Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Hayo ya hela sina uhakika, ila ajira ya mkwe wake ni kweli. Ila kwa sasa hayupo AU tena, alibadilishiwa ajira. Huyo binti alimaliza Law UD mwaka 2000 kama sikosei
 
FM ES hebu tuulizane humu ndani. Je hii taarifa ilikuwa na ukweli kiasi gani au ni uzushi?? Huyo mama hadi leo sijasikia kama amefukuzwa kazi au kesi ya namna hiyo dhidi yake. Au pengine niko outdated. Kama kuna mwenye taarifa updated kuhusiana na ukweli au uongo wa taarifa hii tafadhali anisaidie.

Tusije tukawa tunachafua majina ya viongozi wengine innocent bila sababu yoyote.

Au kama kuna mtu analitaka jimbo lake aseme. Au isikute ni yale yale makundi ya mafisadiz wanataka kumaliza strong ssm MPs?? Au kutaka kuwachafua ili nao waonekane wachafu kama walivyo SSM MP na Mins mafisadiz.

Yaani unasema Mwanahalisi walidanganya au na wewe huna uhakika? Je ni lini mara ya mwihso ulimsikia huyu mama akisema kama zamani? Unafikiri kwa nini amekuwa kimyaa?

Otherwise naona kuna majibu ya kutohs ahapa kuhusu swali lako, wakuu haya ya dini, ukabila na undugu hayawezi kutusaidia wabongo na taifa letu, tukumbuke hapo tunaowapiga mawe hapa JF kila siku na wao pia wana ndugu, makabila yao na dini zao, au tufike mahali tuache kabisa kuwaongelea viongozi.

Naona siku hzizi kila mwenye kiongozi wa dini au kabila lake lazima anajaribu kuwa mkali sana bila hoja, well na viongozi wengine pia wana dini na kabila zao, au?
 
Na Aristariko Konga

BALOZI Getrude Mongella, Rais wa kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) amelazimika kujiuzulu kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na ajira za upendeleo katika ofisi hiyo.

Hatua ya kulazimishwa kuachia ngazi imekuja baada ya mlolongo wa malalamiko kutoka kwa wabunge wa PAP kutokuridhika na mwenendo wa matumizi ya fedha na uendeshaji wa ofisi hizo.

Nafasi yake imechukuliwa na Dk. Idriss Ndele Moussa, Mbunge kutoka Chad, katika uchaguzi uliofanywa na bunge hilo 28 Mei mwaka huu. PAP ina makao makuu katika mji wa Midrand, nchini Afrika Kusini.

Dk. Ndele aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili; Lassane Sawadogo, mbunge kutoka Burkina Faso na Mustafa El Gendy, kutoka Misri.

Dk. Ndele aliapishwa na Dk. Mongella kuchukua wadhifa huo mpya, akiwa na kazi ya kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi na utendaji wa PAP, kutokana na maagizo ya wabunge ya 19 Mei, mwaka huu huko Midrand.

Bunge la Afrika pia lilichagua makamu wanne wa rais ambao ni Bethel Amadi (Nigeria), anayewakilisha Kanda ya Afrika Magharibi na Mary Mugyenyi (Uganda) anayewakilisha Afrika Mashariki.

Wengine ni Laroussi Hammi (Algeria) anayewakilisha kanda ya Kaskazini, na Joram Gumbo (Zimbabwe) anayewakilisha kanda ya Kusini mwa Afrika.

Mabadiliko yanatokana na kuwapo tuhuma dhidi ya Mongella kuwa chini ya uongozi wake, ajira zilipatikana kwa misingi ya upendeleo na bila kufuata taratibu za ajira wala sifa za watumishi.

Habari zinasema kuwa katika siku za karibuni, kabla ya mabadiliko hayo, Mongella alijaribu kungangania ili aendelee na wadhifa huo, lakini alishinikizwa kuachia ngazi, jambo ambalo lilikamilika 28 Mei mwaka huu.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk. Thomas Kashilila, alipoulizwa juzi Jumatatu, alikiri kuwa na taarifa za Mongella kuacha wadhifa huo, ingawa ofisi yake haikuwa na taarifa rasmi kutoka PAP.

Tumepata taarifa kupitia njia nyingine, lakini hatuna taarifa rasmi kuwa kaacha wadhifa huo, alisema Dk. Kashilila.

Mwenendo wa Mongella uliishakuwa hoja hadi wakuu wa nchi za Afrika kuunda kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa usimamizi na uendeshaji wa PAP.

Taarifa zinasema bunge lilijadili kwa kina taarifa ya kamati hiyo na kujiridhisha kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya fedha.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, inaelezwa kuwa serikali ya Tanzania imekubali kubeba mzigo wa kulipa fedha zote ambazo Mongella alituhumiwa kuzitumia vibaya.

Taarifa zinasema awali, hata baada ya serikali ya Tanzania kuchukua mzigo huo, Mongella alishauriwa ajiuzulu ili kulinda heshima ya Tanzania, lakini aligoma kufanya hivyo.

Wabunge wa Bunge walilalamika kwa viongozi wakuu wa nchi za Afrika juu ya uongozi wake kwa ujumla, ambao wanadai haukuwa na dira wala tija.

Kuna madai pia kwamba alingangania kubaki katika nyumba ya Bunge na alipolazimishwa kuondoka akaamua kuhama na fenicha zote za ndani akidai ni zake, jambo ambalo si la kweli, alisema mbunge mmoja wa Bunge la Afrika kutoka Tanzania ambaye hakupenda kutajwa jina.

Aidha, uongozi wa Mongella umelalamikiwa kwa kushindwa kufanya jambo la maana wakati uliendelea kugharimu rasilimali za nchi za Afrika.

Mjadala wote wa kumuondoa Mongella ulikuwa unaripotiwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari vya Afrika Kusini na Namibia. Kuna wakati Mongella alilazimika kukatisha kikao cha Bunge hilo na kufanya mazungumzo ya faragha na makamu wake wawili.

Baada ya kikao hicho cha siri, Mongella aliamuru waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia kikao waondoke, jambo ambalo lilifanyika.

Naye mbunge mpya wa Tanzania katika PAP, John Cheyo amesema Mongella atakumbukwa kwa kuwa rais wa kwanza wa PAP.

Ni MwanaHALISI iliyowahi kuandika katika toleo Na. 73 la Novemba 28 hadi 4 Desemba 2008, kwamba Mongella alikuwa anatuhumiwa kutenda makosa ya kukosa uaminifu, wizi na utoaji ajira kinyume cha taratibu.

Kuhusu wizi, Mongella anatuhumiwa kutafuna dola za Kimarekani 138,000 sawa na Sh. 180 milioni za Tanzania, mali ya PAP.

Katika tuhuma za utoaji ajira, Mongella anatuhumiwa kuajiri jamaa zake ndani ya Sekretarieti ya Bunge hilo, kinyume cha taratibu. Tayari Bunge limeagiza kufuta ajira zilizofanywa na Mongella.

Kwenye moja ya magazeti ya Tanzania leo tarehe 15.06.2009 limeongelea suala la Dkt Slaa kukusudia kuhoji Bungeni kuhusu matumizi ya TZS milioni 180 kumlipia Dkt. Mongella huko Bunge la Afrika kama fedha zilizopotea chini ya utawala wake.

SWALI:NINI KIMEMSIBU HUYU MAMA ALIYEKUWA KATIBU WA ULE MKUTANO WA DUNIA WA AKINA MAMA WA BEIJING?
MAMA ALIYEKUWA ANATAZAMWA KAMA "MODEL" KWA VIONGOZI VIJANA WANAWAKE WA KITANZANIA?
 
MMh kama hizo tuhuma ni kweli atakuwa ametuangusha sana,na nchi yetu kwa ujumla kweli fedha fedheha
 
Tatizo limeanzia humuhumu nchini. Kaona viongozi wenzake wa Bongo wanakuwa mabilionea nae kaamua kula kulingana na urefu wa kamba yake. Ingekuwa we Wayne ungefanyaje?
 
Tatizo limeanzia humuhumu nchini. Kaona viongozi wenzake wa Bongo wanakuwa mabilionea nae kaamua kula kulingana na urefu wa kamba yake. Ingekuwa we Wayne ungefanyaje?
Ingekuwa mimi ningesimama kwenye one of my principles which states that :Value is like a fingerprint/footprint , it remains wherever you touch/put your foot.
 
Tatizo limeanzia humuhumu nchini. Kaona viongozi wenzake wa Bongo wanakuwa mabilionea nae kaamua kula kulingana na urefu wa kamba yake. Ingekuwa we Wayne ungefanyaje?
kama mshahara mizuri na marurupu mbona kesha pata saana kwa kuwa mbunge wa ukerewe sijui miaaka mingapi , waziri, cc, mkutano wa wanawake beijing ndio alikuwa raisi wao kaka nje miaka mitatu kwa post hiyo tena un, na hii mikataba ya ovyo ovyo au rushwa zetu za kitanzania kesha chukua saana, sasa PAP ilikuwa ni arobaini za mwizi
 
Huyu Mama Mongela ndiyo tabia yake, hata UN New York alimchomeka mdogo wake na sasa kuna mtoto wa mdogo wake yuko anafanya kazi pale ubalozi wa Tanzania UN.Kazi ki-undugunization pamoja na ufisadi mwingine.
 
Last edited:
Hizi tabia za kulazimisha kubeba watu kaanzia hapahapa bongo, si mnaona yule kijana wake kmuu wa wilaya kule kigoma! Alikuwa na mikashfa kibao kabla ya hapo na hata waandishi makini walishawahi kulalamikia hilo, lakini nadhani kwa shinikizo la mama huyu hatimaye akapata ulaji wa u-DC.
 
Duu!! ufisadi wa kitanzania umevuka mipaka ya nchi?!! Angalau wabunge wa Bunge la Afrika wamesema enough is enough. No to Mongella. Let it be our motto - NO TO ALL FISADIS
 
Hii si habari mpya hapa JF, na kama wewe ni member mfuatilia hii sio story ufisadi wake ulisemwa and this was coming. Not a suprise at all.
 
na kama Bunge letu liko makini pamoja na chama tawala na serikali yake, huyu anatakiwa asimamishwe kuwa Mbunge au alazimishwe kujiuzulu, kuwa banned kugombea 4 the next 5 years.
 
Sio kila mahali style ya kulindana (kama ya CCM) inafanya kazi. Mama atakuwa amekosea sana kama alifikiri hivyo. Wenzetu wako makini na hawana tabia hizo.
Hii ni aibu kubwa sana kwetu. Kama ni kweli hata watu wa Ukerewe wajulishwe Aibu aliyoileta Mbunge wao kwa Tiketi ya CCM.
 
Kwa Bongo jinsi ilivyo, si ajabu akarudi hapa na kupewa uwaziri au nafasi nyingine kubwa tu ili aendelee kufanya ufisadi!
 
Hii si habari mpya hapa JF, na kama wewe ni member mfuatilia hii sio story ufisadi wake ulisemwa and this was coming. Not a suprise at all.
Unaposema si habari mpya ,you mean 2 say ULIJUA KUWA SERIKALI IMEMLIPIA FEDHA ANAZODAIWA KUCHOTA huko PAP?
 
hiyo yote haisaiidii labda hao PAP wamchukulie shelia wenyewe lakini sisi kama watanzania hatuwezi kufanya chochote juu yake, tutabaki kuumia tu.
 
Mimi naona tungepata source of any of these information ingekuwa bomba zaidi, any way ngoja tujaribu katika haya manews ya kimataifa zaidi.
 
Folks hii habari imejulikana kitambo sana. Ambao hawafuatilii mambo ndo wanashangaa. Ukweli ni kwamba hii kashfa ya huyu mama ni ya siku nyingi..infact JK na Membe walijaribu kulimaliza kikubwa na wakubwa wenzao kwenye mkutano wa wakubwa wa Africa lakini pressure ilikuwa kubwa sana. Ndo maana TZ ilikubali kulipa gharama za upotevu wa pesa. Ilibidi huyu mama afukuzwe kwenye kikao cha AU kule Accra juzi juzi..lakini nadhani JK alitumia diplomasia kuogopa damage kwa nchi yetu.

In all, this is not new. FMES na wengine kibao humu nadhani waliweka details nyingi humu JF na tuhuma zake kuchambuliwa. na huu wizi uliripotiwa na international auditors..nadhani KPMG au Coopers kama sikosei.

Ni kama leo tukisikia Tibaijuka ameondolewa..wengine hatutashangaa maana dossier ipo siku kibao kuonyesha jinsi mama alivyovuruga..

Let her go..its a disgrace..Sema tuu wanaharibia wengine wenye moyo wa kuhangaika na kusonga mbele banking on diplomatic image of our country.
 
Mwalimu akifufuka leo akazisikia habari hizi.....Huyu mama alikuwa ni mmoja wa watu walooaminiwa sana na Mwalimu.
 
Back
Top Bottom