Wee tena ukute ni mkwe wa kitanga, Pole sana, kwa kweli sijui shida ipo wapi kwa hawa wakwe zetu wa kike, wakati mwingine unajishusha down to earth lakini haoni jema lako hata moja, muda wote yeye anakukosoa na kukusema, unakaa kimya unamvumilia tu kwa sababu mwisho wa siku atarudi kwake
Ila kuna wengine hawawezi kuvumilia kabisa, mimi katika watu ambao huwa hawanipi tabu ni mama mkwe, hata nikimkuta amenuna au ananisema huwa natabasamu namuuliza mama nikiletee supu? Au namletea glass ya maziwa halafu namuuliza nini kimekukwaza mama
Wakati mwingine nikimsikia ananisema namletea doti ya kitenge namwambia leo nimekununulia zawadi, mwisho wa siku akaacha kabisa akawa anaona aibu maana niliamua kudeal nae kidiplomasia, akawa sasa anawasumbua madada wa kazi na watoto,nikipanga ratiba anapangua anapanga yake
Halafu hata mtoto wake asikie mama ananisema, akikasirika akitaka kugombana na mama mimi huwa nasimama upande wa mama, namwambia afterall she is a mother na wala huwa simruhusu aingilie makwazo au kero anazosababisha mama hata kwa wadada wa kazi au kwa watoto, maana huwa naona ni mambo ya kupita tu, imefika mahali wake wa mashemeji zangu wote wamemsusia mama, na mama hathubutu kwenda kwao maana akifika wanafungasha wanasepa mpaka mama aondoke, ile mimi walaaaa, hata mama akigombana na mzee huko nyumbani au akikwazika anakimbilia kwangu kupunguza mawazo na wala huwa hanipi shida, naenda nae tu hivyohivyo ingawa wakati mwingine nakwazika naumia na maneno yake, hana shukrani saingine mlalamishi tu anacholalamika hakina maana
Siku moja nimeenda kazini nimemwachia dada maagizo, mama akainhia jikoni kachemsha mihogo na maharage akawalisha watoto, anasema ati tinawapa watoto maisha ya anasa, nimerudi watoto wana njaa namuuliza dada watoto hawajala akanisimulia wala sikukasirika, nikaingia nikawapikia watoto
Jama hupendinkero za mkwe wako, jitahidi usije kuwa mkwe wa namna hiyo huko mbelenu, watoto wako wataoa/olewa, jiulize wewe utakua mkwe wa namna gani, usiruhusu watoto wa wenzio wasononeke kwa sababu yako, kupitia wakwe zetu, tupate somo.