Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!



fundi....

hebu badilisha text hizo unatuumiza macho yakhe,au mpaka BOSI wangu ajue kuwa nasoma JF?
 
Samahani najaribu kuondoa bold bila mafanikio. Hivi text gani ndiyo inayofaa? Mimi bado mwanafunzi.
 
Naipitia hii thread mara kadhaa lkn nakosa la kusema/kuandika, maana sikumfikiria kabisa huyu mama kufanya km alivyofanya! Kweli viongozi wetu wengi walio ktk system ni mafisadi; ni vigumu kumpata kiongozi safi kutoka ktk wale walio ktk system kwani mbinu zote za 'kula' wanazo; wanazi-update tu.
 
Watu wa CCM mnataka kuleta Ubalali hadi kwenye nyumba za watu!!Ingekuwa Tanzania hapa tungeambiwa ni mjanja na hao ndugu wana Qualifications.Mimi huwa sina huruma na watu wa namna hii kama kweli amefanya hivyo wacha lungu na aibu zimshukie.Kama ni kujinyonga wacha afanye hivyo si itakuwa ni hiari yake.Kwani kibaya ni kipi tendo la kuiba au watu kukusema kutokana na tendo ulilofanya.

Hii ndo image halisi ya viongozi wa Tanzania
 
Wote wachangiaji mko sahihi. Viongozi wetu ni reflection yetu. Lakini as we move forward, information is power. Haya yote tumeyajua kwa sababu tuna wigo wa kuyajua, asikudanganye mtu jamii yenye kupata habari ni tofauti na jamii inayosikiliza redio tanzania tuu. Jiulize watanzania wangapi watayajua haya? ila kwa sababu ya email na sms hii habari itaenea, kitu ambacho viongozi wetu wasingependa.

Sina la zaidi ila kwa kweli JF idumu, inatuhabarisha mengi ya manufaa kwetu wenyewe na taifa letu.
 
Kunahaja ya kuanzisha "Tanzania Parents Day" tuwatunuku wazazi na walezi bora. Yaani katika watoto 5, 2 maprofesa, 2 shahada za juu! kazezeta ndo kana BA! FMES tuambie wanao zimo? au ndo wanao tumwagia pombe baa!
 

Ni kwamba magugu yamekuwa mengi kuliko ngano, sasa tunashindwa kutofautisha, tunayavuna yote na kuyatia ghalani. Tunalia njaa wakti ghala limejaa, kumbe tumejaza magugu tu! Tulikuwa wapi msimu wa palizi?

Tunaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!

Enyi wana JF, je mko kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura? Na ninyi na nyumba zenu huwa mnamchagua nani wakati wa kura, na kwa nini? Pengine ufisadi unaanzia kwenye familia zetu, hebu tujitafiti vema!
 

Mtanzania:

Kuna mtu anaitwa Oscar Kambona ambaye alitembea mikoani kutafuta wanachama 10,000 wapya wa TANU na kupewa hela za kufungua akaunti ya kwanza ya chama, kwanini akuchukua hizo pesa na kuweka kwenye akaunti yake?

Kuna mtu anaitwa Azizi, alitumia gari lake binafsi na kuwa dereva wa kumtembeza Nyerere sehemu zote Tanganyika kupiga kampeni. Baada ya uhuru, huyu jamaa alirudi kwao Chalinze na hakumuomba Nyerere kitu chochote.

Mifano hiko chungu mzima ya kuonyesha kuwa waliopigania uhuru na waliojua umuhimu wa sisi kupata uhuru hawakuwa na tabia ambazo ni reflection ya viongozi wa Tanzania wa sasa.

Baada ya uhuru makosa yalifanyika. Watu walimaliza shule na kupewa nafasi bila kuwa na uzoefu au maadili yoyote ya kazi (ethics). Na hawa ndio wanaoi-cost nchi sasa hivi.
 
Quote:-

"FMES tuambie wanao zimo? au ndo wanao tumwagia pombe baa!"

Mkuu heshima mbele, nilisema kuwa nimenawa mikono na hiyo ishu, lakini ni mwiko kwangu kukimbia maswali mapya kama hili lako, kwa hiyo mkuu nina watoto wawili, mmoja wa kiume miaka 11 ni mcheza Cinema za cartoon za Dora The Explorer na Sesame Street, wa kike ana miaka 7 yeye ni Champion wa Spelling Bee, Kwa hiyo mkuu, wanaoawamwagia bia kwenye mabaa sio wa kwangu,

Ahsante Mkuu, ila please lets stick na the real ishu muhimu kwa taifa letu hapa, yaani uozo wa viongozi wetu kina Mama Mongella, mambo yangu personal nitafute kwenye PM nitakufahamisha zaidi ili na wewe ununue hizo DVD za Cinema za mtoto wetu mkuu na wewe uonyeshe watoto wako waone mbongo mwenzao anvyowakilisha taifa lake mkuu!

Otherwise, moja ya DVD alizocheza kijana wetu inaitwa "Dora The Explorer..Nick JR..World Adventure" Imetengenezwa na Viacom Company, ukiuliza kwenye maduka makubwa ya Video & DVD, kama Time Warner, Toys "R" Us, Circuit City, Best Buy, au The Whiz, utaipata tu.

Ahsante Mkuu!
 
Kwa kusema kweli sijui, lakini nitajitahidi kujifunza ili niweze kumudu hii teknolojia ya kisasa maana si mtu mmoja tu aliyelalamikia maandishi yangu. Kwa sasa naona tuwaachie wenye mada waendelee nayo.
 
Mimi simjui Mama Mongela lakini naamini tusimhukumu kabla hatujajua story yote. Kunyamaza kwake sio lazima kumaanisha ni kuzikubali tuhuma hizo. Bahati mbaya wengi wetu tunayo tabia yakuwatakia wenzetu mabaya. Wachache wapo tayari kumuonea huruma na kusubiri ukweli. Kinachosikiitisha zaidi ni kutumia tuhuma hizi kuwatuhumu sio tu viongozi wetu wote bali hata Watanzania wote kama wezi. Mimi nadhani tutumie muda mwingi kujijenga na kujengana badala ya kushabikia kwa furaha mwenzetu anapoanguka. Pole Mama Mongela.
 
Kunyamaza ni kukubali, kama ana side yake ya story itolewe.
 

Mtu mwizi!

Tusipoteze mda kujengana na kuoneana huruma ya nini?

Haya ndo mambo yanaturudisha nyuma kila siku!

Ingekuwa ni China- sasa Mongela tungeongelea tu mengine!

Tusiwavumilie wezi- tuwaogope kama ukoma!
 
Waliosema "innocent until proven guilty" walijua kwamba one cannot be fairly tried in the court of public opinion! Half truths half lies!! Tuvute subira na ukweli utakapobainika tutayajadili na kutoa hukumu. Is this too difficult to ask this?
 
Kunyamaza ni kukubali, kama ana side yake ya story itolewe.
Waliosema "innocent until proven guilty" walijua kwamba one cannot be fairly tried in the court of public opinion! Half truths half lies!! Tuvute subira na ukweli utakapobainika tutayajadili na kutoa hukumu. Is this too difficult to ask for?
 
Sasa wewe unayetaka fair trial defense yake iko wapi? The public is entitled to know and if her strategy is mum, then she probably has much to be mum about.
 
Quote

"Mimi simjui Mama Mongela lakini naamini tusimhukumu kabla hatujajua story yote. Kunyamaza kwake sio lazima kumaanisha ni kuzikubali tuhuma hizo."

Mama aliyekuwa mstari wa mbele kuwaamsha kina mama na Beijing, aliyekuwa very vocal kuhusu kutaka kuwa rais wa kwanza mwanamke, na ambaye majuzi tu alimshitaki Waziri Chenge, mbele ya wananchi na Waziri Mkuu, unasema inapokuja uozo wake tena kwenye taasisi ya kimataifa kuwe na subira?

Yeye hiyo subira hakuiona kwa Waziri Chenge na kumuabisha kiongozi mwenziwe mbele ya umma? Sasa vipi na media yetu ambayo kwa mujibu wa sheria ndiyo inatakiwa kuripoti na ndiyo iliyoripoti hii habari, nayo vipi kazi yake ni kufurahia kuanguka kwa kiongozi?

Tabia ya kuwaomba viongozi wetu wabovu waanguke, unasema ni tabia mbaya? So be it! Mkuu mimi nimesema toka tukiwa BCS, na hapa JF kwamba tatizo namba moja la nchi yetu ni viongozi wezi na wasiokuwa na vision, once hilo likitatuliwa basi mengine yote yatajipanga yenyewe, mkuu kuanzia IPTL, Radar, Buzwagi mpaka Richmond wewe bado mpaka leo unasubiri story ya upande wa pili? Hivi unajua kuwa tunalipia Mamillioni ya dola kila mwezi kwa ajili ya umeme ambao hatuna, na mpaka leo bado waliohusika ni "innocent until proven guilty?" Unafikiri ni lini watakuwa proven guilty? Wapi? na Where?

Unasema furaha ya mwenzetu anapoanguka? Je siku ile mble eya Waziri Mkuu, kule Ukerewe Mama Mongella alipokuwa anamshitaki Waziri Chenge, angefukuzwa kazi Mama Mongella angelia? Kwa kumchongea Waziri Chenge, kwa mkubwa wake wa kazi tena mbele ya umma unasema alikuwa anamjenga?

Jamani somebody please help me, hivi taifa hili tuna nini vichwani? I mean some of us tunahitaji kuhamia another planet kwa sababu haiwezekani kuwa haya maovu tunayona na kuyasikia, halafu tunakuwa na this kind of thinking!

Mkuu, AU baada ya kufuatia uchunguzi uliofanywa na independent sources yaani SADC na KGM, wamemshitaki M-Tanzani mwenzetu mbele ya rais wetu, tena akiwa mbele ya marais wenzake wa Afrika, wangekuwa wa Europe, tungesema wanamuonea wazungu hao, lakini this is all Africans, halafu wewe unataka sisi wa-Tanzania at large tukisikia tusi-comment, maana ni innocent until proven guilty? Kama unayosema ni ya kweli kwa nini rais wetu hakusema hayo ya kumtetea? Halafu kwa nini hii habari ilifichwa?

I mean unahitaji kuwa professor kuelewa kuwa siku za mwizi ni arobaini, na kwa mama ya arobaini ndiyo hiii imefika period! Mkuu if yours is the case, then kwa nini hujatoa pole kwa Karamagi, mkono, na Mkapa? Halafu mbona hujajitahidi kuwajenga hapa JF?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…