Mama Rwakatare ni Mtakatifu au Mtakavitu?

Mama Rwakatare ni Mtakatifu au Mtakavitu?

Mimi pia huwa napata wasiwasi na huyu mama, kama kweli yeye ni safi basi atakuwa alidandia treni kwa mbele wakati iko kwenye kasi kubwa. Ninachoamini mimi ni kuwa mtu mwenye dhamira safi kabisa, na anayeangalia kwa upana mkubwa namna ya kumkomboa mtanzania wa leo hawezi kuwa ndani ya CCM kama hana maslahi yake binafsi anayotaka kuyalinda kwa kujenga urafiki na utawala mbovu uliopo hivi sasa.

Mama huyu ni mfanyabiashara mkubwa mbali ya kuwa mchungaji, amewahi kulalamikiwa kuhusiana na kubebwa na mamlaka kutokana na nguvu kubwa ya kiuchumi aliyonayo pale alipokuwa ananyang'anyana viwanja vya kujengea shule yake mojawapo dhidi ya wananchi waliokuwa hawana uwezo. Sijui hilo sakata liliishia wapi.
 
ni mtakavitu maana Ubunge Yeye, Viwanja Yeye, Siasa Yeye, dhuruma Yeye, Kukosa Mumu yeye, Pesa na Madhhabu Mwili Mzima Yeye, he?
 
jamani hizi hoja nyingine tunaweka tuuuuuuuu . JF Kinakua kijiwe cha kuongelea watu :A S-confused1:
 
Huwa nawaza pamba anazopiga akiwa madhabahuni pale kama Yesu anageshuka ghafla naona anagetafuta pa kukimbilia.
Ata sijui huwa anaihubiri biblia gani iyo
 
jamani hizi hoja nyingine tunaweka tuuuuuuuu . JF Kinakua kijiwe cha kuongelea watu :A S-confused1:

Jamaa katoa dukuduku lake, we unakimbilia kusema ni umbea...!!

Ameuliza Rev Mama Lwakatare ni mtakatifu au Mtakavitu? Cha muhimu hapa ni kujibu kwa hoja (substantiate) kwa wewe unavyomfahamu kiundani na si kukimbilia kusema jamaa kaleta umbea!! kama ndo hivyo basi hata kumzungumzia ama kumhusisha EL na Dowans, JK na mafisadi, Ngeleja na siasa za Tanesco, Chenge na Radar, Mataka na Wikileaks na memngine mengi ni umbea!

Haya mambo yote yana maslahi ya umma ndani yake, so haiwezi kuwa umbea. Mfano,

1. Unajua kwamba Mama Lwakatare anaingiza vitu nchini bila kulipa kodi kwa kisingizio cha kanisa?

2. Je anawezaje kutumikia watu kiroho (Uchungaji) wakati huo huo anahusika kuchakachua kura ili CCM iweze kushinda?

3. Sadaka zinazotolewa pale kanisani zinaenda wapi? Je zinatumika kueneza neno la uzima na kusaidia wasiojiweza kama ilivyoandikwa kwenye Biblia Takatifu au zinaenda kutunisha mfuko wake binafsi?

4. Kama zinaenda kutunisha mfuko wake binafsi basi anastahili kulipa kodi (PAYE) kwa sababu sadaka zinazotolewa pale ni personal income yake.

5. Wakati JK na Makamba akimpiga dongo Askofu Kakobe kuchanganya dini na siasa, mbona wako kimya kwa Mchungaji mama Lwakatare (ambao wao CCM wamefikia hatua ya mpaka kumpa ubunge)

6. Nini changamoto tunazopata kama taifa kwa viongozi wa dini kujihusisha moja kwa moja na uongozi wa kisiasa (kofia 2 kwa wakati mmoja) hasa tunapoelekea kuunda Katiba mpya ya JMT?

Kwa hiyo mi nadhani mtoa hoja hajaleta umbeya jamvini, ni mada nzuri na yenye changamoto kwa Taifa.
 
jamani hizi hoja nyingine tunaweka tuuuuuuuu . JF Kinakua kijiwe cha kuongelea watu :A S-confused1:
Kwani kuongelea watu hadharani hivi ni kosa? nyie ndio mnadhani mkiongelewa ni kijiwe, lakini kadri tunavyowaongelea ndivyo tunavyowajua. Ukisha kuwa public figure ujue utaongelewa tu mwenzangu! usiwazuie watu kuongea wacha waongee. Ukikelwa ondoka nenda kwa position nyingine ziko position nyingi tu humu ndani ya JF.
 
Brooklyn,

Umeeleza kwa vizuri nadhani kila mmoja ataelewa,

Ukiingia kwa ndani itakuwaje ikitokea Rais kachaguliwa af anateua wabunge wa viti maalumu wote wachungaji au mashehe halafu hao hao awape uwaziri! Hii kitu inasound vipi?

Kwa jinsi hali ilivyo hata leo, Rev Rwakatare anaweza kikatiba kuwa hata waziri-discuss!

Kama ni mfanyabiashara je inawezekana vipi kutofautisha mali ya kanisa au kibiashara kama si kukwepa kodi kwa mgongo wa kanisa?

Kiimani pia inaruhusiwa kukitumikia chama kama CCM 100% kichaka cha wezi aka(Watakavitu) af hapo hapo kutumikia kanisa 100% ulokole aka (utakatifu)

Kuna umuhimu wa kumchambua huyu mdini mwanasiasa ambaye mimi sijaelewa kama ni mtakavitu au mtakatifu
 
How could you people dare to give this business woman-politician a REVERAND title??
 
Huyu Mama ni MATERIALIST kwa sababu zifuatazo:
(i) Kwenye kanisa lake kuna special preference kwa watu wenye uwezo
(ii) Make up kali anayofanya ni manifestation ya materialism na ni typical kwa makanisa feki ya uamsho ya Marekani
(iii) Dini, biashara na Siasa haviendani: Haiwezekani kutumikia vyote na ukijaribu, dini lazima itakuwa compromised. Biashara na Siasa vinaendana na materialism
Kwa hiyo yeye ni MATERIALIST.
 
Imewahi kuelezwa hela alizo nazo alipewa kutoka ulaya baada ya kuandaa proposal ya kuanzisha shule za ada nafuu
kwa watu wasiojiweza lakini sidhani kama shule zake ni za ada nafuu,kama ni kweli yeye ni mtakavitu ingawa tunaambia tusihukumu! Lakini ni vema tuseme
 
Huyu mama ana nguvu za kitakatifu. Niliona kwenye TV live akimponya binti mmoja aliyekuwa na mashetani. Pia anaongea na anauwezo wa kuyaita majini yaliyomo ndani ya mtu. Si hivyo tu pia anayatoa na binti anapona. Hii yote live kwenye tv mbele ya maelfu ya wauminil. Ananguvu za roho mtakatifu. Mimi binafsi sina majini na siyajui, ila ningekuwa nayo ningemtafuta.
kumtoa mtu mashetani sio kigezo mtu wangu kwani kuna watu wengisana ambao wanafanya hayo mambo na si watakatifu hata kidogo, tukubali tu huyu mama ni mtafutaji kama wewe, ila kila mtu ana style yake ya utafutaji, tujifunze jamani na tumuogope Mungu jamani kwa kuwapa watu utatifu kwani hatujui la moyoni mwake na anafanya nini Nyuma ya pazia.
 
Hivi mmeshawahi kuingia kanisani kwake? Viti vya mbele vinatengewa wale vigogo na watu wenye fedha tu. Pia sijawahi kuona siku ametangaza sadaka amepata kiasi gani bali huwa anatangaza tu wale walio toa fedha nyingi kuanzia laki moja na kuendelea. Michango huwa ni zaidi ya mara 4-6 katika ibada moja ya jumapili.

Huduma ya maombi na kumuona huwa inatolewa kwa wale walio na fedha tu, watu wa kawaida huwa hawaruhusiwi kumuona huyu mama.

Wakati wa harusi ya mwanae watu walichangishwa kwa nguvu tena kwa vitisho huko kanisani kwake. Mimi nipo so conviced kwamba huyu mama ni mtakavitu...!
 
Duh! Hakika huyo ni Mtakavitu na si mtakatifu
 
Ninavyoamini mimi, wachungaji ni watu maalum katika jamii ambao wamejaliwa kuwa viongozi wetu wa kiimani....nimesoma kwa mshtuko from some newspapers that mchungaji mama Getrude Rwakatare (MB), amedanganywa na vijana, tena wadogo mno kiumri (7-10 yrs), waliojifanya ni wachawi waliodondoka toka safari zao

...eti cha kushangaza zaidi, ilibidi ipigwe ibada ya nguvu kuwaombea!

Utata ninaopata mimi, na ninaomba wadau wenzangu mnisaidie ni kwamba, je mama Rwakatare alishindwa kutumia nguvu za kiroho alizonazo kutambua kwamba those guys were con-men? Uko wapi mpako wa roho mtakatifu kwa mchungaji wetu? haya, kazi kwenu, tudanganyeni tu!!!??

hawa vijana (wachawi) sio kwamba huwa wanawapandikiza wenyewe wachungaji ili kuvutia waumini!
 
Kabla ya kutoa kibanzi katika jicho la mwenzako, toa kwanza boriti katika jicho lako. Mbona macho yenu yamefunguka sana kuangalia ya wengine nyie wenyewe mko safi ili muwe na haki ya kuwahukumu wengine? Msijichukulie hukumu isiyokuwa yenu kwa jambo ambalo mhukumu wake yuko tayari na ujira wa kila mmoja mkononi mwake. Kama ukiona huduma ya huyu mtumishi haikubariki muombee tafuta mahali pengine na uendelee kumuombea badala ya kuweka mjadala wa kumchafua Mungu ukifikiri unamchafua mwanadamu kwa sababu hakuna hata mmoja ambaye ana uhakika na yale anayoyasema kwamba huyu mtumishi hatumii nguvu za Mungu. Suala kwamba mama huyu anatafuta kitoweo ni vema kuwa na uhakika juu ya yale tunayoyasema kwa kuwa kila mmoja atatoa hesabu ya kila neno analolinena kwa kinywa chake. Je kati ya mali alizo nazo huyu mama na huduma ya kanisa ni kipi kilianza. Siko hapa kumtetea kwa kuwa hajaniweka kuwa wakili wake lakini tunaponyoonshea wengine kidole tuangalie vitatu vinaelekea wapi. Tuache kuhukumiana yapo mengi sana ya kujadili katika hii nchi hii, ya Mungu tumwachie Mungu mwenyewe.
 
Yawzekana ni mtafutaji, hatahivyo hazuiwi kutafuta kwani ataishije asipotafuta, ila swala la mchungaji kugundua liko tofauti kidogo, mchungaji sio kama mganga wa kienyeji kwamba mtu mteja wake akifika tu anaanza kumtajia matatizo, la bali watumishi wa Mungu huliweka hitaji mbele za Mungu hata kama wamehisi kitu flani huiombea na kupata jibu sasa sio tu kwa hivihivi ndo maana ya utumishi lazima utumike kimaombi.
 
Back
Top Bottom