Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete akiwa Rais ajaye sitashangaa

Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete akiwa Rais ajaye sitashangaa

Agombee kwanza ubunge wa jimbo, akifanikiwa apewe wizara ya mambo ya nje. Hivi anayo shahada yoyote (hitaji la katiba kuwa Rais)
 
Natazama hapa mahojiano Mubashara Clouds TV kipindi cha 360 wakimuhoji huyu Mbunge na Mhe 1st Lady Mstaafu.

Ukweli ni kwamba ametulia sana akijieleza kama Mwalimu wa hesabu shule ya Msingi alieendelea kufundisha ata Mume wake alipokuwa Waziri.

Mara zote anasisitiza kuhusu malezi ya Familia ndio msingi wa maendeleo ya Taifa endapo jamii itazingatia kuwa watoto ni wa jamii nzima kwa kauli mbiu kuwa "MTOTO WA MWENZIO NI MWANAO,MLINDE"
Tukijenga watoto wenye nidhamu na adabu Taifa litaendelea

Mama huyu kumbe ameanzisha shule mbili za sekondari Wama Nakayama -Nyamisati na WamaSharifu -Lindi zilizoongoza kimkoa zikisomesha watoto wakike bure na wakipewa kila kitu muhimu.

Uongozi wa kijiji toka nchi nzima unakaa nakipitisha mtoto wa kike aliemaliza darasa La saba ambae ni yatima ama anaishi mazingira magumu bila kujali kabila lake wala Dini yake

Shule inamchukua anaishi shuleni hadi anapomaliza na ikibidi kwenda likizo anapewa nauli ya kwenda na kurudi na akifika kijijini anapokelewa na uongozi wa kijiji unaopewa jukumu la kumlinda

Baadhi ya mabinti waliopitia shule zake wameshahitimu vyuo vikuu na wapo makazini sasa.

Ukifatilia siasa za nchi zilizoendelea Mara nyingi wagombea Urais wa nchi kama Marekani wamekuwa wakielezea Sera zao katika kushindana nani akipewa nchi watoto na familia zitakuwa bora zaidi,kumbuka ile hotuba ya Obama maarufu alivyozunguzia mambo ya uzazi,bima ya matibabu ilivyompa umaarufu.

Kuwa Wamarekani wanachagua Rais ambae wanauhakika watoto wao watakuwa salama na watatimiza Malengo yao.

Katika dunia tuendayo lazima kuamini kuwa siku moja nchi yetu itaendeshwa na Mwanamke kwa kuwa Wanawake wanahaki hiyo,wanahuruma na ndio Mama zetu,Sasa tuna makamu wa Rais, basi ipo siku tutapata Rais MwanaMama

WANAWAKE WANAWEZA hasa unapokuwa na Mwanamke ametulia kama Mama Salma Kikwete ambae ni Mwalimu na Tayari ameishi Ikulu kwa Miaka 10

Hongera sana Mama Salma Kikwete,baada ya Rais wetu wa sasa kumaliza Miaka 10 yake,Mwenyezi akikusaidia ukiwa Rais wetu sitashangaa zaidi ya Kukuombea Mungu uwe kiongozi wa busara zaidi ya Zile za Mzee Jakaya.

SITASHANGAAAAA.

View attachment 1332733View attachment 1332734

Sent using Jamii Forums mobile app

Tumekuwa vichwa panzi kweli kweli siku hizi 😂
 
Una wivu??ndio maana Marekani wanachaguaga baba na mtoto kuwa marais maana wanajua wizi unapungua na ni rais watu kupata elimu ya Urais
Mfano G W Bush atakuwa alipata msaada mkubwa wa mambo kwa babake ambae alisha wahi kuwa Rais

Uingereza
Wanamalkia yani familia moja inaongoza nchi miaka yote hii inapunguza gharama na watu kuja kwenye cheo kikubwa kama cha urais kujaribu uongozi

Sasa hapa kwetu masikini lakini tunalikataa hilo asikwambie mtu kunagharama kubwa sana kutengeneza Rais mpya na si chini ya miaka 3 ya madarakani ndio mtu anajua na kuzoea...

Angeshinda Hillary isingesumbua sana kwa kuwa Bill yupo nyuma anajua itifaki zote sasa umeona kinachotokea kwa Trump

Hapa naelewa kwann nchi zingine zinamfumo wa ufalme na usultan

Angalia Oman no gharama za uchaguzi wala masiasa.
Kafa mtu anapanda mtu usiku huo huo..

Kwa kuwa serikali inaendeshwa kwa mifumo
Rais kama mfalme ama sultan anakaa kuiboresha tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijaelewa uhusiano wa post yangu na post yako
 
Back
Top Bottom