Mama ntilie Tanzania wachafu; wa Rwanda wana usafi wa hali ya juu

Mama ntilie Tanzania wachafu; wa Rwanda wana usafi wa hali ya juu

Rwanda hakuna Wapumbavu na Wachafu kama huko Kwingineko Mkuu Mtani wangu.
Huku kwetu sasa ni shida, unakuta mama ntilie na mtoto wake mdogo anayetambaa. Mtoto akijisaidia anaenda kumsafisha bila umakini wowote na anaendelea kuhudumia wateja bila ya kunawa mikono kwa usahihi. Maji wanayooshea vyombo ukifanikiwa kuyaona unaweza ukaahirisha kula, alafu vyombo vyenyewe hawaoshi wanachovywa tu kwenye maji na kusevia vyakula.
Angalia sasa wasaidizi wa hao mama ntilie, kuanzia nguo walizovaa hadi usafi wao binafsi, ni majanga matupu. Yaani ni kama baadhi ya watu wanaishi tu kwa kudra za mwenyezi mungu kutokupata magonjwa ya matumbo/kuhara.
 
Kwenye usafi Rwanda ipo Ligi Kuu na Tanzania ipo Ligi daraja la tatu. Nina ushahidi kuhusu Hilo.
usafi wa wapi? wa kigali mitaa michache ya katikati tu? au rwanda mikoa yote? hata bongo ukienda oysterbay, masaki na baadhi ya maeneo, ni kama ulaya tu hata nchi hakuna, ila ukija manzese ndio utaona hilo. kuna maeneo Nairobi hayafai kuitwa africa kabisa, ila maeneo mengine ndio hivyo tena kwa waswahili. ukitaja rwanda, sema rwanda, na ukitaja Kigali sema kigali.
 
Nyama za kukaanga anashika tu na mikono anaweka kwenye bakuli. Nikasema ehee.mtu hanawiii.Hapana
Sasa hivi nanunua mchele wangu nusu na robo napika asubuhi nakula mpaka usiku.
Halafu anapokatia katia nyama mbichi kabla ya kuchoma, ndipo tena anaweka nyama iliyokwisha chomwa kabla ya kukusevia. Mwingine anapokea pesa na kurudisha chenji halafu anaendelea kukuhudumia bila ya kunawa mikono.
 
Hivi mabibi afya na mabwana afya nchi hii wapo kweli?
Ripoti ya wafaransa imeeleza Kwa kina mama ntilie Tanzania ni wachafu kuanzia kutooga, vyombo hawaoshi vizuri na ripoti imesema mama ntilie Tanzania ni sawa na mazingira ya kulelea watoto, yaani kwenye mama ntilie 10 basi saba huenda na watoto wadogo,
Rwanda kinara, imeonekana mama ntilie Rwanda wana usafi wa hali ya juu kuanzia mazingira hadi wao wenyewe, na wamepongezwa sana.
Hivo tukaze buti ili mwaka mwingine walau tuongoze
Hao Wafaransa wamepoteza muda na rasilimali kufanya huo utafiti. Wangeuniuliza ningewapa majibu sahihi.
 
Ila wabongo ustaarabu Ziro kabisa. Mtu anapuliza mfukoni anakuwekea vitafunwa na Wala haoni shida.
mwingine zile tissue za kufutia glass kwenye glossery huwa wanazikata mara mbili. Ila sasa anazimwaga zote kwenye mapaja (sketi) yake then anakuwa anakata na kuziweka kwenye glass tayari kwa kuhudumia wateja. Toothpick zikimwagika chini kwa bahati mbaya wanazizoa na kuzitumia tena kwa kuwapa wateja.
 
Halafu anapokatia katia nyama mbichi kabla ya kuchoma, ndipo tena anaweka nyama iliyokwisha chomwa kabla ya kukusevia. Mwingine anapokea pesa na kurudisha chenji halafu anaendelea kukuhudumia bila ya kunawa mikono.
Wala sipingi,wana mengi hao wala hawajaonewa
 
Si hivyo tu. Utaenda kwa mama ntilie au muuza chipsi,utaona jinsi anavyojitahidi kufanya jambo subtle kuchafua chakula chako .
Yaani inabidi umuangalie kwa makini kama unavymwangalia yule mchezeshaji kamari ya karata tatu.
Yaani you have to beware of sleight of hand.
Watu hawana dini!
I would like to know more of “watu hawana dini”.

Can i?
 
Ni vile nchi yao ndogo tu sasa ikiwa chafu wangekuwaje? Ila tangu nakua watu wachafu walifananishwa na wanyarwanda, nimekua nikabahatika kuishi nao hao watu ni wachafu na wavivu ovyo kabisa, mitandao inadanganya sometimes
 
Nilodhani
Hivi mabibi afya na mabwana afya nchi hii wapo kweli?

Ripoti ya wafaransa imeeleza Kwa kina mama ntilie Tanzania ni wachafu kuanzia kutooga, vyombo hawaoshi vizuri na ripoti imesema mama ntilie Tanzania ni sawa na mazingira ya kulelea watoto, yaani kwenye mama ntilie 10 basi saba huenda na watoto wadogo.

Rwanda kinara, imeonekana mama ntilie Rwanda wana usafi wa hali ya juu kuanzia mazingira hadi wao wenyewe, na wamepongezwa sana. Hivo tukaze buti ili mwaka mwingine walau tuongoze

Nilidhani kama umeenda huko Rwanda ukayashuhudia hayo kumbe umeona ripoti Tu? Shame on you
 
Kwa mama ntilie na hotel nyingi za bongo jagi linalotumika kunawaishia mikono linatumbukizwa kwenye maji machafu ya chombo cha kunawia na baadaye linatumbukizwa tena kuchotea maji safi ya kunawaishia kwenye ndoo, uchafu mtupu.
 
Hii nchi kinyume chake, ukiwa msafi sana watu around wanakuzodoa.

Wazazi hatufanyi kazi yetu ya malezi vizuri, kundi kubwa sana la watu ni wachafu, tatizo ninini?

Na WaTz sio wachafu wa mwili tu hata maadili, wachafu sana, tumejaaliwa tu kuongea taratibu, ukiongea taratibu utasikia fulani mstaarabu 😅😅😅
 
Back
Top Bottom