Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Dr. Shein the next Tz President?!...God forbid. Whatever good have been said about him, his dullness is an obstacle. Siasa sio lele mama, inahitaji werevu. Hivi huyu jamaa tangu awe VP kuna kitu gani alikisimamia kikaonekana? In fact hata hiyo position aliyo nayo hafai hata kidogo.

TZ Pride, With respect nakuuliza, Je hao werevu, ambao sio dull, na ambao wameifanya siasa siyo lelemama wametufikisha wapi??, si wanachofanya ni kutumia huo werevu wao kutuingiza mjini kila siku??, Miradi kama ya Richmond, Radar, Madini, ununuliwaji wa mashangingi kwa ajili ya vigogo ndiyo faida ya kuwa na viongozi werevu na ambao siyo dull????

Simfahamu huyo VP, ila kama watu wanasema ni mchapakazi na hana kashfa mimi nitampa kura yangu, hata kama mtanicheka...huko kuzubaa kwake, au kutokuwa mwerevu hakuniumizi kichwa hata kidogo kwani kuchagua werevu ndiko kunakoimaliza Tanzania.

Samahani wanabodi kwa kutoka nje ya mada, ila nilishindwa vumilia.
 
Field Marshall Es,
Bila samahani mkuu wangu, hapa ni mahala ambapo tunamkoma nyani mchana kweupee bila uso kutushuka.
habari za mama yetu ndio hivyo kama walivyokuwa viongozi wengine wengi tu ndani ya CCM ambao pengine wamerithi Charisma ya mwalimu huko Kivukoni nikichukua maneno ya Ogah. Haiwezekani kabisa kiongozi bora kwetu ni yule mjuzi wa kutuvika vilemba bila kujali matendo yake..By the way Komando yupo Ubalozi France, naye mchovu vile vile huwezi kuamini ati kanisahau, nilikutana naye kwenye harusi Bongo pale mess akauchuna macho makavu bila kujua kama hapa ndio kafikaa...nasikia kwenye Uchaguzi sauti ilimkwama akapatwa na kigugumizi cha ghafla, Bi mkubwa alikuwa akicheza ngoma ya warumba pembeni... usifanye mchezo na UK.

Hata hivyo, uncle ndio maana nasisitiza zaidi kuwa CV ya mtu ni muhimu ikiambatana na hulka ya mtu huyo kiuongozi toka huko kwao maanake hii dream ya kuwa kiongozi wanayo wengi sana na wengi wao wamejipanga kwa madigree kibao, na wakarimu sana ugenini hasa wanapohitaji kitu lakini wakishafika mahala wakapata kile walischokihitaji basi hugeuka wakawa wanyama.

hata mwalimu wengi wamezungumza mengi kuhusu tabia yake ktk ujana wake. waliosoma naye walifahamu kuwa alikuwa mtu wa misifa, kutaka sana attention na pia mwenye uchu kiasi kwamba hakupenda kuwa nyuma. Ajabu, tabia ambayo hutumika sana kwa wale wenye uchu wa Utajiri na sio Wanasiasa kwani siasa hutanguliwa na mapenzi ya nchi na wananchi wako ktk kupata haki zao...

Nyerere, kwa charisma zake aliweza kumix tabia yake ktk siasa badala ya kutafuta Utajirina na ikakubalika, jambo ambalo sii rahisi hata kidogo na sasa hivi tunaendelea kuwaona wanafunzi wake wakijaribu kutufunga kamba za shingo kama mbuzi hali macho yao yamegota kwenye Utajiri.

Wangeweza kufanikiwa lakini wameshindwa kuelewa kuwa sasa hivi wananchi wameamka na siasa leo hii ni uchumi sio tena habari za utumwa na Ukoloni ama kufungamana na Upande wa kushoto/ kulia. Macho ya wananchi wote ni ktk fedha, hawatajali kama ni Ujamaa ama Ubepari utakao wawezesha kuondokana na Umaskini, sasa unapojaribu kuwaibia hasira zao hazina mfano.

Watakuhukumu hapa hapa duniani.
 
Bunge la commonwealth lina Dr. Shija, Bunge la Afrika lina Mama Mongela, na Bunge la dunia (utani tu) yaani UN kuna Dr. Migiro. Kwa hiyo mabunge makubwa yote yana watu wetu. Miaka ya Nyuma tulikuwa na Dr. Salim pale OAU na AU. Sina rekodi sahihi ya utendaji wa Salim pale OAU/AU ila najua kuwa hakupatwa na skendo ya aibu kama hii. Sasa kama Mama Mongela anaanza kwa kutupaka matope namna hii inawezekana generation ijayo isipate nafasi za kuongoza kwenye body za kimataifa tena.

Ningefurahi kama iwapo baada ya kuthibitishwa tuhuma hizo, serikali ya Tanzania ingechukua hatua za kisheria dhidi yake ili kuionyesha dunia kuwa alilofanya siyo hulka yetu kama taifa.
 
FM ES hivi kwanza tupe issue ya mama Tibaijuka! anything you know Maana nasikia kila kona kwamba vijana wanafanya investigations zao Nairobi, is there any grain of truth?

Ogah nimekupata mkubwa wangu. Sasa JKN is gone, what next?Surely JKN alikuwa na influence kubwa lakini at the end of the day, hatuwezi kuendelea kumbebesha mzigo, sasa destiny iko mikononi mwetu we have to do somthing. History imeshaandikwa na haifutiki lakini inawezekana tukaendelea kuwa watumwa wa hiyo historia?? Hapana mkuu!

Kwa waungwana wote, kwa kweli hapa kuna shule, muwambie vijana wanaofanya research weaje hapa wanaweza kuambulia mawili matatu.

Shalom!
 
Huyu mama naye anakosa ustaarabu na uungwana sasa kama report imetoka si aachie ngazi na kuomba msamaha maana ukiangalia hela aliyotia kibindoni kusema kweli ni ndogo,kulitia TAIFA aibu tuu.
 
Ndio uzuri wa wabongo hata uki haribu vipi be assured of support. Jamani hapa si suala la majungu wala nini Mama kalikoroga sasa alinywe tu........
 
FM ES hivi kwanza tupe issue ya mama Tibaijuka! anything you know Maana nasikia kila kona kwamba vijana wanafanya investigations zao Nairobi, is there any grain of truth?

Mkuu Heshima mbele,

Huyu mama naye ndiye wa kwanza kulikoroga na undugunization, investgations nafikiri ilishakamilika tayari, mara ya mwihsop alikuwa akihanja kutafuta support ya akina Dr. Mahiga, Mama Migiro, na Balozi Manongi kule UN, na yeye it is only a matter of time kabla hawajashauri aondolewe, yeye binafsi anajua na alishaanza kuhamisha vitu vyake nyumbani siku nyingi!
 
Mkuu Heshima mbele,

Huyu mama naye ndiye wa kwanza kulikoroga na undugunization, investgations nafikiri ilishakamilika tayari, mara ya mwihsop alikuwa akihanja kutafuta support ya akina Dr. Mahiga, Mama Migiro, na Balozi Manongi kule UN, na yeye it is only a matter of time kabla hawajashauri aondolewe, yeye binafsi anajua na alishaanza kuhamisha vitu vyake nyumbani siku nyingi!

Asante mkuu, tuzidi kuhabarishana kuhusu hawa vinara wa nchi yetu wanaoharibia vizazi vingine. Ila nadhani hapa kwa vizazi vya leo kuna kitu cha kujifunza. Ubadhirifu na upendeleo ni vitu vibaya sana, hatuna budi kuvipiga vita. Imagine top diplomat kama huyu mama na usomi wake wote anakuwa na atitude za business as usual alizozoea bongo!! Jamani tubadilike watanzania/waafrica. Vinginevyo dunia itatubadilisha at a heavy price!
 
Mwisho wa yote,,, technologia ndiyo imewezesha haya kujulikana kwa haraka na kusambaa kwa watu wengi,,, miaka ile ya nyuma Field Marshall ES angekaa na habari yake hii na kusimulia marafiki zake wachache ambao wangekuwa interested na habari hii na akiona hawako interested anaachana na hiyo story,,, anawasifia rafiki zake kwa kukomba TRA na kushusha mjumba ya nguvu kule Mbezi Beach,,, na baada ya hapo mambo yanaishia hapo!!!

Siku hizi hata mimi!!! nilioko mkabala na Pub huku Ukanda wa Gaza, nayapata haya clearly kama nasukuma mlevi vile...

Tuendelee,,,kwenye hili wengine hatuna cha kuchangia zaidi ya kuchagiza tu na kusoma kwa makini!!!
 
Wakuu,

Hili limesemwa hapa mara nyingi kwamba Watanzania tuna matatizo makubwa, hasa sisi tunaojiita tumesoma. Akina Mkapa, JK, Mongela ni refelction ya sisi Wadanganyika ambao tunapenda vya bure, tunanyanyasa wanaotaka huduma zetu na kupiga majungu badala ya kuchapa kazi.

Watu huwa hawapendi kusikia hili lakini muhumu ni radical changes juu ya suala la kazi na kufuata sheria. Kila unapopindisha sheria hata kama madhara yake ni kuua sisimizi lazima ujue bado kuna madhara na ukipata nafasi utapindisha sheria kuua tembo.

Kwa watanzania ambao nakutana nao mimi nyumbani kwenye mabank, maofisi ya serikali, hospitali na hata kwenye sehemu za huduma, naona wengi wetu hatuna tofauti sana na hawa viongozi wetu, ukiachia wao wana nafasi ya kuiba wakati sisi hatuna.

Inabidi tuchukie rushwa, tuchukie unyanyasaji wa aina yoyote hata kama anayeguswa ni house girl, na tukiridhika labda ndio tuje na kuwanyoshea vidole akina JK, Mongela na wengine.

Ninavyoandika hivi kuna kichanga kinakufa sio kwasababu hakuna dawa, bali kwasababu mama yake hana pesa ya kuhonga, au nurse kaamua kufunika maadili aliyojifunza. Tutakavyorudi kazini Alhamisi kuna watanzania watakaa nje ya ofisi zetu masaa kibao na kuambiwa waje kesho, sababu kubwa hawana kitu kidogo cha kutuhonga ili tuwashughulikie kazi ambayo tunalipwa kila mwezi kuifanya. Badala yake wenye nacho watapitishwa mbele na kushughulikiwa.

Hata CCM waondoke madarakani, nina wasiwasi sana kama wadanganyika sisi bila kujali ni CCM, CHADEMA, CUF au TLP kama tuna nia ya kufanya tunayohubiri hapa JF.

Tuendelee kumkoma Nyani Giladi na kumsema mama Mongela kadri tuwezavyo lakini tujiangalie na sisi, je tuko tofauti na akina Mkapa? Je leo tukipelekwa TRA au kuwa gavana bank kuu, tutafanya tofauti na aliyoyafanya Balali?

Wakuu, mimi sina jibu kamili, ila kwa Watanzania ninaowajua mimi labda mmoja kati ya 100 anaweza kufanya yale tunayotaka yafanyike, wengine wote sisi hatuna tofauti na akina Mkapa au mama Mongela.

Mara nyingi nikisema haya maneno huwa namkumbuka prof. Mmari, wako wapi watiifu, wauungwana, wachapa kazi, wasiopenda makuu kama huyu mtanzania mwenzetu? Angelikuwa mla rushwa si ajabu sasa angekuwa anajulikana kuliko anavyojulikana sasa, angeheshimiwa kuliko sasa, kanisani angepewa kiti cha mbele ili
akae karibu na askofu, mchungaji au padre.

Nina imani akifa watu tutaandika sana na kumsifu mno, lakini kwanini tumsitukuze sasa na kumpandisha mbele ili vijana wetu wajue kwamba ukiwa mwadilifu unaweza kufaidika? Mungu amsaidie huko aliko.
 
Mtanzania,
Mawazo yako yana ukweli mwingi sana lakini sii ndio kazi ya kijiwe hiki kujaribu kubadilisha mawazo ya wananchi kifikra?... tukiendelea kufikiria kuwa tunayoyafanya ni mazuri hali nchi inazidi kuporomoka tutafika kweli?..
Binafsi nina imani kuwa nisemayo naweza kabisa kuyaweka ktk vitendo as a fact nimekuwa nikishika fedha toka miaka ya 80 na sikuweza hata siku moja kufikiria kuiba kwanza kabla ya kujenga kile nilichotakiwa kukijenga...kifupi Tanzania kiuchumi tunakula mbegu za maendeleo yetu wenyewe badala ya kula tunachovuna na hili ndilo somo kubwa tunalojaribu kulitazama.

Moja ya magonjwa yetu ni pamoja na Undugunization lakini kama tutaelewa sumu iliyomo ktk hili na kujaribu kulitafutia anti venon ambayo inatokana na sumu yenyewe ni bora zaidi kuanza kufikiria hilo. Makosa ya mama Mongella yawe fundisho kwetu na sidhani kama ni yeye pekee alokuwa UN wapo wengi watanzania na hawa kwa hekima zao wameweza kutenganisha mila zetu chafu na kufuata taratibu walizozikuta huko. Mama Mongella katuonyesha wazi kuwa pamoja na elimu yake, hekima zake bado alikuwa na siri kubwa ktk hulka zake ambazo akiwa relaxed zimeweza kujitokeza.

Wengine tuliyajua haya longtime!
 
Mtanzania na Mkandara,
Post zenu zimenigusa sana :-
1. wahujumu uchumi, wala rushwa, mafisadi, wabaguzi wa rangi/kabila/familia kwernye kazi waendelee kukemewa ikiwezekana kukiwa na ushahidi waingie kwenye vitabu va kumbukumbu.

2. Viongozi wetu ni full reflection yetu sisi,hili nakubaliana nalo kwangu mimi vita hii wapiganaji ni jamii nzima na washindi ni Jamii nzima sio CUF wala CCM.Tuanze sasa, vita hii haiwezi kupiganwa na wanasiasa ambao kwao siasa ni ajira yao, kwa hiyo wakipata sehemu ya kula wanakula bila huruma yoyote.

3. Jiulize, mdoga wako, ndugu yako akimaliza mafunzo ya polisi pale CCP, je utapenda aajiriwe idara gani ya polisi? magereza, traffic, FFU? etc.

4. Kama jibu lako ni Traffic. jiulize ni kwa nini?
5. Je ni kwa sababu traffic kuna rushwa? hivyo ndugu yako huyu atapata mapato ya ziada?
 
Wakuu,

Mara nyingi nikisema haya maneno huwa namkumbuka Prof. Mmari, wako wapi watiifu, wauungwana, wachapa kazi, wasiopenda makuu kama huyu mtanzania mwenzetu? Angelikuwa mla rushwa si ajabu sasa angekuwa anajulikana kuliko anavyojulikana sasa, angeheshimiwa kuliko sasa, kanisani angepewa kiti cha mbele ili
akae karibu na askofu, mchungaji au padre.

Nina imani akifa watu tutaandika sana na kumsifu mno, lakini kwanini tumsitukuze sasa na kumpandisha mbele ili vijana wetu wajue kwamba ukiwa mwadilifu unaweza kufaidika? Mungu amsaidie huko aliko.


Heshima mebele mkuu,

Huyu Prof ni yupi...naomba mwanga kidogo?
 
On Mongela...ni vizuri watanzania mmoja mmoja waanza kuona vitendo kama hivi ni aibu kwa muhusika na jamii nzima. Tuendelee kuelimishana na kumkoma giladi.

Stupid Mama Mongela...heshima yote aliyojingea kitaifa na kimataifa inayeyuka kwa sababu ya pesa. Nimejiuliza...kwa umri wake na kipato cha halali alichonacho na ambacho angeweza kupata kabla siku yake haijafika...kweli alihitaji sana hizo USD 130,000..??!!! I don't think so. Her accomplishments and respect was priceless...Somo la bure kwa Watanzania wengine, popote walipo.

Chrismas Njema.
 
Heshima mebele mkuu,

Huyu Prof ni yupi...naomba mwanga kidogo?

Mkuu Yebo Yebo,

Unaweza kusoma kidogo hapa japo yaliyotajwa ni machache mno kwenye mafanikio ya huyu gwiji.

http://www.ippmedia.com/ipp/observer/2005/10/02/50917.html

Pia alikuwa VC wa Sokoine na UDSM. Alipoondolewa na rais Mwinyi kwa kukataa kutii amri mbovu za serikali na kutetea wanafunzi, alipelekwa wizarani na kupewa desk lisilo na kazi, bila kulalamika akaendelea kuchapa kazi yake akipanda dala dala kwenda kazini.

Baadaye akaenda Open University ambako kuwepo kwake pale kulisaidia mno kukitangaza hicho chuo.
 
Mtanzania, Mkandara na Kilitime asanteni sana kwa kuliweka wazi tatizo hili. Jamii yetu imekubali mno uchafu huu hata pale unapotendewa haki inavyopaswa bila upendeleo unaona ni lazima umshukuru kwa kumkatia kidogo aliyekutendea.

Tunawalaumu wageni wanapokuja nyumbani na kuajiri jirani zetu bila kujiangalia sisi wenyewe matatizo yetu! Vijana wetu hawaambiliki, wanataka utajiri wa haraka haraka kiasi cha kutisha! Bila aibu utawasikia wanavyojisifu wanavyomkomba aliyewaajiri. Hatuwaenzi waliofanya kazi kiadilifu. Kama alivyosema Mtanzania hata uzee wa kanisa hawapati maana hawana cha kuchangia kanisa bali mawazo ambayo hakuna anayeyataka. Wanapotuacha ndipo tunaandaa makongamano ya kuwaenzi kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Wakina Chiume waliishi nasi mbona tumeanza kuwaimbia ngojera pale walipoondoka tuu? Tunapenda vilemba vya ukoka, mijisifa ambayo hatustahili, maPh.D, Arusha kuitwa Geneva, n.k. Tumekuwa cynical, tusiotaka kukemewa tukijificha nyuma ya kivuli cha ubaguzi,mercenaries ambao tuko tayari kumsifia yeyote ili mradi atutupie makombo ya kwenye meza yake n.k. Mungu ainusuru nchi yetu. Mungu alinusuru bara letu.
 
Back
Top Bottom