Mama mzazi amzika mwanaye usiku wa manane baada ya mtoto kufa kwa njaa

Mama mzazi amzika mwanaye usiku wa manane baada ya mtoto kufa kwa njaa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Salah Jackson (5) mwenye ulemavu wa viungo, mkazi wa kijiji cha Makiwaru Mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kutokana na njaa na kisha mama yake mzazi kumzika kimyakimya usiku wa manane.

Mtoto huyo anadaiwa kuzikwa na mama yake mzazi aitwaye Rebecca Siowi (30) usiku wa kuamkia Aprili 22, 2022 nyumbani kwa bibi yake walikokuwa wakiishi yeye pamoja na mama yake baada ya mume kumtelekeza na watoto watano.

Tukio hilo liligundulika baada ya mtoto huyo kutoonekana jioni ya Aprili 21 nyumbani alikokuwa akiishi kwa bibi yake, ambapo bibi yake huyo alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake huyo bila mafanikio ndipo Aprili 22 alipobainika kuwa amezikwa.

Akizungumzia tukio hilo leo Aprili 23, 2022 Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amekiri kuwepo kwa tukio hilo, akisema baada ya kupata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa wananchi walifika eneo la tukio kuona sehemu alipozikwa mtoto huyo.

Kamanda Maigwa amesema walipofika eneo la tukio walilazimika kuomba kibali cha kuufukua mwili wa mtoto huyo ili kujua sasababu hasa za kifo cha mtoto huyo kutokana na maneneo ambayo yalikuwa yakisemwa mtaani.

"Hili tukio kweli lipo na baada ya Jeshi la polisi kupata taarifa juu ya tukio hilo tulienda kuomba kibali cha kufukua mwili wa mtoto ili kujiridhisha sababu za kifo cha mtoto huyo ni nini kutokana na maneno mengi yaliyokuwepo mtaani.

"Tulifukua mwili jana na kuupeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na majibu ya daktari yalipotoka yalionyesha kwamba huyu mtoto alikufa kutokana na njaa,” amesema Kamanda Maigwa

Akizungumzia tukio hilo, jirani wa familia hiyo, Maria Nko amesema hata kama mtoto huyo alikufa kwa njaa mama yake huyo hakupaswa kumzika mwanaye kama mbwa tena usiku wa manane.

"Kwa kweli hili tukio linaumiza na inaonekana huyu mama alikuwa akimtesa huyu mtoto kutokana na ulemavu aliokuwa nao, inakuwaje hao watoto wake wengine hawajafa na njaa na kwa nini amzike mwenyewe tena?” amehoji.


Source: Mwananchi
 
Sidhani kama ni sahihi ku "attack"jamii fulani kwa ujumla katika sifa mbaya
Matukio mabaya yameshamiri sana huko uchagani siku za hivi karibuni.tulitegemea wao ndio atleast jamii iliyokua imestaarabika hapa Tanzania,sasa na wao wamekengeuka.
 
Mtu kazika mwanae kwa uchungu wewe unashauri asizike peke yake wakati wa njaa hamkumsaidia

Ukiangalia maneno ya jirani utajua kuna kitu
Tangu lini mwanamke akazika peke yake ingawa hawajasema mila zake ila jina ni la kikristo
Wengine hawakufa na njaa ila mlemavu ndio kafa kwa njaa huoni Kuna kitu hapo

Alimtesa kwa ulemavu wake na inaonyesha hakuwa anampa chakula ili afe
 
Unafiki wa wanadamu utaonekana hapa, mama wa watu kapambana na mwanae ,wanadamu wanamtazama Leo wanajifanya wema na linaloshikitisha zaidi msibani watapika chakula
Umesoma na kuelewa kweli?
Huyo mama ana watoto wengine na wako na afya vzr, kwanini hao wengine hawajafa njaa?
 
Umesoma na kuelewa kweli?
Huyo mama ana watoto wengine na wako na afya vzr, kwanini hao wengine hawajafa njaa?
Nikuulize wewe kama umesoma na kuelewa kwamba huyo mtoto alikuwa na ulemavu au huoni hiyo ni changamoto kwake?

Pengine hao wengine walikuwa wanaenda hata jalalani kujiokotea chochote lakini huyo ilishindikana kutokana na hali yake.

Ila wanadamu ndivyo walivyo siku wa msiba wa mtu aliyekufa kwa njaa kitapikwa kila kitu ambacho marehemu alikihitaji kidogo tu
 
Tena mwanadamu anahoji kwa kushangaa kabisa watoto wengine kuwa hai na kutokufa njaa. Mama wa watu kafanya lililo jema kwake kama hakuna aliyeweza kumsaidia wakati mtoto akiwa hai kwa nini ahangaike na watu akiwa mfu?
 
Back
Top Bottom