Mama mzazi amzika mwanaye usiku wa manane baada ya mtoto kufa kwa njaa

Si huwa mnasema kwamba kilimanjaro ni matajiri inakuwaje mtoto anakufa kwa njaa ?
 
Jamii mbona haijamsaidia kitu hilo gazeti limeweza kupata habari na kuuza ila hawakuweza kupata taarifa ya mtoto mwenye njaa..
Majirani husika ndio ujua watoto wanaishije then wao ndo utoa taarifa kwa mamlaka husika au media,kisha Media inapost kisha Jamii utoa msaada husika
 
Aafu kuna wachungaji na manabii wananunua ma VX,Range na Prado badala ya kusaidia wasiojiweza km hawa. Upuuzi mtupu!
 
Kweli Tanzania tumefikia njaa ya namna hiyo, ya kuua mtoto na kuzika usiku? Hili tukio lina ukakasi
 
Jamani hamna hata majirani, angepewa japo uji tu? Kufa kwa njaa Tz hii😪, ndiyo maana najisikia vibaya nikibakisha chakula nikataka either kukitupa kumbe kuna watu wanakufa njaa, so sad
 
Mtu kazika mwanae kwa uchungu wewe unashauri asizike peke yake wakati wa njaa hamkumsaidia
Kabla hawajamsodoa huyu mama walikuwa wapi kumpa Msaada!! Sasa hata wakichonga midomo hiyo mama akifungwa hao wengine nao si watakufa!? Serekali imuonee huruma kaya Maskini
 
Kama ni kweli basi huyo mkurugenzi aletwe jela hapa Arusha ajikwe tyakko lake.
Akitoka hapa ataheshimu hata kuku wake wa kisasa.
 
Tatizo hapo ni Ulemavu wa huyo Mtoto na sio Njaa kama inavyosemekana. Ni kweli amekufa kwa njaa lakini yupo aliyemuua ambaye alipaswa ampe Chakula na hakumpa.

Swali la Msingi: Kwanini hakumpa chakula Mtoto kwa wakati hata kupelekea kufariki kwa njaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…