sisi tukitoka nyumbani kwetu nilishatoa maelekezo Kwa mke wangu haijalishi nyumbani amebaki nani lazima chumba tunacholala na mke wangu kifungwe na funguo tuwe nazo sisi wenyewe

lakini ajabu siku moja mama mkwe alihoji kwa Nini mnafunga chumba chenu wakati Mimi nipo? Hatukumjibu Siku za hivi karibuni nilienda Malinyi kwani shughuli zangu za kilimo ni huko tulishajenga kibanda cha kufikia lakini kwa vile sisi tunaishi mkoa mwingine pale tulimwacha mama mkwe akae.

Akiwa anafahamu kabisa kwamba nipo safarini naenda Malinyi huyu mama katika chumba chetu alileta mwanaume maana yeye hajaolewa nilifika usiku kwa changamoto za usafiri pale nakuta anajivinjari nililazimika kulala Lodge asubuhi mapema niliamkia pale nyumbani nikabadili nguo nivae za kwendea shamba bado nikamkuta hawara yake yupo.

Kwa tamaduni za kwetu sikuingia ndani alitumwa mtoto akaniletea nguo nikabadilishia bafuni nikaenda shamba.Hilo likapita wakati naandaa shamba yeye alisema kijana wake ambae ni shemeji yangu ana ng'ombe hivyo nisitafute ng'ombe wa kulimia kwingine basi nikalipa pesa kabisa kuwahi nafasi ili msimu ukianza waanze kunilimia Mimi

lakini tarehe za kulima zilipofika wakagoma kulima shamba langu nikamuuliza shemeji kwa nini wakati nilishalipa pesa mapema nikajibiwa mama mkwe amezuia kulimiwa Mimi hadi wamalize mashamba yao.

Naunganisha dot naona kama huyu mama mkwe heshima ninayompa hailingani na anayonilipa nasisitiza binti yake hana tabia hizi naomba kujua nifanye nini au huyu mama kusudio lake nini kwenye ndoa yetu na zaidi ni mbinafsi hata tumpe msaada kiasi gani haonyeshi kurizika ni lawama tu amefikia hatua ya kusema mwanaume anaemuoa Binti yake ikiwa hatoelewana na yeye mama mkwe basi hatodumu na Binti yake.

Mimi nilikuwa nikisikia huyu mama ana uhitaji wowote nitapambana kumtimizia lakini kwa hizi tabia na matendo na kauli zake nafika hatua natamani kuamua niishi kwa kutoelewana nae ili niweke mipaka ya kutozoeana kwa Afya ya ndoa yangu. Naomba maoni na ushauri wa wadau tafadhali"
Wewe jamaa!!

Kwanini usingechukua fimbo ukaingia ndani na kumtimua huyo mama na hawara yake!!?

Hasta polisi na ustawi was jamii wangekusaidia kesi!

Hao unapiga fimbo za kichwani wanatoa damu halafu unawaambia sitaki kuwaona tena!!!

POLE SANA KWA USTAARABU ULIOZIDI,NDUGU WA UKWENI HUWA NI MSALABA!

NILIWAHI MTIMUA SHEMEJI WA KIKE KISA ALILALA NJE JAPO BABA MKWE ALITETEA NILIGOMA AKAMALIZIA SHULE HOSTEL HUKO!!

KILA MWANAMME ANA A POINT OF NO RETURN!!

NENDA KAMTIMUE NA MKEWE AKILETA KELELE TIMUA!!
 
Dhambi, Mungu hapendi
 
Tuma picha ya mama mkwe wako kwanza tuonane tatzo lipo wapi
IMG-20240215-WA0037.jpg
 
Hapa ndo penye tatizo la ndoa yako ,usithubutu kuoa familia ambayo mwanmke kalelewa na mama tu, unless iwe aliolewa huyo mama na kwa bahati mbaya akafiwa mume, Ila kama mama mkwe wako ameishi maisha ya kisimbe tangu mwanzo au alivunja mji na kuanza kuishi peke yake hakika umeumia, una muda mchache sana wa kuishi na huyo mkeo.

NOTE: huu ni mtazamo wangu yawezekana isiwe hivyo ninavyoamini mimi
Ndio ukweli wenyewe sasa mkuu yani mwanaume ukioa mwanamke ambaye amelelewa na Mama pekee hapo jua huna mke lazima itafika wakati atakua kama Mama yake tu
 
Wewe ni Mjinga na unaonekana hujakamilika kama Mwanaume kamili yaani Mama Mkwe analeta mwanaume wake kwenye kitanda unacholala na Mkeo unahisi kwa nini kafanya hivi?sababu kubwa jitathmini kama ni mwanaume kamili au lah Asante
Hapana, ulitakiwa umshauri kama alivyoomba.

Muoneshe njia afanye nini 'kumalizana' na tabia chafu ya mamkwe wake?

Kuishia kusema ajitathimini kama ni mwanaume kamili bila kumshauri cha kufanya, ni matusi umemtukana.
 
Back
Top Bottom