Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 11,074
- 20,608
Acheni roho za korosho kwani wangapi wanakufa kwenye magari?Bodaboda siku ya harusi ya mwanaye? Msiwe mnawaleta wazazi mjini kama hamuwapendi hivyo.
Kubadili nguo salasala ? Tena wewe mgeni bongo.
Ukute ndo hiyo wanasema "Tunataka damu ya uchungu" Ngoja tu tutasikia.
Hakushangaa kutomuona mama yake ukumbini?Na Bwana harusi akaenda honeymoon... Eti wakaenda kumpa taarifa akiwa anakata mauno kwa mbuchuchu iliyobarikiwa. Watu wana roho ngumu sana wallah....
Yaani mama yuko kwenye friji wanamwacha mtoto akakate mauno kwanza ndo wampe taarifa....
AiseePale Africana kwa akina Mange Kimambi kuna shetani kwenye mbuyu!
Na kwamujibu wa mc Pilipili ni ajali iliyohusisha bodaboda mbili na pia marehemu mama mzazi pamoja na mama mdogo walikuwa wamepanda mshikaki. Elimu bado inahitajika kwa hawa bodaboda na watumiaji bodaboda kuchukua tahadhari kuepuka ajali Kama hizi.Mwendazake huyo akienda hudhuria harusi ya mtoto wake na kupata ajali hiyo mbaya usiku wa kuamkia Desemba 20,2020 maeneo ya Afrikana Jijini Dar es Salaam.
Tunatoa pole nyingi kwa familia yote
Kuanzia SKANSKA (IPTL) mpaka Kona ya Kwenda Kwa KUSAGA Mbele ya Kina Mange Mataa ni hatari sana,Pamekula Vichwa Vingi Sana!! Nikitoka Arusha kuja Dar sipandi magari ya njia hiyo(Bagamoyo) ,napanda ya morogoro road.Pale Africana kwa akina Mange Kimambi kuna shetani kwenye mbuyu!
Sasa Ajali imetokea wapi? Africana au Africasana?Africana — Mbezi Beach.
Africa Sana — Sinza.
Subhana Allah Kifo kina sababu jamani!!!daahMama mwenyewe alitoroka bila kuaga akachukua toyo mc pilipili Wana mtafta haonekani ndio kupigiwa simu ajali imetokea
Sasa Ajali imetokea wapi? Africana au Africasana?
Sure mzee, yyko Instagram anapost kwa kwenda mbele utadhan hajafiwaSema unatania!!
Huyu jamaa nilishaacha kumfuatilia tangu alipoonesha ulimbukeni wa kupitiliza kwa wanawake!! Wacha leo nimtembelee!!!
Dereva Boda boda amepona?Inasemekana mama yake alikuwa na nguo specific antaka kuivaa ikabidi aifate kwa fundi chap na boda boda maana mda wa kwenda Ukumbini ulishafika.
Na kifo hutafta sababu Mungu awatie nguvuSubhana Allah Kifo kina sababu jamani!!!daah
Acha woga mkuu! Huko unakopita hakunaga ajal?Kuanzia SKANSKA (IPTL) mpaka Kona ya Kwenda Kwa KUSAGA Mbele ya Kina Mange Mataa ni hatari sana,Pamekula Vichwa Vingi Sana!! Nikitoka Arusha kuja Dar sipandi magari ya njia hiyo(Bagamoyo) ,napanda ya morogoro road.
Mkuu umesema kweli kabisa. Kuna siku nilikuwa naenda airport nikaona foleni kubwa na check in international flight haikuwa rafiki kabisa nikaona ndege itaniacha. Nilichukua bodaboda 2 moja ya mizigo na moja Mimi. Hapo utaniita mshamba au maskini? Hatupendi bodaboda ila wakati mwingine zinaokoa jahazi la muda.Kuna elements za dharau kwenye post hii,au wewe ni mzito kujiongeza.Wewe hujui board inatutoaga hasa kama kuna foleni na umechelewa unakokwenda? inawezekana siyo kwamba ni suala la uwezo kuwa mdogo bad timing too.Hiv huwezi tuu kujiuliza siku ya harusi ya mtoto wako usafiri usafiri na bodaboda.hata kama huna gari
Yaani hakikwepeki aiseeKifo kikifika siku yake, kinakuita na unakifuata
Acha woga mkuu! Huko unakopita hakunaga ajal?
Kumbe unaogopa kifo eeh, haaaa haaaMorogoro road sio hatari sana kipande kidogo cha ruvu ndio kilikuwa hatari ila kwasasa kipo poa.
Kumbe unaogopa kifo eeh, haaaa haaa
Uzembe, ujinga utazungumzwa tu, kama ndio chanzo Kifo....Mf.kupanda mishkaki serikali imetahadharisha sana....Mkuu umesema kweli kabisa. Kuna siku nilikuwa naenda airport nikaona foleni kubwa na check in international flight haikuwa rafiki kabisa nikaona ndege itaniacha. Nilichukua bodaboda 2 moja ya mizigo na moja Mimi. Hapo utaniita mshamba au maskini? Hatupendi bodaboda ila wakati mwingine zinaokoa jahazi la muda.
Kuna siku moja nilikuwa maeneo ya Hyatt Reagency the Kilimanjaro. Kuhamaki anamuona Mo Dewji anashuka kwenye Bodaboda anawahi business meeting. Alimpa yule Boda nyekundu kadhaa mpaka nikaona kama aliduwaa hakuamini. Hapa utasema Mo ni maskini? Baada ya kama 30 minutes ndiyo Range la Mo likaingia Kilimanjaro kumsubiri.
Kwa huyu mama inasemekana walikuwa wanakimbilia kwa fundi kuchukua nguo ya kubadili. Hapa alaumiwe fundi kwa kutokamilisha nguo mapema au wenye nguo kuchekewa kuchukua.
Ila yote tisa kifo ndiyo kitu pekee mwanadamu hajui siku yake na kwa namna gani. Hivyo tuache maneno mengi.