TANZIA Mama Mzazi wa MC Pilipili afariki Dunia kwa ajali

TANZIA Mama Mzazi wa MC Pilipili afariki Dunia kwa ajali

Bodaboda siku ya harusi ya mwanaye? Msiwe mnawaleta wazazi mjini kama hamuwapendi hivyo.

Kubadili nguo salasala ? Tena wewe mgeni bongo.

Ukute ndo hiyo wanasema "Tunataka damu ya uchungu" Ngoja tu tutasikia.
Acheni roho za korosho kwani wangapi wanakufa kwenye magari?

Cha msingi ni kuwa makini ila sio kusema ukitumia usafiri flani huwezi kukumbana na kifo.

Watanzania acheni ujuaji wa kila kitu.
 
Na Bwana harusi akaenda honeymoon... Eti wakaenda kumpa taarifa akiwa anakata mauno kwa mbuchuchu iliyobarikiwa. Watu wana roho ngumu sana wallah....

Yaani mama yuko kwenye friji wanamwacha mtoto akakate mauno kwanza ndo wampe taarifa....
Hakushangaa kutomuona mama yake ukumbini?
 
Mwendazake huyo akienda hudhuria harusi ya mtoto wake na kupata ajali hiyo mbaya usiku wa kuamkia Desemba 20,2020 maeneo ya Afrikana Jijini Dar es Salaam.

Tunatoa pole nyingi kwa familia yote
Na kwamujibu wa mc Pilipili ni ajali iliyohusisha bodaboda mbili na pia marehemu mama mzazi pamoja na mama mdogo walikuwa wamepanda mshikaki. Elimu bado inahitajika kwa hawa bodaboda na watumiaji bodaboda kuchukua tahadhari kuepuka ajali Kama hizi.
 
Pale Africana kwa akina Mange Kimambi kuna shetani kwenye mbuyu!
Kuanzia SKANSKA (IPTL) mpaka Kona ya Kwenda Kwa KUSAGA Mbele ya Kina Mange Mataa ni hatari sana,Pamekula Vichwa Vingi Sana!! Nikitoka Arusha kuja Dar sipandi magari ya njia hiyo(Bagamoyo) ,napanda ya morogoro road.
 
Bodaboda ni usafiri hatari sana kwenye barabara yenye magari mengi....Pili madereva wengi wa bodaboda si madereva kabisa ni mtu tu anjifunza leo kuendesha bodaboda baada ya siku mbili anaenda kwa muhindi na laki yake anapewa boda ya mktaba anaingia barabarani kula vichwa! Madereva wa bodaboda wanaojielewa hawazidi 5% yaani katika 100 unapata wa 5 wanaojielewa.
 
Sema unatania!!

Huyu jamaa nilishaacha kumfuatilia tangu alipoonesha ulimbukeni wa kupitiliza kwa wanawake!! Wacha leo nimtembelee!!!
Sure mzee, yyko Instagram anapost kwa kwenda mbele utadhan hajafiwa
 
Kuna elements za dharau kwenye post hii,au wewe ni mzito kujiongeza.Wewe hujui board inatutoaga hasa kama kuna foleni na umechelewa unakokwenda? inawezekana siyo kwamba ni suala la uwezo kuwa mdogo bad timing too.Hiv huwezi tuu kujiuliza siku ya harusi ya mtoto wako usafiri usafiri na bodaboda.hata kama huna gari
Mkuu umesema kweli kabisa. Kuna siku nilikuwa naenda airport nikaona foleni kubwa na check in international flight haikuwa rafiki kabisa nikaona ndege itaniacha. Nilichukua bodaboda 2 moja ya mizigo na moja Mimi. Hapo utaniita mshamba au maskini? Hatupendi bodaboda ila wakati mwingine zinaokoa jahazi la muda.

Kuna siku moja nilikuwa maeneo ya Hyatt Reagency the Kilimanjaro. Kuhamaki anamuona Mo Dewji anashuka kwenye Bodaboda anawahi business meeting. Alimpa yule Boda nyekundu kadhaa mpaka nikaona kama aliduwaa hakuamini. Hapa utasema Mo ni maskini? Baada ya kama 30 minutes ndiyo Range la Mo likaingia Kilimanjaro kumsubiri.

Kwa huyu mama inasemekana walikuwa wanakimbilia kwa fundi kuchukua nguo ya kubadili. Hapa alaumiwe fundi kwa kutokamilisha nguo mapema au wenye nguo kuchekewa kuchukua.
Ila yote tisa kifo ndiyo kitu pekee mwanadamu hajui siku yake na kwa namna gani. Hivyo tuache maneno mengi.
 
Poleni sana wafiwa. Mungu awarehemu mama MC na mama yake mdogo
 
Uzembe, ujinga utazungumzwa tu, kama ndio chanzo Kifo....Mf.kupanda mishkaki serikali imetahadharisha sana....
 
Back
Top Bottom