Wakuu,
Hili limesemwa hapa mara nyingi kwamba Watanzania tuna matatizo makubwa, hasa sisi tunaojiita tumesoma. Akina Mkapa, JK, Mongela ni refelction ya sisi Wadanganyika ambao tunapenda vya bure, tunanyanyasa wanaotaka huduma zetu na kupiga majungu badala ya kuchapa kazi.
Watu huwa hawapendi kusikia hili lakini muhumu ni radical changes juu ya suala la kazi na kufuata sheria. Kila unapopindisha sheria hata kama madhara yake ni kuua sisimizi lazima ujue bado kuna madhara na ukipata nafasi utapindisha sheria kuua tembo.
Kwa watanzania ambao nakutana nao mimi nyumbani kwenye mabank, maofisi ya serikali, hospitali na hata kwenye sehemu za huduma, naona wengi wetu hatuna tofauti sana na hawa viongozi wetu, ukiachia wao wana nafasi ya kuiba wakati sisi hatuna.
Inabidi tuchukie rushwa, tuchukie unyanyasaji wa aina yoyote hata kama anayeguswa ni house girl, na tukiridhika labda ndio tuje na kuwanyoshea vidole akina JK, Mongela na wengine.
Ninavyoandika hivi kuna kichanga kinakufa sio kwasababu hakuna dawa, bali kwasababu mama yake hana pesa ya kuhonga, au nurse kaamua kufunika maadili aliyojifunza. Tutakavyorudi kazini Alhamisi kuna watanzania watakaa nje ya ofisi zetu masaa kibao na kuambiwa waje kesho, sababu kubwa hawana kitu kidogo cha kutuhonga ili tuwashughulikie kazi ambayo tunalipwa kila mwezi kuifanya. Badala yake wenye nacho watapitishwa mbele na kushughulikiwa.
Hata CCM waondoke madarakani, nina wasiwasi sana kama wadanganyika sisi bila kujali ni CCM, CHADEMA, CUF au TLP kama tuna nia ya kufanya tunayohubiri hapa JF.
Tuendelee kumkoma Nyani Giladi na kumsema mama Mongela kadri tuwezavyo lakini tujiangalie na sisi, je tuko tofauti na akina Mkapa? Je leo tukipelekwa TRA au kuwa gavana bank kuu, tutafanya tofauti na aliyoyafanya Balali?
Wakuu, mimi sina jibu kamili, ila kwa Watanzania ninaowajua mimi labda mmoja kati ya 100 anaweza kufanya yale tunayotaka yafanyike, wengine wote sisi hatuna tofauti na akina Mkapa au mama Mongela.
Mara nyingi nikisema haya maneno huwa namkumbuka prof. Mmari, wako wapi watiifu, wauungwana, wachapa kazi, wasiopenda makuu kama huyu mtanzania mwenzetu? Angelikuwa mla rushwa si ajabu sasa angekuwa anajulikana kuliko anavyojulikana sasa, angeheshimiwa kuliko sasa, kanisani angepewa kiti cha mbele ili
akae karibu na askofu, mchungaji au padre.
Nina imani akifa watu tutaandika sana na kumsifu mno, lakini kwanini tumsitukuze sasa na kumpandisha mbele ili vijana wetu wajue kwamba ukiwa mwadilifu unaweza kufaidika? Mungu amsaidie huko aliko.