Nyota Njema
Senior Member
- Nov 18, 2010
- 148
- 16
Mimi pia huwa napata wasiwasi na huyu mama, kama kweli yeye ni safi basi atakuwa alidandia treni kwa mbele wakati iko kwenye kasi kubwa. Ninachoamini mimi ni kuwa mtu mwenye dhamira safi kabisa, na anayeangalia kwa upana mkubwa namna ya kumkomboa mtanzania wa leo hawezi kuwa ndani ya CCM kama hana maslahi yake binafsi anayotaka kuyalinda kwa kujenga urafiki na utawala mbovu uliopo hivi sasa.
Mama huyu ni mfanyabiashara mkubwa mbali ya kuwa mchungaji, amewahi kulalamikiwa kuhusiana na kubebwa na mamlaka kutokana na nguvu kubwa ya kiuchumi aliyonayo pale alipokuwa ananyang'anyana viwanja vya kujengea shule yake mojawapo dhidi ya wananchi waliokuwa hawana uwezo. Sijui hilo sakata liliishia wapi.