1.
haindoi ukweli umekuwa ukiwatetea sana jamaa zako waliopo Foreign kwa amna mbali mbali na saa zingine huwa unaomba threads zihamishwe pale tuhuma zinapokuwa nzito zaidi na mfano ni ule wa Caro wa Ubalozi wetu London na mumewe kuuza bwimbwi na ulipoambiwa ulikuja juu.
Madai kuhusu Caroline, kwamba amerushwa vyeo hayakuthibitishwa sio mimi niliyeihamisha ile thread, mmiliki wa hii forum alisema wazi kuwa zitolewe evidence na akatoa muda maalum, hazikutolewa akaamua kuihamisha ile thread, mimi sio mmiliki wa hii forum huo ubavu nitautoa wapi mkuu?
Mimi siko hapa JF kufuata mkumbo na sitegemei kuwa kuna wanaofuata mkumbo wa wengine, yaani kushambulia tuu wananchi wengine bila sababu ya msingi, ili mradi kushambulia tuu waonekane wanajua na kuchafua majina ya wengine no mkuu, na wala sina jamaa foreign kama unavyodai,
However, Walter mume wa Caroline, ni mwanasheria wa kujitegemea tena kijana anayeheshimika sana Dar, kutokana na kazi zake za kisheria na yeye ni mshiriki wa umiliki wa Law Firm na baba yake, kuna vijana wengi sana wa rika lake ambao wamebobea kwenye sheria, kama kina Masha, Margai, Mujulusi, Ishengoma, na hawa kina Walter, hawa vijana ni matajiri sana kwa standard zetu za bongo na wameupata kwa haraka haraka kutokana na kufunguliwa milango ya kiuchumi hivi karibuni, sasa kama Walter anauza bwimbwi basi ina maana hawa wote niliowataja hapo juu mpaka kina Mkono wanauza hilo bwimbwi, that is a big lie kama sio a pure nonesense, wanachi ni lazima tukubali kuwa wanasheria walibanwa sana zamani, lakini sio sasa milango imefunguliwa sasa tusishangae kuwaona wanatanua ni haki yao mkuu, wao na madaktari wanatakiwa kutanua katika nchi yoyote ile yenye maendeleo.
2.
Kuhusu wakina Mahiga ndio usiseme
Kuhusu suala la Mahiga, ni yale yale kuna mtu ana chuki naye binafsi akaamua kuja hapa kumchafulia jina tu bila sababu ya msingi, mkombwa data hamna sasa hivi mkuu mnatakla tuje tu hapa na kuanza kuwatukana viongozi na wananchi bila sababu?
3.
Mzee sie wengine tunao hao jamaa huko huko CCM lakini hatuishi kuwatoa nishai kila kukicha maana nchi yetu wote na hatuwezi kujidai tunaitakia mema nchi huku tunakuwa na double standards jamaa zetu wakituhumiwa kwa ubadhirifu
Kama ni kweli basi mkuu weka ukweli hapa sio kuharibu majina ya viongozi bila sababu za msingi, mimi sina jamaa yoyote huko CCM kama wewe, lakini msimamo ni very clear kwa kila mjumbe hapa kuwa mnyonge mnyongeni lakini haki apewe, ukweli uwekwe hapa hakuna sababu ya kuleta viroja, hoja hujibiwa kwa hoja ila mimi msimamo wangu ni ule ule siwezi kushambulia wananchi wasiokuwa na makosa ili tu nionekane nimo kwenye crowd, hapana mkuu!
4.
Nakuheshimu sana lakini saa zingine huo moyo wako wa kuwatetea hawa watu huwa inaboa haswa
Nimekusikia mkuu, lakini kwenye hoja hakuna boa nia na madhumuni hapa ni kuweka hoja na kupingana kihoja, anything else ni lazima iboe maana hakuna ukweli ndani yake sasa si lazima iboe!