jamani hamjui kuwa siku za mwisho kutakuwepo na manabii wa uongo, wenye kupenda pesa na kujisifu na kiburi, ambao katika hao wamo wajiingizao kwa siri ili kuharibu kanisa la Mungu na kuwauwa kiroho kondoo wa Bwana?
Hamjui kuwa ndo siku zimekaribia za mpinga kristo kutawala dunia hii yote muonayo ni dalili tosha ya mambo yanayokuja.
Wewe uliona wapi kwa mtanzania wa kawaida hasa mchungaji kumiliki jumba la kifahari namna ile itadhani ikulu ya marekani, uliona wapi kumiliki shule na vitu vikubwavikubwa lukuki kiasi kile ambacho inatubidi tushangae na kubaki midomo wazi kama sio kujifunika na shuka la dini kumbe kuna siri nzito humo? Mungu ameamua kufichua na kuandika moja baada ya jingine ipo siku mtamjua mtumishi wa kweli na yule asiye wa kweli yaani MNUFAISHAJI BINAFSI