Mama Samia ameanza vibaya kwa kupuuza kuvaa Barakoa

Mama Samia ameanza vibaya kwa kupuuza kuvaa Barakoa

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2007
Posts
1,117
Reaction score
4,772
Tarehe 19.05.2020 wakati Tanzania ikikabiliwa na wimbi la kwanza la janga la korona, nilichapisha uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu mustakabali wa urais wa Magufuli kwa jinsi "alivyozembea" kushuguhulikia janga hilo. Na katika kuhitimisha uchambuzi huo wa kurasa 23 nilibashiri kuwa janga hilo lingegharimu urais na uhai wake. You know the rest of the story. Kanuni za JF zinakataza kuweka links, otherwise I would have shared (it's a free ebook anyway).

But I'm not here to take credits bali kutanabaisha kuwa I am disappointed kuona Mama Samia akiendeleza "ubishi" wa mtangulizi wake katika handling ya janga hilo. I know mie si mtu sahihi kumshauri Rais wetu lakini yeye na takriban kila Mtanzania anafahamu vizuri the price late Magufuli paid kwa negligence kwenye kushughulikia janga hilo. As much as nisingependa kuwa "prophet of doom," Mama Samia anapaswa kuchukua hatua sasa, vingenevyo...

Pongezi nyingi kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa "kuonyesha uongozi licha ya kuwa mstaafu."

jk.jpg


Na pongezi pia kwa mama Janeth Magufuli ambaye leo amewasili Dodoma akiwa na barakoa.
mama janet.jpg


Mama Samia anapaswa kuelewa kuwa licha ya dunia kumwangalia kwa makini endapo atachukua hatua stahili kuinusu Tanzania dhidi ya janga hilo, lakini pia anaangaliwa na mamilioni ya Watanzania kuwapa leadership katika kuikabili Korona.



Kuna watakaosema ni mapema mno "kulaumu," lakini when it comes to COVID, timing is everything.

I'm not expecting much from her, kwa sababu tatizo zaidi ni CCM na sio mtu gani anaongoza nchi, lakini hili la barakoa lipo ndani ya uwezo wake.

I stand to be corrected.
 
Oya ulijuaje mzee wetu kavuta kabla hata ya kuwekwa public?
 
Kwani ndio leo ameanza kutokuvaa barakoa?
Nikweli hajaanza leo kutovaa barakoa mama D, lakini hata akianza leo sio mbaya, hali huku mtaani sio nzuri, najua wao wanajua zaidi yangu hali ilivyo lakini wanasababu zao ambazo gharama zake zimefikia pakubwa, Mama Janet sio mjinga, naamini hapo kuna ujumbe ametuma.
 
Kwani ndio leo ameanza kutokuvaa barakoa?
... inawezekana yeye Mh. Rais ana kinga dhidi ya Corona but as a leader anatakiwa kuonesha uongozi dhidi ya Corona kunusuru mamilioni ya watanzania wengine ambao pengine hawana kinga kama zake. Kinachoonekana ni kuipuuza Corona na, as an icon, wengine watamwiga na kuishia kuteketea!
 
Usiwachoshe waombolezaji kwan kaanza leo kutokuvaa? ? Mama kajifukiza inatosha msilazimishe tuamini tiba za wazungu.

Lemme remind you Mr Fugitive modern war is all about infiltration, invasion is no longer a theme....as long as Double S won't step on their interests we all know Corona sio weapon😉.

Have a cup of tea....
 
Group linalomzunguka ndio linampumbaza namshauri alitimue lote... Akae sana na Kikwete atamsaidia Kikwete hajawahi Shindwa vita yeyote even Marehemu alimtafuta sana akaambiwa utaondoka wewe Jk Mtoto wa Mjini
 
Hayati JPM hakukataza watu kuvaa barakoa, bali alisisitiza tuwe makini na hizi imported stuffs pía ikiwezekana tutengeneze nyenzo zetu wenyewe

Rejea speech yake ktk msiba wa The Late John Kijazi pale Karimjee
 
Evarist Chahali Kama hofu yako ni maambuki ya COVID 19 fanya kitu chochote kilicho ndani ya uwezo wako kutoa suluhu kwa hao watanzania unaowaongelea hapa akiewemo rais wetu. Kumbuka hakuna rais wa nchi bila wananchi

Na nikukumbushe makusanyiko ya watu bila barakoa wala sanitzer yapo nchi nzima. Hata ukimuuliza Tundu atakuambia alikua anaingia hadi kariakoo bila barakoa.

Labda sababu wewe na ukoo wako mnaishi ughaibuni ndio maana hujui. ila kama una ndugu huku waulize vile wanaishi watakusaidi labda ili uweze kulisaidia taifa lako

Kama nia yako ni COVID 19 acha kulalamika fanya kitu chochote kilicho ndani ya uwezo wako kutoa suluhu kwa hao watanzania unaowaongelea hapa.

Na kwa msaada zaidi nikukumbushe makusanyiko ya watu bila barakoa wala sanitzer yapo nchi nzima.

Labda sababu wewe na ukoo wako mnaishi ughaibuni ndio maana hujui..... ila kama una ndugu huku waulize vile wanaishi watakusaidi labda ili uweze kulisaidia taifa lako


Hii ni Kawe leo




Hii ni Mwenge leo




Kariakoo 5 months ago







Hii ndio hali halisi
 
Tarehe 19.05.2020 wakati Tanzania ikikabiliwa na wimbi la kwanza la janga la korona, nilichapisha uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu mustakabali wa urais wa Magufuli kwa jinsi "alivyozembea" kushuguhulikia janga hilo...
NIT- PICKING
 
Back
Top Bottom