Mama Rwakatare anahaha kumuokoa Mch. Jean aliyekamatwa kwa Ubakaji!!!

Mama Rwakatare anahaha kumuokoa Mch. Jean aliyekamatwa kwa Ubakaji!!!

watu kama hao ndio wanaosababisha watumishi wa ukweli nao wadhaniwe kuwa ni fake.

yaani umeongea vizuri ndugu yangu ni kweli kabisa matendo ya baadhi ya watumishi yanarudisha nyuma kanisa,yanafanya watumishi wote waonekane fake,mungu tusaidie
 
Huyo kapiga anakashfa ya ushoga toka kitambo ss wasitutanie kutwambia ni mchungaji huo uchangaji kautoa wap?
 
Shetani yuko kazini, Kumbuka hata watumishi wa Mungu ni wanaadamu. We need to pray for them constantly that God may deliver them from the attack of the enemy. Biblia yasema Mungu anajua walio wake na kila alitajae Jina la Bwana na aache uovu.
 
tatizo lipo polisi kulea maovu
Zipo taarifa kuwa Mch
Jean Felix Bamana (DRC) (45) amekamatwa kwa Kwa jarida BNG/RB/862/2013
na IR682 ya tarehe 21 Feb,2013 kosa likiwa kumutoroshwa Mwanafunzi wa
St. Mary Goreth ambaye ni mtoto wa Swai na kufanya naye Zinaa kwenye
hotel ya GRAND Magomeni DSM huku bill zote zikilipwa na Mama Rwakatare
Mbunge Viti Maalum CCM.

Kukamatwa kwa Mch Jean kumetokea baada ya kupata sms za mapenzi
alizotuma Jean kwenda kwa mtoto huyo na kukutwa na baba yake Mzazi.

Polisi walipofuatilia simu ya Mch Jean wakakuta kuna mawasiliano ya Siri
na Mama Rwakatare wa Mikocheni B na Ushahidi huo ukatoa Mwanya wa
Kwenda Kanisani kwa mama Rwakatare ambapo alipohojiwa alikubali
kumufahamu Mch Jean na kwamba ni mgeni wake Maalumu na mhubiri wa
Kimataifa.

Hata hivyo imebainika kuwa Mch Jean amekuwa anafundisha semina ya
Ndoa na masomo ya Kichungaji kanisani Kwa mama Rwakatare.

Wafanyakazi wa Hotel ya Grand wamebainisha kuwa bill ya Mch Jean imekuwa
inalipwa na mama Rwakatare kwa mda wote huo sambamba na watoto wengine
wa Tz na Wakongo ambao wapo hapo wakisubili safari ya kwenda nje ambayo
inasukwa na Mch Jean na mama Rwakatare!!

Polisi walipo fika kanisani Mama Rwakatare ndiye alikwenda kumuchukua
mwanafunzi aliyetorshwa na kumuleta kanisani huku akiwasihi polisi
wayamalize matatizo hayo kifamilia.

Pia haikuweza kufahamika ni kwa nini Mama Rwakatare hakutaka Mgeni wake
huyo alale kwenye Jumba lake na badala yake anampeleka huko
NB.
Mwaka 2004 Mch Shansi kutoka DRC alikamatwa na kupigwa PI na serikali
baada ya kujificha kanisani kwa Mama Rwakatare huku akijihusisha na
Ujambazi na madawa ya kulevya hadi leo hakuna aliyejifunza.

Lipo sakata la Bi Maimuna ambalo nitaeleza baadaye ila kwa mara ya
kwanza naunga mkono kauli ya Rais Kikwete kuwa wapo Viongozi wa Dini
ambao wanajihusisha na madawa ya Kulevya.
 
Lile kanisa ni kichaka.ukichunguza kwa makini waumini wote maarufu na front liners pale utabaini kuwa kila mmoja wao kama hana kesi mahakamani basi ni mpigaji mkubwa hapa mjini,kama hilo halitoshi wapo wale fuata upepo wakiwaona wenzao na masuti ya gharama wanadhani ni upako kumbebjamaa walishaHOMOLA mahali
waumini wa kikristo mnabidi mjifunze historia za makanisa haya kabla hamjajitumbukiza humo
 
Shetani yuko kazini, Kumbuka hata watumishi wa Mungu ni wanaadamu. We need to pray for them constantly that God may deliver them from the attack of the enemy. Biblia yasema Mungu anajua walio wake na kila alitajae Jina la Bwana na aache uovu.

.
Rwekatare sii mtumishi wa Mungu. Biblia hairuhusu mwanamke katika ofisi ya kichungaji. Hivyo wale wote wanaoketishwa vitini na kusalishwa na mwanamke huyu mtaliki, wameangamia ikiwa hawataghairi uasi wao na kutubu kwa kuirejelea kweli. Chunguza katika biblia yote mwanamke pekee aliyeikalia ofisi ya kikuhani ni Yezebel tu na kazi yake kubwa ilikuwa kuwaajiri makuhani(manabii wa kisidoni) katika hekalu la Yerusalemu dhidi ya manabii wa kweli waliokuwepo Yerusalemu wakati huo. Vivyo hivyo na huyu Rwekatare ni wakala mzuri sana wa freemason. Ni kiungo muhimu sana ndani ya hii kada ya ma-dealers wa mjini Dar.
.
 
Kama hili ni kweli huyu mama anapaswa kujiuzulu kabisa na ubunge. Lakini pia ni kasoro kubwa kwa rais kudai kuna viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya bila kuwachukulia hatua. Alisha sema anaorodha ya watu hao. Mbona hawachukulii hatua? Rais wetu nae amekuwa mtu wa kulia lia kama tunavyolia au kulalamika sisi raia tusio kuwa na rungu la sheria.
 
Yanaongewa mengi sana kuhusu rwakatare, kuhusu huduma yake, kuhusu kuwa muuza unga, na pia umalaya. kuhusu huduma ni kweli anakiuka misingi ya biblia, lakini hayo mengine mawili yanahitaji ushahidi wa uhakika ndipo tuyaongee. Je kuna mtu mwenye ushahidi kuhusu rwakatare kuuza unga atuwekee? kuhusu kupenda dogodogo je? Ninadhani tukishajiridhisha na haya tuna haki ya kuongea kwa ujasiri wote
 
Tupa jela uyo anakula kondooo badala ya kuchunga
 
Huyu si ndiye alitamkwa wazi wazi bungeni kuwa MWIZI WA UMEME -TANESCO!pia magari yake ya shule hayana rangi za njano kama sumatra inavyotaka,pia kuna kesi nyingi kazizima za madereva wa school bus kubaka wanafunzi wanapowarudisha nyumbani,mwisho anasifa ya kuwa tapeli hapa dar ukifanya nae biashara imekula kwako
 
Yanaongewa mengi sana kuhusu rwakatare, kuhusu huduma yake, kuhusu kuwa muuza unga, na pia umalaya. kuhusu huduma ni kweli anakiuka misingi ya biblia, lakini hayo mengine mawili yanahitaji ushahidi wa uhakika ndipo tuyaongee. Je kuna mtu mwenye ushahidi kuhusu rwakatare kuuza unga atuwekee? kuhusu kupenda dogodogo je? Ninadhani tukishajiridhisha na haya tuna haki ya kuongea kwa ujasiri wote

Hivi pepo la Mchungaji linatolewa na nani ?
 
Mama Kokuu! Sitetei Kapiga, lakini ningeshauri kuwa wale wanaomtuhumu kuwa shoga wasemi lini walisikia ni shoga. Mimi nijuavyo YESU hubadilisha makahaba hata mashoga kuwa waumini wazuri. Husamehe wauaji na wanyang'anyi kuwa wema! Yumkini wale wamjuao Kapiga ni wale wa matukio ya zamani. Biblia inasema,...Tazama mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa KIUMBE KIPYA. Ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya. Kwa hiyo si ajabu huyo wa Clouds ni Kiumbe kipya na Kristo peke yake anaweza kumhukumu. Nani anafahamu kuwa Kapiga alishatubu na kusamehewa dhambi, isipokuwa Kristo mwenyewe? Ni nani anafahamu toba ya kweli ya Kapiga kwa Yesu Kristo? Simtetei kama anafanya uovu huo, lakini nachelea kumnyoshee mtu kidole wakati hufahamu mahusiano yake na Muumba wake!
Huyo kapiga anakashfa ya ushoga toka kitambo ss wasitutanie kutwambia ni mchungaji huo uchangaji kautoa wap?
 
Well said mkuu....
Mama Kokuu! Sitetei Kapiga,
lakini ningeshauri kuwa wale wanaomtuhumu kuwa shoga wasemi lini
walisikia ni shoga. Mimi nijuavyo YESU hubadilisha makahaba hata mashoga
kuwa waumini wazuri. Husamehe wauaji na wanyang'anyi kuwa wema! Yumkini
wale wamjuao Kapiga ni wale wa matukio ya zamani. Biblia
inasema,...Tazama mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa KIUMBE KIPYA. Ya
kale yamepita, tazama yamekuwa mapya. Kwa hiyo si ajabu huyo wa Clouds
ni Kiumbe kipya na Kristo peke yake anaweza kumhukumu. Nani anafahamu
kuwa Kapiga alishatubu na kusamehewa dhambi, isipokuwa Kristo mwenyewe?
Ni nani anafahamu toba ya kweli ya Kapiga kwa Yesu Kristo? Simtetei kama
anafanya uovu huo, lakini nachelea kumnyoshee mtu kidole wakati
hufahamu mahusiano yake na Muumba wake!
 
Mama Kokuu! Sitetei Kapiga, lakini ningeshauri kuwa wale wanaomtuhumu kuwa shoga wasemi lini walisikia ni shoga. Mimi nijuavyo YESU hubadilisha makahaba hata mashoga kuwa waumini wazuri. Husamehe wauaji na wanyang'anyi kuwa wema! Yumkini wale wamjuao Kapiga ni wale wa matukio ya zamani. Biblia inasema,...Tazama mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa KIUMBE KIPYA. Ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya. Kwa hiyo si ajabu huyo wa Clouds ni Kiumbe kipya na Kristo peke yake anaweza kumhukumu. Nani anafahamu kuwa Kapiga alishatubu na kusamehewa dhambi, isipokuwa Kristo mwenyewe? Ni nani anafahamu toba ya kweli ya Kapiga kwa Yesu Kristo? Simtetei kama anafanya uovu huo, lakini nachelea kumnyoshee mtu kidole wakati hufahamu mahusiano yake na Muumba wake![/QUOT

Umeongea point tupu.
 
Ndio maana mimi najiombea mwenyewe sitaki udalali wa imani mimi...
 
nijuavyo mm rais mweledi tunamwita 'A MAN OF ACTION' kama alivyofanya Mzee BENNY,sio rais hupenda kusemasema tu na wala hana uwezo wa kutoa maamuzi.
 
[h=1]Mchungaji asomewa mashitaka hospitalini[/h]




MCHUNGAJI Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo(DRC) Jean Felix Bamana (45) amesomewa mashitaka akiwa kitandani katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi mjini Moshi, akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha binadamu.
Mchungaji Bamana ambaye ni mlemavu wa miguu, aliibua mvutano mkubwa ndani ya Jeshi la Polisi na serikali, alikamatiwa jijini Dar es Salaam akiwa na watoto wawili ndugu ambao aliondoka nao mjini Moshi, kwa ahadi ya kwenda kuwatafutia shule.
Alisomewa mashitaka hospitalini baada ya kugoma kupelekwa mahakamani tangu jumatatu wiki hii akidai ni mgonjwa huku askari wanaomlinda wakilalamika kuwa anafanya mchezo wa kuigiza.
Mshitakiwa huyo alisomewa mashitaka mawili ambayo yanaangukia kwenye sheria ya usafirishaji binadamu namba 6 ya mwaka 2008,mashitaka ambayo hayana dhamana hivyo kupelekwa rumande katika gereza kuu la mkoa wa Kilimanjaro la Karanga.
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya,Naomi Mwerinde,mshitakiwa huyo anadaiwa kuwa mnamo Februari 18 mwaka huu huko Masama wilaya ya Hai,alimsafrisha(Jina tunalo) kwenda Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na wakili wa serikali,Stella Majaliwa,mshitakiwa huyo pia anashitakiwa kwa kumsafrisha (jina tunalo) kutoka Masama wilaya ya Hai Kwenda Jijini Dar es salaam kosa ambalo lilitendekea .
Baada ya kusomewa mashitaka hayo mshitakiwa alikana na iliamuliwa apelekwe katika mahabusu ya gereza la Karanga na hadi waandishi wanatoka katika wadi namba moja ambako mashitaka hayo yalisomwa,alikuwa bado hajaondolewa.
Kesi hyo imeahirishwa hadi machi 27 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa kutokana na upelekezi wa shauri hilo la jinai namba 13 la mwaka huu kutokamilika.
Kabla mahakama haijamalikiza kazi katika Hospital hiyo,mshitikiwa alilalamika kutokuwapo na huduma za vyoo vinavyokidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu ndnai ya wadi hiyo na hata alipokuwa akitaka kituo kikuu cha polisi mjini moshi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusomewa mashitaka hayo,mchungaji Bamana anayehudumu katika kanisa la Mikocheni B Assembles of God,aliwataka waandishi wa habari kuwasilisha kilio chake kwa mamlaka zinazohusika ili tatizo hilo la kutokuwapo na vyoo vya kukaa katika wadi hiyo liweze kutafutiwa ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom